TFF wamebeba ushauri wa Sammy Hyppia bila kwanza kuangalia mazingira ya soka letu. Kwa muda mfupi ujao tutapata taabu na soka letu lakini faida yake tutaiona baada ya miaka mingi sana ijayo tutashuhudia soka letu likipanda rejea kilichoikumba Uingereza miaka mingi iliyopita kabla ya siku za karibuni kuanza kufanya vizuri kwa timu zake za vijana na hata ya wakubwa kwenye world cup. Na hii inatokana na kanuni za mabadiliko yoyote duniani kuwa huwa na athari mwanzoni lakini faida huja baadae. Kwa kizazi cha baadaye kitakuja kukutana na haya mabadiliko bado wakiwa wadogo hivyo watapambana sana ili kwenda sambamba na wageni. Hiki kizazi cha sasa cha akina Ndemla, Makapu, Muzamiru, Pato Ngonyani n.k badala ya kupambana chenyewe kinaridhika kukaa benchi mpaka mtu aumie au huruma ya kocha imkute. Namwangalia kwa jicho la tatu mchezaji kama Gyan. Alikuwa benchi muda mrefu mpaka aliwekwa kwenye listi ya kuachwa kwenye usajili lakini alipopewa nafasi moja tu ya kucheza tena beki na sio nafasi yake ya ushambuliaji hakufanya makosa na kila mpenda soka anamjua sasa Gyan ni nani. Lakini tujiulize huyu Ndemla, Ajibu, Ramdhani Singano, n.k. kwa nini soka lao linapanda na kushuka kila siku kama homa na tunatatuaje hili tatizo? Jibu ni moja tu turuhusu ushindani lakini wenye mipaka. Turuhusu wasajiliwe wachezaji wa kigeni 10 lakini wanarohusiwa kuwa uwanjani wakati wa mechi wawe watano tu basi inatosha. Nina hakika watakuja wakina Chilunda, Zaidy, Rashid Juma, Maka Edward wengi tu wa kupamabana na akina Kagere. Mimi kama mpenda maendeleo ya soka namuomba waziri Mwakyembe aingilie kati hii kanuni ifanyiwe marekebisho kabla ligi haijaanza - sajilini kumi lakini watano tu wawe uwanjani kwa wakati mmoja hii ni kwa ajili ya kulinda wachezaji wetu na timu ya taifa kwa ujumla.