Wachezaji 20 Simba SC waondoka nchini kuelekea Alexandria Misri kuifuata Al- Ahly

Wachezaji 20 Simba SC waondoka nchini kuelekea Alexandria Misri kuifuata Al- Ahly

Wakifungwa siku waki rudi bongo tunawapiga mawe sasa
 
Soma hiyooooo
50218048_366839840771740_2101282998329540608_n.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni hivyo punguza ukali wa vitisho, mpira ni mchezo wa makosa, wale Nkana hawakupenda kutoka katika michuano hiyo mkuu lakini imewabidi kutokana na makosa yao

Wape nguvu, Hima, na Ushauri..SimbaNguvuMoja

Sent using Jamii Forums mobile app
Nisawa ila kama ni kuwapa moyo tumewapa ili nguvu ya mashabik ibaki kiukweli hii game ya Jumamosi wakaze sana maana ukiangailia kunamashabiki baadhi washaanza kukata tamaa kabsa
 
Msafara wa klabu ya Simba SC, Mnyama ukiwa na wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi umeondoka nchini leo Januari 29, 2019 kuelekea nchini Misri tayari kuwakabili klabu ya Al-Ahly kwa mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa inalezwa kuwa msafara wa Simba SC utapitia Addis Ababa nchini Ethiopia na kisha kuelekea mjini Alexandria nchini Misri ambako mchezo huo utachezwa siku ya Jumamosi Februari 2, 2019.

Katika hatua nyingine klabu ya Simba imemteua Patrick Rweyemamu kuwa meneja huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Abbas Ally akitakiwa kuendelea na majukumu yake ya awali kama mratibu wa timu.

This Is Simba Sports Club NguvuMoja

View attachment 1007942

Sent using Jamii Forums mobile app
Timu imeondoka kimya kimya, sio kama raundi zilizopita. Afadhali Manara kapigwa breki. Huwaweka wachezaji under pressure.
 
Back
Top Bottom