Wachezaji Bongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kwenye soka

Christopher Alex Massawe
 
Katika waliocheza Soka la muda mrefu umemsahau Kiungo wa Mtibwa Henry Joseph Shindika, na mwenzie Monja Liseki ingawa huyu nadhani hayuko sasa.
 
Alikwenda kucheza soka nje ya nchi. Kuna layer fulani ya wachezaji wa Yanga waliindoka kimya kimya, nakumbuka katika kundi hili alikwepo pia somebody Credo Mwaipopo.
 
Record zangu zinaonyesha mchezaji aliyevuma na kuporomoka kwa muda mfupi sana ni.MOSES GODWIN MWAZEMBE huyu bwana mdogo alicheza mechi tatu tu za ligi kuu akiwa pale Simba sports club alifanikiwa kufunga goli moja tu.

Mwalimu Maxio Maximo alimuona bwana mdogo huyu mara moja lakini hakubahatika kucheza hata mechi moja, baada ya dogo huyu hajawahi kusikika popote hata kwenye dondo alikuwa brilliant sana akiwa na mpira sema ndiyo dogo kupotea mazima kwenye soka.

Matukio yote haya yalifanyika ndani ya mwaka mmoja tu sijui nini kilimpata Moses.
 
Steven Mazanda - Mbeya City
Hujamtendea haki Steven Mazanda,kumbukumbu zangu zinaonyesha Steven mazanda aliichezea Moro united kwa misimu mitano mfululizo mpaka iliposhuka daraja mwaka 2010 kama sijakosea.

Steven Mazanda walitengeneza ukuta mgumu sana pale Moro united akicheza pamoja na Samson Mwamanda moro united hii iliundwa na wachezaji mahiri sana
1 Shaban Mkongwe
2 Steven Mazanda
3 Mashaka Jumanne
4 Ally Yusuf Tigana
5 Julius Mrope
6 Ivo Mapunda
8 Aman Simba
Etc
Chini ya mwalimu John Simkoko baadae akaja James Siang'a Moro united wakashika nafasi ya pili ligi kuu kwenye mashindano ya CAF walitolewa na Experance de Tunis kwa aggregate 4:2

Mwaka huo huo walifika finali ya kombe la Kagame wakafungwa na Polisi ya Uganda iliyokuwa ikiongozwa na Sam Timbe, katika dakika za nyongeza.

Mazanda alienda Mbeya city baada ya Moro united kushuka daraja kikawaida huyu jamaa alidumu kwenye soka kwa muda mrefu tu.
 
Emanuel Gabriel
Yusuf Macho
Christopher Alex
Steven Mapunda
Amri Said
Said Sued
Ulimboka Mwankingwe japo aliposajiliwa baada ya simba kumtoa Zamaleck
Primus Kasonso
Nteze John Rungu
Mohamed Athuman Machuppa
Patrick Betwel
Ramadhan Wasso

Unanikumbusha viumbe kama Boniphace Pawasa, Emmanuel Gabriel, Suleiman Matola, kocha James Siang'a, daa walikuwa ni moto wa kuotea mbali aise

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…