Wachezaji Bongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kwenye soka

Wachezaji Bongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kwenye soka

Pale Mtibwa Sugar, kuna nahodha kiongozi Shaban Nditi. Amecheza soka la kiwango cha juu kwa muda mrefu bila kuchuja. Amedumu sana kwenye soka la ushindani hapa Bongo.

Ukifika kwenye kikosi cha Kagera Sugar wanankurukumbi, utakutana na George Kavila Master. Ni karibia miaka 20 sasa anacheza ligi kuu ya Tanzania. Ni moja kati ya wachezaji wakongwe na wenye nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya uwanja.

Lakini habari ni tofauti kwa baadhi ya wachezaji wengine. Kuna wachezaji wa kibongo waliovuma kwa muda mfupi kisha wakapotea kabisa katika ramani ya soka.

Leo, tujikumbushe list ya wachezaji hao.

Mimi naanza na hawa wafuatao...
Rashid Gumbo

Said Bahanuzi

Jerry Tegete

Endelea na wewe...

Sent using Jamii Forums mobile app
Edward Christopher wa simba
 
Chibe Chibe Chibindu na SAMSON MWAMWANDA waliisha ndani ya msimu mmoja tu pale Jangwani baada ya kufanywa kitu mbaya na Machupa.
 
Record zangu zinaonyesha mchezaji aliyevuma na kuporomoka kwa muda mfupi sana ni.MOSES GODWIN MWAZEMBE huyu bwana mdogo alicheza mechi tatu tu za ligi kuu akiwa pale Simba sports club alifanikiwa kufunga goli moja tu.

Mwalimu Maxio Maximo alimuona bwana mdogo huyu mara moja lakini hakubahatika kucheza hata mechi moja, baada ya dogo huyu hajawahi kusikika popote hata kwenye dondo alikuwa brilliant sana akiwa na mpira sema ndiyo dogo kupotea mazima kwenye soka.

Matukio yote haya yalifanyika ndani ya mwaka mmoja tu sijui nini kilimpata Moses.
 
Chibe alienda malizia soka lake bandari ya Mtwara, alikuwa anapiga majalo hadi sio poa. Alikuwa mtaalamu sana wa set pieces hususani kona.
 
Chibe Chibe Chibindu na SAMSON MWAMWANDA waliisha ndani ya msimu mmoja tu pale Jangwani baada ya kufanywa kitu mbaya na Machupa.

Daah lile goli lilikuwa hatari sana, Machupa alipokea mpira akiwa kalipa mgongo goli la Utopolo, kisha akafanya turn kama zile za akina Thierry Henry kisha aka-curve mpira wenyewe uswahilini tunaita akazungusha! What a goal! Afu kumbuka hapo shamba la bibi lilijaa tope baada ya mvua kunyesha sana!

Hao akina Mwamanda walistahili tu kutimuliwa
 
Back
Top Bottom