Wachezaji gani walistahili kutwaa Ballon D'or?

Wachezaji gani walistahili kutwaa Ballon D'or?

Hahahaaa imebidi nicheke tu, yani messi umlinganishe na hao!!!, ebu kuwa muwazi basi kamanda, hao wote ulowataja sio kweli....alafu nataka uniambie mwaka upi messi alidrop? Maana kuna kipindi aliumia na akakaa nje miezi kibao, na alivyorudi alikiwasha kama kawaida yake....
kwanza naomba utengue kauli sijamfananisha Messi na mchezaji yeyote, pili hiko wanachosema wachambuzi ni mawazo yao siwezi kuwapinga wanafacts zao kusema hivyo na mimi pia nna facts zangu na mawazo yangu, tatu, hakuna mwaka Messi aliumia akakaa nje kwa muda mrefu zaidi ya miezi mitatu kama upo huo mwaka nitajie.

hii ni miaka ambayo Messi alidrop nnaposema kudrop si kwamba hakuwa bora ila hakuwa bora kupita hao niliyowataja.
2010.....Sneijder alikuwa bora zaidi
2013.....Ribery alikuwa bora zaidi
2014.....Neuer alikuwa bora zaidi
2015.....Neymar alikuwa bora zaidi
2016.....Ronaldo alikuwa bora zaidi
2017... .Ronaldo alikuwa bora zaidi
2018.....Ronaldo alikuwa bora zaidi
 
Mwaka 2010 hadi Leo cjaamini kwamba Andres Iniesta hakuchukua hyo tuzo akaishia kupata Messi. Ili na wewe ushangae jaribu kucheki mafanikio yao kwa mwaka huo. Na iniesta alifunga bao hadi siku ya final ya world cup mwaka huo.

Na kuna mwaka hapa Africa Adebayo alipewa uchezaji bora Wa Africa kwa sababu alikuwa mfungaji bora ktk timu ya Arsenal hapo haikuchukua ubingwa, wakati opponent wake mmoja wapo alikuwa Mohammed Aboutrika akiwa Captain Wa Al Ahly, aliiongoza timu hyo kutwaa kombe LA klabu bingwa Africa, akiwa captain tena Wa timu ya taifa mwaka huo huo akaiongoza timu hyo kutwaa ubingwa Wa Africa na alikuwa mfungaji bora Wa mashindano. Mwenye kukumbuka vema mwaka na kisa hicho anikumbushe zaidi, mana niliumia sana.
Kwahiyo hata afrika ni figisu tu
 
Back
Top Bottom