Wakuu nimekutana na hii post, ina ukweli?
- Tunachokijua
- Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa orodha iliyotajwa ni ya kupotosha. Uchunguzi wetu mtandaoni, hasa kupitia mtandao wa YouTube, umeonyesha kuwa katika orodha ya wachezaji waliotajwa, wote wamewahi kufunga magoli isipokuwa mchezaji mmoja, ambaye ni Stuart Taylor aliyekuwa Mlinda Mlango. Ufuatao ni Uchambuzi wa kila mchezaji:
1. Gary Neville – Akiwa Manchester United, aliwahi kufunga goli. Mfano, alifunga goli lake la kwanza mnamo 3 Mei 1997 dhidi ya Middlesbrough. Angalia video hapa.
2. Franco Baresi (AC Milan) – Ingawa alikulwa beki maarufu wa AC Milan, Franco Baresi alifunga magoli zaidi ya 10 katika Maisha yake ya soka. Video hii imekusanya magoli 12 aliyoyafunga katika Ligi Kuu ya Italia Miaka ya 1980. Angalia video hapa.
3. Des Walker – Des Walker alifunga goli lake la pekee akiwa na Sheffield Wednesday, klabu aliyohamia baada ya Nottingham Forest. Pia alifunga goli moja dhidi ya Denmark wakati akiichezea timu ya Taifa ya Uingereza mnamo 11 Mei 1994 (Angalia video hapa).
4. Steve Potts (West Ham) – Steve Potts alifunga goli lake la pekee kwa West Ham United katika mchezo dhidi ya Hull City mnamo Oktoba 6, 1991. (Angalia video hapa).
5. Stuart Taylor – Huyu alikuwa mlinda mlango namba 3 wa Arsenal, vyanzo vinaeleza kuwa alicheza mechi 97 tu katika Maisha yake ya Soka la Ushinani (soma hapa). Aidha, vyanzo pia vinaonesha kuwa hakuwahi kufunga goli lolote katika Maisha yake. Hivyo, taarifa hiyo ni sahihi kwa mchezaji huyu.
6. Tony Hibbert ni mmoja wa wachezaji wa soka maarufu kwa kutofunga goli lolote katika michezo ya Mashindano akiwa na Everton. Hata hivyo, vyanzo vinaonesha mchezaji huyu amewahi kufunga goli moja katika mchezo wa mwisho ambao ulikuwa mechi ya kumuaga tazama hapa.
Kwa hivyo, ni upotoshaji kusema kuwa wachezaji wote katika orodha hiyo hawajawahi kufunga kabisa, kwani wanne kati yao wamewahi kufunga angalau goli moja katika taaluma zao