ngara23
JF-Expert Member
- Aug 31, 2019
- 9,091
- 21,087
Kweli wewe mbumbumbuAzam Media, LLC ndiyo inadhamini ligi. Hii ni kampuni. Azam FC ambayo ni kampuni tofauti inadhaminiwa pia na Azam Media kama ambavyo timu zingine zote zinadhaminiwa kwa mujibu wa kanuni za TFF. Azam FC ina wadhamini wengine kama ambavyo timu zingine zinafanya.
GSM anaimbwa Yanga inapofunga magoli, mbona haimbwi mdhamini mkuu SportPesa. Mnadhani mnadili na watoto wa chekechea?
Achana na mambo ya katiba, kwani katiba ya Yanga inatambua rangi nyeupe katika rangi za timu? Usifanye nikakuitia Mzee Magoma.
Swali linabaki pale pale, kama mnatuaminisha GSM siyo mmiliki wa Yanga, kwa nini mnatumia mfano wa Bakhresa ambaye mnaamini ndiye mmiliki wa Azam FC na anadhamini ligi nzima? Hamuoni kwamba mnajisnitch?
Kwaiyo unakataa kwamba Bakhresa haimiliki Azam media, Azam fc- na Azam beverages
Suala la kumuimba GSM mashabiki wa Yanga haihisiani kuwa anamiliki Yanga
GSM ni mfanyabiashara yupo Yanga kunufaika na Yanga inufaike
Kudhamini Yanga sio kifungo kwamba asijitangaze kwenye timu zingine
Matangazo ya GSM yapo kwenye magazeti, redio, Tv na mabango sio kwenye timu, yeye anatangaza biashara zake
Na nyie Simba kama mpo tayari kaongee nae awadhamini, msibaki mnalia tu