Wachezaji kurudi makwao mara kwa mara kwa sababu za kifamilia ni kutokuwa na professionalism, haifai

Wachezaji kurudi makwao mara kwa mara kwa sababu za kifamilia ni kutokuwa na professionalism, haifai

Kumekuwa na tabia inayokera sana ya wachezaji kuruhusiwa hovyo na viongozi wa timu kwenda makwao eti tu kwasababu za matatizo ya kifamilia na hili naliona sana katika klabu yangu pendwa ya Yanga sc.

Haingii akilini timu iko pre season kwa maandalizi kabambe then unasikia mara pacome karuhusiwa kusafiri kurudi kwao, msimu ulioisha ilikuwa ni kama wimbo wa taifa katika kila mechi kubwa na muhimu nilazima usikie kuna baadhi ya wachezaji muhimu wanamatatizo ya KIFAMILIA, Rubbish

Ndiyo maana wachezaji wanalipwa mamilioni mengi ,nahii ni kuwataka kuzitumikia timu zao hata katika nyakati mbaya za maisha yao binafsi.. jambo hili sio jema kwa muunganiko wa timu na linakera kweli kweli, ni upumbavu na kukosa uweledi
Wewe unaishi na familia ni rahisi mwenzako anaishi kambini. Panua wigo wa fikra.
 
Back
Top Bottom