Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nasikia Kelvin John anatakiwa na TP Mazembe?
Wameanza visingizio wakifungwa wadai hatukulipwa posho
Walipwe hela zao , hatutaki dhuluma .
Mungu awasaidieNi kweli na Jamaa ( TP Mazembe ) wako Jijini Dar es Salaam tokea jana Kuzungumza na Viongozi wa Vilabu na wanawataka Wachezaji Watatu Mohammed Hussein Tshabalala ( Zimbwe Jr ) wa Simba SC, Faisal Salum ( Fei Toto ) wa Yanga FC na huyo Dogo Kelvin John.
Wawalipe tu pesa zao wasitake kuwadhulumu.
Mimi naomba wasiwalipe kabisa ili Wachezaji wapandwe na Jazba kisha Wafungishe Makusudi ili tuondolewe mapema na wale tunaomchukia Kocha Amunike tujiandae Kumpopoa na Mawe pale JNIA kama akirudi na Timu.
Juzi mama samia kachangisha au kina karia wamepita nazo
Kazi ya ukocha ilitangazwa, uliomba? Isiwe ni mahaba niue kwa hao wachezaji!Hao Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars, Kocha wao Amunike ambaye namchukia mpaka basi kwakuwa hafai na hatufai pia pamoja na TFF hadi Wizara husika wasitake kutufanya Watanzania wote ni Majuha. Ukweli ni kwamba wameshajua kuwa Makapu ya Magoli tunaenda Kurudi nayo kutoka huko nchini Misri hivyo sasa wanatujenga Kisaikolojia ili hata wakifanya huko vibaya basi Kisingizio kikuwa kiwe Wachezaji waligoma, michango haikutosha na kwamba Serikali iliwatenga.
Ni Mwendawazimu tu pekee ndiyo atadhani kuwa Taifa Stars itazifungwa Timu za Senegal, Algeria na Kenya ambazo itakabiliana nazo. Kitu pekee ninachokijua na nina uhakika nacho kama Taifa Stars hii ya Kocha Mbovu na Mbinafsi itatoka huko na Alama ( Point ) basi ni 1 moja ila nina uhakika wa 100% kuwa Taifa Stars itamaliza huko ikiwa na Alama ( Point ) Sifuri ( Zero ) kabisa.
Kocha mwenye Akili na anayejua vyema Mpira kamwe hawezi Kuwaacha Wachezaji wazuri, tegemeo na muhimu kama akina Mkude, Ajib, Chilunda, Banda na Kichuya huku akifanya pia Kosa kubwa mno la Kumuacha ( Kumuondoa ) Kikosini Mchezaji Kinda kabisa Kelvin John ambaye nina uhakika angekuwepo tu huko hata kama asingempanga Kwake Yeye ( Kelvin John ) ingekuwa ni exposure ya Kutosha ambayo ingemjenga na kumsaidia pia hata Kisaikolojia na baadae ndiyo angekuja kuwa Mbadala mzuri mno wa Nahodha Mbwana Ally Samatta Kikosini.
Kama kuna Mtanzania ambaye anaiombea mabaya Taifa Stars ifungwe basi ni Mimi na mtanisamehe sana kwa hili.
Hakuna uzalendo kwenye kazi.Timu hii itanipa pesa sana ntaiua mechi zote vilaza kabisa inabidi watangulize uzaelendo kwanza kwasababu ni nchi sio club
Rais wa TFF Wallace Karia wakati anaomba Kura alikuwa na Kg 47 nina uhakika kwa jinsi alivyo sasa na kwa Pesa anazopiga na Maslahi anayoyapata hapo ukimpima atakuwa na Kg 175.
Kwani Makonda anasemaje?
Bado michango inakusanywa, Baba Mkuu kauchuna serikali ipo kimya, hadi wamalize kukusanya zile ahadi.