Wachezaji wa Red Sea Walioingia mitini kupata timu?

Wachezaji wa Red Sea Walioingia mitini kupata timu?

sir echa

Member
Joined
May 28, 2010
Posts
85
Reaction score
3
Siku chache zilizopita kuna taarifa tulipata kuhusu wachezaji wa Red Sea walioingia mitini badala ya kurudi kwao baada ya kuondolewa kwenye mashindano hatua ya robo fainali,ila mwisho wa siku ikabainika wamejisalimisha wizarani,naomba wadau mnisaidie mambo mawili..

i) Maombi yao ya ukimbizi yamefikia wapi??
yalikubaliwa au yalipigwa chini?

ii)Kwa sheria za CECAFA,FIFA e.t.c,hivi wakikubaliwa kuwa wakimbizi wanaruhusiwa kutafuta timu za kuchezea hapa bongo?

Naomba mwenye ufahamu wa masuala hayo mawili or any anisaidie.
 
Wananeda Simba, Rage anawahitaji kuimarisha timu ha ha ha
 
Nimesikia kadhaa wameshafika Zambia kuelekea Bondeni si mnafahamu Tanzania ni transit tu ya wakimbizi lengo ni kufika South baadae Ulaya/Marekani.
 
Mkuu status gani itawafanya waishi kama wakimbizi hapa Tanzania?
 
Mkuu status gani itawafanya waishi kama wakimbizi hapa Tanzania?

Status ya kuwafanya waishi kama wakimbizi hapa tz zipo nyingi,naweza kukutajia kadhaa..

i)Hali tete ya amani nchini mwao:ni haki ya mtu yeyote kuomba ukimbizi nchi nyingine endapo hali ya amani nchini mwake hairidhishi,mfn. vita au mapigano ya wenyewe(civil war);

ii)Njaa au ukame unaotishia uhai wa mwanachi;

Sio expert sana wa eneo hilo ila najua kuna aina nyingi za ukimbizi zinazotambuliwa kimataifa( according to U.N.H.C.R),na ndio maana msemaji wa wizara alisema wanachunguza sababu zao kama zina mashiko wafikiriwe kupewa ukimbizi..nadhani umenisoma mkuu!
 
Back
Top Bottom