Wachezaji wa Simba na familia zao kupatiwa Bima ya Afya

Wachezaji wa Simba na familia zao kupatiwa Bima ya Afya

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Klabu ya Simba leo Oktoba 28, 2022 imeingia mkataba wa miaka miwili wa Bima ya Afya na kampuni ya Mo Assurance ya Jijini Dar es Salaam. Mkataba huo uliosainiwa una thamani ya sh 250 milioni kwa mwaka na utahusika kwa timu zote tatu za Simba kwa maana ya timu kubwa, timu ya wanawake na ile ya vijana.

Bima hiyo pia itawafikia waajiriwa wote wa Simba na familia zao ambapo kila mmoja atakuwa na nafasi ya kuongeza watu wanne tegemezi kwenye bima hiyo ambao ni mke/mume na watoto.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo, Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameeleza namna timu hiyo itakavyonufaika na mkataba huo.

"Tumekuwa tukitumia gharama kubwa kwenye matibabu ya wachezaji na waajiriwa wengine wa Simba lakini ujio wa bima hii utatusaidia kwenye gharama hizo nakuongeza ufanisi kwa kila mtu kwenye eneo lake", amesema Barbara.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya Mo Assurance, Fatema Dewji amesema mkataba huo umesainiwa baada ya majadiliano ya muda mrefu huku akiamini utakuwa msaada kwa Simba na kampuni yake.

"Pande zote mbili tumejadili kwa muda mrefu kuhusu mkataba huu na Sasa tumesaini. Utasaidia katika matibabu na kuwafanya Wachezaji na waajiriwa wengine wa Simba kutowaza Tena suala la matibabu na kutimiza majukumu yao kwa kujiamini zaidi", amesema Fatema.

Huduma ya bima hiyo inapatikana kwenye hospitali zote kubwa nchini na itatumika kwa matibabu ya kawaida, kulazwa na majeraha yanayotokea mchezoni.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Ni aibu kwa club ya Simba eti wachezaji na staff hawana bima ya afya, narudia tena hii ni aibu na fedhea kubwa, bora wangefanya internal kimya kimya kuficha aibu hii.

Halafu hii familia ya Dewji muwe mayo makini maana yake familia itakuwa inalipwa kila mwezi na Simba kwa akili ya hizo bima.

Wasiokuwa na akili timamu hawawezi kuugunduwa huu Utapeli unaofanyika hapa kula pesa za Simba.

Wazoefu wote wa bima tunajuwa hakuna pesa ya burebkama pesa ya bima kwa mwaka hili kwa kampuni ya bima.

Kina GENTAMYCINE mnaibiwa huku na wahindi hawa familia ya Dewji mchana kweupe.
 
Pesa ina toka mfuko wa kushoto ina ingia wa kulia... safi sanaaaa...

Vijana fanyeni kazi muanzishe makampuni kama vunja bei...

Unganisheni nguvu, boss anuniwi, jifunze kutoka kwa walio fanikiwa sio kwa masikini wenzio wanao lalamika kila uchwao

Fatma boss simba
Fatma boss mo’s vikampuni

Hersi boss yanga
Hersi boss gsm

Azam ana baki na azam yake wala hatupiwi mawe... ni yakeee, hizi zingine ni za wote kila mtu ana kula kwa wakati wake

Vijana pigeni kazi hacheni lawama
 
Kuna klabu ina bima? Ata azam sizani kama wana bima na kama wanayo haina muda mrefu...

Utasikia uko jangwani kibuyu kimelia cha bima na chamanzi nao wana gawa bima
 
Kuna klabu ina bima? Ata azam sizani kama wana bima na kama wanayo haina muda mrefu...

Utasikia uko jangwani kibuyu kimelia cha bima na chamanzi nao wana gawa bima
Wewe kichwani siyo mzima, jifunze kwanza uelewe bima ni nini na mkataba ya wachezaji inaandikwaje.

Ni kichekesho mtu ni Mwalimu wa taasisi ya See Simba mpaka leo hana bima ya afya, achana na wachezaji mkataba yao in a include matibabu.

Labda hao matapeli wa kihindi ningeona wana jipya kama wangewakatia bima za maisha wachezaji na siyo huu Utapeli wa kupiga pesa za Simba kila mwezi kuilipa familia ya Mo Dewji.
 
Weka mikataba ya wachezaji tuone hiko kipengele wewe mwelevu

Nenda kaulize kama wachezaji hao wa timu za azam simba yanga kama wana bima

Achilia mbali wachezaji wa polisi au kmc au mtibwa sijui ihefu nao wana mikataba isiyo na bima za afya

Wanacho jali ktk mikataba ni nyumba, gari, pesa basi

Kama una mkataba weka

Alicho fanya mo ni kuangalia fursa ili pesa iweze kurudi mfukoni kwake...

Na kutangaza biashara...

Kama utaweza weka mkataba wa dilunga wenye bima ya afya... wana tibiwa kwa hisani na umuhimu wa mchezaji kwa wakati huo

Tofauti na hapo una temwa... shomari kapona kanisani na kuokoka juu... bima hawana ila wana bima za magari sio za afya
 
Mo assurance. Hivyo watakuwa wanakatwa mishahara au?Ila Mo Dewji bwana. Hivyo hawana ruhusa mfano ya kujikatia Jubelee n.k. Sawa Mo tumejua kuwa una Mo kampuni ya Bima.
 
Mo assurance. Hivyo watakuwa wanakatwa mishahara au?Ila Mo Dewji bwana. Hivyo hawana ruhusa mfano ya kujikatia Jubelee n.k. Sawa Mo tumejua kuwa una Mo kampuni ya Bima.
Yeah yeye ni mfanyabiashara tusisahau hilo...

Kama kuna kitu hakipo sawa basi wa kulaumiwa ni watu kama try again, magori, mwenyekiti na wajumbe wengine

Yeye ana 49% hana mamlaka hayo dhidi ya 51%

Ukiona limepita basi kuna jambo...

Timu ilikuwa ina toa pesa mfukoni kutibu wachezaji na sasa mchezaji ana jitibia chini ya utaratibu wa bima

Zipo kampuni na taasisi kibao hazina bima kwa wafanyakazi wake (zipo za kimataifa na za ndani) ata yanga hawana ila kila taasisi ina angalia uwekezaji utakao patikana

Una zani nhif watatoa mkataba wa 250 kwa ajili ya kutangaza na pia kuwapa bima wachezaji na wafanyakazi?
 
Pesa ina toka mfuko wa kushoto ina ingia wa kulia... safi sanaaaa...

Vijana fanyeni kazi muanzishe makampuni kama vunja bei...

Unganisheni nguvu, boss anuniwi, jifunze kutoka kwa walio fanikiwa sio kwa masikini wenzio wanao lalamika kila uchwao

Fatma boss simba
Fatma boss mo’s vikampuni

Hersi boss yanga
Hersi boss gsm

Azam ana baki na azam yake wala hatupiwi mawe... ni yakeee, hizi zingine ni za wote kila mtu ana kula kwa wakati wake

Vijana pigeni kazi hacheni lawama
Hersi boss GSM, Hersi boss Yanga, GSM ina sign mkataba na yanga na Hersi anaiwakilisha GSM na pia anaiwakilisha Yanga na kusaini mkataba wa hizo pande mbili...[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Club ya Simba SC leo kupitia CEO wao Barbara Gonzalez imetangaza kuingia mkataba wa udhamini wa miaka miwili na kampuni ya bima ya MO Assurance chini ya usimamizi wa @fatemagdewji ambapo itawezesha Simba SC kuanzia wafanyakazi wake na wachezaji wa timu zote za Simba kupata bima ya afya.

Mkataba wa huo una thamani ya Tsh milioni 250 kwa mwaka nje ya gharama za matibabu watakazokuwa wanalipa MO Assurance na bima hiyo ya afya itatolewa kwa mchezaji/mfanyakazi wa Simba SC na wategemezi wake wanne (mke/mume na watoto watatu).

Mwaka jana tu Simba SC imeingia gharama ya kutoa zaidi ya Tsh milioni 300 kwa ajili ya matibabu kwa wachezaji wake kitu ambacho baada ya mkataba huo sasa MO Assurance ndio watakuwa wanalipia kupitia bima yao. #MillardAyoSPORTS
 
Ni aibu kwa club ya Simba eti wachezaji na staff hawana bima ya afya, narudia tena hii ni aibu na fedhea kubwa, bora wangefanya internal kimya kimya kuficha aibu hii.

Halafu hii familia ya Dewji muwe mayo makini maana yake familia itakuwa inalipwa kila mwezi na Simba kwa akili ya hizo bima.

Wasiokuwa na akili timamu hawawezi kuugunduwa huu Utapeli unaofanyika hapa kula pesa za Simba.

Wazoefu wote wa bima tunajuwa hakuna pesa ya burebkama pesa ya bima kwa mwaka hili kwa kampuni ya bima.

Kina GENTAMYCINE mnaibiwa huku na wahindi hawa familia ya Dewji mchana kweupe.
Mo Dewji anapenda sana kutufanya wana Simba SC wote ni Mipan'gang'a ( Mipumbavu ) tupu tu na sijui ni kwanini.

Uwanja wa Mazoezi ni Mo Arena, Jezi za Simba SC zimejaa Chapa za Products zake na Leo tena kaja na Mo Insurance yake.

Halafu hata CEO Wetu nao huwa anawahi tu Kututangazia Masuala ila huwa hatudadavulii tujue ni kwa jinsi gani Klabu ya Simba inafaidika Financially and Economically pia.

Ninachokiona kwa sasa ni Mo Dewji Kujitajirisha zaidi Kimapato kupita Klabu ya Simba na kwa Upan'gang'a ( Upumbavu ) Wetu Mashabiki wala hatushtuki na tunaona ni sawa tu.

Namheshimu Mo Dewji ila simuelewi.
 
Hersi boss GSM, Hersi boss Yanga, GSM ina sign mkataba na yanga na Hersi anaiwakilisha GSM na pia anaiwakilisha Yanga na kusaini mkataba wa hizo pande mbili...[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Hatari ila swalamaa
 
Babra utakumbukwa daima umeitoa simba kwenye uswahili na kuipeleka duniani
 
Back
Top Bottom