Wachezaji wa Simba wapimwa corona huko Sudan na majibu yanaonyesha hawana

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825
Kwa nyakati tofauti katika mashindano ya Kimataifa kama Ligi ya mabingwa Afrika na mengineyo kunakuwa na madai ya figisu inapofika kwenye vipimo vya covid 19.

Kikosi cha Simba kilifanya vipimo hivyo jana Februari 4 asubuhi katika kambi yao hapa katika hoteli ya nyota tano ya Al Salam.

Majibu ya vipimo hayo yametoka na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wote waliokuwa katika msafara majibu yao yametoka safi na hakuna mwenye maambukizi.

Kuwa safi kwa majibu hayo kazi inabaki kwa kocha wa Simba, Didier Gomes kuchagua wachezaji ambao anawataka kuwatumia katika mechi hiyo.

Ikumbukwe Simba walivyoenda kucheza ugenini dhidi ya AS Vita kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Mwananchi
 
Kikosi cha Simba kilifanya vipimo hivyo jana Februari 4 asubuhi katika kambi yao hapa katika hoteli ya nyota tano ya Al Salam...

Kuna watu wanapata tabu sana. Hivi ni mchezaji gani ambae hapendi hizi raha
 
hili kundi limenifurahisha sana bado sijajua tukienda kucheza na Al ahly au sijui kwa kuwa mechi zinaanzia kwao hawana figisufigisu za kuwabambikia wachezaji tegemezi kuwa wana corona
 
Sudan ni rafiki mkubwa wa China katika nyanja mbalimbali ikiwemo utabibu. Kwa hakika kipimo kilichotumika kuwapima hawa wachezaji wa Simba ni kile kipimo kipya kutoka China.
 
Mbona majibu yametoka haraka sana au wametumia kile kipimo cha china
 
Kwa nyakati tofauti katika mashindano ya Kimataifa kama Ligi ya mabingwa Afrika na mengineyo kunakuwa na madai ya figisu inapofika kwenye vipimo vya covid 19.

Kikosi cha Simba kilifanya vipimo hivyo jana Februari 4 asubuhi katika kambi yao hapa katika hoteli ya nyota tano ya Al Salam.

Majibu ya vipimo hayo yametoka na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wote waliokuwa katika msafara majibu yao yametoka safi na hakuna mwenye maambukizi.

Kuwa safi kwa majibu hayo kazi inabaki kwa kocha wa Simba, Didier Gomes kuchagua wachezaji ambao anawataka kuwatumia katika mechi hiyo.

Ikumbukwe Simba walivyoenda kucheza ugenini dhidi ya AS Vita kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Mwananchi
Kwenye makalio
 
Back
Top Bottom