Wachezaji wa Taifa Stars kupewa Viwanja, Golikipa kuvuta Toyota Crown Asiporuhusu goli

Siasa, Siasa, Siasa

Ndio zitatutoa mchezoni siku ya leo. Ma ahadi mengi focus ya mchezo inaondoka kina Kagoma watataka nao wafunge magoli. Toa ahadi mkishinda mtapata kiasi fulani TOSHA, Sasa mambo ya ma assist sijui goli ndio italeta tafrani hapo.
Naomba yawe magoli 100
 
Kuelekea mchezo wa michuano ya CHAN kati ya Taifa Stars dhidi ya Morocco utakaochezwa leo Agosti 22, 2025 katillka dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila ametangaza zawadi na motisha zitakazotolewa na uongozi wa mkoa kwa kishirikiana na wadau mbalimbali ili kuchochea ushindi katika mchezo huo.

Zawadi hizo ni pamoja na kitita cha shilingi za kitanzania milioni ishirini zitakazotolewa kabla ya mchezo huo, zawadi ya shilingi milioni tano kwa kila goli, shilingi milioni moja kwa kila mfungaji wa goli huku atakayetoa pasi ya mwisho kuelekea goli (assist) atazawadiwa shilingi laki tano.

Kwa upande wa mlinda mlango (Goalkeeper) katika mchezo huo atazawadiwa gari aina ya toyota crown endapo mchezo huo utamalizika bila kufungwa goli lolote.

Mbele ya Morocco hata wangeahidiwa kupewa ikulu yote na kizimkazi watapigwa tu leo
 
Kuelekea mchezo wa michuano ya CHAN kati ya Taifa Stars dhidi ya Morocco utakaochezwa leo Agosti 22, 2025 katillka dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa huo Mhe. Albert Chalamila ametangaza zawadi na motisha zitakazotolewa na uongozi wa mkoa kwa kishirikiana na wadau mbalimbali ili kuchochea ushindi katika mchezo huo.

Zawadi hizo ni pamoja na kitita cha shilingi za kitanzania milioni ishirini zitakazotolewa kabla ya mchezo huo, zawadi ya shilingi milioni tano kwa kila goli, shilingi milioni moja kwa kila mfungaji wa goli huku atakayetoa pasi ya mwisho kuelekea goli (assist) atazawadiwa shilingi laki tano.

Kwa upande wa mlinda mlango (Goalkeeper) katika mchezo huo atazawadiwa gari aina ya toyota crown endapo mchezo huo utamalizika bila kufungwa goli lolote.

Moroco,tandika hao watu bila huruma.Hiyo sio timu ya Taifa tena ishapata nuksi kwa wanasiasa.
 
Back
Top Bottom