SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Kuna utamaduni wenzetu wanao, mchezaji akifikisha umri au stage fulani anatangaza mwenyewe kwamba mwaka huu ni mwaka wangu wa mwisho kutumikia timu ya taifa.
Hii ina faida kubwa sana kwa mchezaji. Kama umecheza kwa muda mrefu, watu watataka waweke kumbukumbu zako za mwisho ukichezea timu ya taifa. Waliokuwa wanakukubali watakuja viwanjani kukupongeza katika kila mechi zako za mwisho, watanunua jezi zako na kuomba uzisaini, watapiga picha na wewe, nk. Unaweza kuingia mkataba na kampuni fulani wakakutengenezea bidhaa kama t-shirts utakazozisaini na kuziuza. Ni kumbukumbu nzuri kwa mchezaji na wale waliokuwa wanakusapoti.
Ukiwasiliana na mamlaka za soka, wanaweza hata kukuandalia mechi rasmi ya kirafiki au kuchagua mechi iliyo katika ratiba ambayo inakuwa ndiyo ya mwisho kwako ya kukuaga rasmi. Mapato ya mechi hiyo kama ni ya kirafiki unaweza kupewa wewe kama zawadi na unaweza kutoa asilimia fulani kwa ajili ya jamii yenye uhitaji. Familia yako inaweza kuwepo pale, unaweza kucheza kwa dakika fulani tu na ukiingia au ukiwa unatoka watu wanasimama kukupigia makofi. Ni kumbukumbu unayoweza kuiweka kwa ajili ya familia yako kwa muda mrefu sana.
Sasa wachezaji wetu, sijui ni tamaa au labda kivuli cha kucheza timu ya taifa kinawabeba huko wanakocheza wanapata fursa au heshima fulani kwa hiyo wanaogopa kuipoteza. Wanang'ang'ana weee mwisho wa siku wanaachwa kiholela tu.