Wachezaji wa timu za wenzetu wanalia kwa kutoingia nusu fainali ila Taifa Star yetu ni full tabasamu ilipoishia

Wachezaji wa timu za wenzetu wanalia kwa kutoingia nusu fainali ila Taifa Star yetu ni full tabasamu ilipoishia

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Nimeona jinsi timu za Morocco, Egypt na leo Guinea walivyolia kwa kutoingia quarter final au semi final. Yaani wanaumia. Ila wachezaji wetu sikuwahi kuwaona wakisikitika kwa kutofanya vizuri
 
Ila Watanzania tuna maneno sana, yani unawalaumu wachezaji kwa kutokulia kweli?

Halafu kwa stage gani tuliyowahi kufika sasa? Zile point 2 tu yalikuwa mafanikio tosha!
 
Wachezji na mashabiki wa Tanzania wanatakiwa washangilie kwa matokeo ya point mbili, hatukua na wachezaji wengi wenye uzoefu na uwezo wa kutosha.

Kulalamika kiwango Cha timu ya Taifa ni kutotambua status ya soka letu kwa wenye ufahamu na soka letu ata point 2 ni za kushukuru.
 
mwijaku na baba levo ndio waongozaji wa taifa star unategemea nini hapo lazima wacheke mda wote wachezaji
 
Nimeona jinsi timu za Morocco, Egypt na leo Guinea walivyolia kwa kutoingia quarter final au semi final. Yaani wanaumia. Ila wachezaji wetu sikuwahi kuwaona wakisikitika kwa kutofanya vizuri
Ile ni kikundi cha maigizo ....kinaongozwa na Mwijaku
 
Wachezji na mashabiki wa Tanzania wanatakiwa washangilie kwa matokeo ya point mbili, hatukua na wachezaji wengi wenye uzoefu na uwezo wa kutosha.

Kulalamika kiwango Cha timu ya Taifa ni kutotambua status ya soka letu kwa wenye ufahamu na soka letu ata point 2 ni za kushukuru.
Maximo alishaitengeneza timu. Tulishavuka viwango vya kufurahia pointi 2.
 
Malengo yetu kwanza ilikuwa ni kushiriki halafu kupata angalau point moja
2025 ni kushiriki na kushinda angalau mechi moja
2027 sisi ndio wenyeji angalau tuishie 16
 
Hili hata mm nimekuwa nikilijadili sana Kijijini Kwetu kwann wenzetu wanalia sana?Na wakati Mwingine wachezaji hao wana Uraia pacha.
 
Nimeona jinsi timu za Morocco, Egypt na leo Guinea walivyolia kwa kutoingia quarter final au semi final. Yaani wanaumia. Ila wachezaji wetu sikuwahi kuwaona wakisikitika kwa kutofanya vizuri
Ndio maaana hata Viongozi wao Wakikosea wanajiuzulu. Hapa kwetu Viongozi wameshindwa kumudu majukumu lkn bado wamekalia Viti vyao.

Chukua hii:
Mara nyingi; Nchi zilizopata Uhuru kwa Demokrasia huwa Wananchi wake hawana Agressiveness kupambania Nchi zao ni waoga, hawana uchungu nk.
Lkn Nchi ambazo zimejipambania kwa Jasho na Damu toka kupata Uhuru zina Spirit na Morali spirit katika kupambania Mataifa yao daima! Hivyo yani
Mcongoman Mmoja aliwahi kusema. UKIONA TIMU IKO NYUMA GOLI 3 na HAKUNA MCHEZAJI WAKO ANAFURA kwa HASIRA za HISIA asipewe hata kadi ya Njano vunja hiyo timu!
 
Hahah unataka tulie kama Senegal walivyolia Hadi kushindwa kutembea.
 
Maximo alishaitengeneza timu. Tulishavuka viwango vya kufurahia pointi 2.
Maximo hajawahi kutengeneza timu ila alijitahidi kwenye hamasa na uzalendo Tena yeye mfungaji wake alikua ngasa wa Futi 5 pale mbele.
Maximo ni mtu wa saikolojia na hamasa.

Mfano wale watoto wa saint Francis Girls shule maalum kule mbeya, ushindanishe na shule zetu za kawaida za serikali na utegemee utapata ushindani.

Ndivyo ilivyo kwa timu yetu ya Taifa kule AFCON.
Kuna timu zimepata wastani wa Alama C kwenye mashindano zimelia kwa huzuni na sisi timu yetu imepata alama D Tena 2 mnataka tulie wakati mara ya mwisho tulipata D Moja.
Hatuwezi kuvuna tusipo panda.
 
Ila Watanzania tuna maneno sana, yani unawalaumu wachezaji kwa kutokulia kweli?

Halafu kwa stage gani tuliyowahi kufika sasa? Zile point 2 tu yalikuwa mafanikio tosha!
Walie tu [emoji3][emoji3]
 
Maximo hajawahi kutengeneza timu ila alijitahidi kwenye hamasa na uzalendo Tena yeye mfungaji wake alikua ngasa wa Futi 5 pale mbele.
Maximo ni mtu wa saikolojia na hamasa.

Mfano wale watoto wa saint Francis Girls shule maalum kule mbeya, ushindanishe na shule zetu za kawaida za serikali na utegemee utapata ushindani.

Ndivyo ilivyo kwa timu yetu ya Taifa kule AFCON.
Kuna timu zimepata wastani wa Alama C kwenye mashindano zimelia kwa huzuni na sisi timu yetu imepata alama D Tena 2 mnataka tulie wakati mara ya mwisho tulipata D Moja.
Hatuwezi kuvuna tusipo panda.
Ila mkuu, kimahesabu kushinda mashindano haya ni jambo rahisi, maana timu inacheza mechi chache na kila siku inakua na muda wa kujisahihisha.

Mfano Congo walivyoanza walikua wanasua sua lakini sasa hivi haoo wanakwenda.. yaani ugumu ni kwenye makundi tu, sasa pale ndio unakuta timu kama inaleta mzaha hivi.

Kuhusu wachezaji, tunasema kila siku hapa, TFF ipeleke wachezaji watoto wa miaka 10 na kuendelea academy za timu kubwa za Brazil huko, za Spain, Uingereza nk, baada ya miaka 5 tutakuwa na timu ya maana sana.. au TFF hawapendi Taifa kupata sifa??

Kama serikali inatoa scholarship watu wakasome vyuo vikuu nje ya nchi, TFF na wizara ya michezo wanashindwa au hawataki tu kupeleka watoto academy za nje ya nchi??
 
Kwanza Afcon tuliyofaulu kuingia kihalali ilikuwa ni ile ya mwaka 1980 kule Nigeria tu, ile ya 2019 na ya safari hii ni za figisu tupu.

Mpira wetu ni mdogo sana ila kelele ndio nyingi. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom