Yaah rajab rashidi anajichanganya kwa kusikia filimbi ya mashabiki na kudhani ni ya muamuzi anaukamata mpira ndani ya kumi na nane mwamuzi anaweka tuta almarhumu gaga anapiga mpira unagonga mtambaa panya kisha yanga wanaenda kupata bao. Wale ambao walikuwa wakifuatilia mpira kupitia RTD khasa mashabiki wa simba wanashangilia bao wakidhani gaga kaukwamisha mpira kumbe sivyo. Simba alikula tatu kwa moja mabao ya yanga yakifungwa na makumbi juma (homa ya jiji )Thomas kipese na sanifu razaro (tingisha ).