Wachezaji waliochezea vilabu vyote vya Simba na Yanga kwa mafanikio

Wote Simba na Yanga hawajawahi kuwa na wachezaji wazuri ila majina tu na mpira si jina bali kipaji na akili. Binafsi sijawahi ona mchezaji yeyote mzuri toka hizi club tajwa na ndiyo maana hatujawahi kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Ni mtazamo wako hatuna budi kuheshimu mtazamo wako
 
Wote Simba na Yanga hawajawahi kuwa na wachezaji wazuri ila majina tu na mpira si jina bali kipaji na akili. Binafsi sijawahi ona mchezaji yeyote mzuri toka hizi club tajwa na ndiyo maana hatujawahi kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Msuva siyo mchezaji mzuri? Samatta je? Ajibu ,Mrisho Ngassa etc.Acha dharau mkuu.
 
Wote Simba na Yanga hawajawahi kuwa na wachezaji wazuri ila majina tu na mpira si jina bali kipaji na akili. Binafsi sijawahi ona mchezaji yeyote mzuri toka hizi club tajwa na ndiyo maana hatujawahi kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Naona umeamua kuja kivingine
 

ulinzi wa Simba chini ya beki mbovu kabisa kuwahi kutokea ADOLPH KONDO
 
Tuko naye jamaa huku mbez pamoja na Aboubakary salum

Bado.anapiga kinywaji baa ile ile pale mbezi??.. kina gulamali mungu anawaona!!..walimfanya asiendelee na masomo yake na kumsajili...baadae akaenda ujerumani walimrudisha Tz then wakamtosa na umasikini wake..lkn wahindi wa yanga wana tatizo hilo historically bora simba kina dewji waliwatoa kina mogela mwameja dua said masatu kaseja nk..lkn yanga mtu kama lunyamila anakuja kusaidiwa na harambee za kina shiffih dauda kutibiwa malaria? Kizota?? Mwanamtwa?? Dah Sad!
 
Rambirambi ya Mafisango nayo ililiwa na wahindi wa Yanga.
 
method mogella aka fundi, dally kimoko fundi mwingine huyu kutoka ukoo wa kihwelo, steven nemes,
Mwanamtwa Kihwelu
Muhesa Kihwelu
Jamhuri Kihwelu

Maanamtwa alicheza Yanga sikumbuki kama alicheza Simba...

Jamhuri ni Simba wa kufa mtu..

Muhesa nadhani ni neutral...
 
Ezekiel Greyson kutoka Yanga kwenda Simba. Ilikuwa vurumai kweli . Miaka ya 70 hiyo wengi wenu hamukuwa mumezaliwa.
 
Siku Thomas Kipese "uncle Thom" anasajiliwa Simba niliumia sana....

Hata Saidi Mwamba "Kizota"...

Athuman Abdalah "China" alisajiliwa Simba baada ya kutoka Uarabuni...
Yaah wote hao walikuwa na uwezo wa kucheza soka nje ila tuseme sijui kutotambulika kimataifa maana mtu kama selif keita mjomba wake na seydou keita aliekuwa barca kenda kucheza nantes miaka ya sitini alipo staafu akaja fungua academy ambayo huyo seydou keita aliendelezwa kisoka hapo. Sasa sisi wengi wa wachezaji wetu ilikuwa wanaishia fanja ya oman basi.
 
Hivi hii Fanja ipo kweli?

Niliisikia kitambo sana...

Watanzania tuna matatizo ya peke yetu mkuu na nadhani hili tuliache maana litaharibu siku bure...

Kuna mtaalam mmoja wa soka alisema Afrika kuna ncho mbili tu zinazotoa vipaji vya kipekee kabisa huku duniani zikiungana na Brazil...

Nchi hizo ni Nigeria na Tanzania...

Wabongo sijuwi tuna nini tu. Mtu kama Chambua,Husein Masha,Edward Chumila,Ramadhan Lenny kwa kuwataja wachache qa nafasi ya kiungo wangekuwa gumzo duniani kama wangepata nafasi lakini wakaiashia hapa hapa......
 
kuna fundi mwingine alitoka sigara kwenda yanga then akaenda simba shaban ramadhan nae alikua anaujua sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…