Wachezaji wanaosajiliwa Simba na Yanga sio wale wanaotafutwa Ulaya

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Tusidanganyane, Hakuna mchezaji mzuri sana ambae hakuonwa na timu kubwa za Ulaya, Afrika Kaskazini au Afrika Kusini. Ukiona mchezaji anakubali kuja kucheza kwenye ligi yenye viwanja vibovu kama Mkwakwani, Mabatini, Manungu, Kambarage au Lake Tanganyika ujue kuwa huyo ni mchezaji wa kawaida sana anaehitaji kukua ili aonekane na timu za Ulaya na Afrika Kaskazini.

Uwezo wa wachezaji wa ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na Kati hautofautiani sana, vipaji vipo lakini kinachowatofautisha ni bidii binafsi ya mazoezi na nidhamu ya mchezaji ndani na nje ya uwanja. Matunzo ya mchezaji kunachangia pia. Ukanda hauna wachezaji wazuri ndiyo maana hata timu na nchi wanakotoka hazina mafanikio kwenye soka la Afrika, kama wangekuwa wazuri hivyo kiasi cha kugombaniwa hivi na simba na Yanga basi mchango wao ungeonekana kwenye club na mataifa yao katika kuchukua makombe ya CAF na FIFA ranking.

Nazionya timu zetu tusije kufanya kosa la kuchezesha wageni 8 kwenye mechi moja na kuwaweka benchi wazawa kwakisingizio kuwa wamenunuliwa kwa pesa nyingi, tutaua soka letu, TFF, BMT na Wazari wa michezo tungeni kanuni ya idadi ya wageni kwenye mechi moja, vinginevyo tutalea vipaji vya nchi jirani na kudidimiza vya kwetu na timu ya taifa. Tusidanganyane "practice makes perfect", mtu yeyote akipewa fursa nyingi za kulitenda jambo hilohilo kwa muda mrefu anakuwa bora na mahiri kwenye jambo hilo. Mfano, hata maprofesa wetu wa leo wako wengi ambao walitahiriwa vizuri sana na mangaliba ambao hawana elimu ya chuo, ila uzoefu wao tu katika kuifyeka mikono ya sweta.

Tuepuke vita na uhasama wa kugombania wachezaji ambao hawajaonekana na timu za ulaya na timu kubwa za Afrika. Maana kama mchezaji angekuwa mzuri sana bila shaka tusingeweza kushindana na Aesernal na Al-Ahly kumsajili, ni wachezaji wa kawaida tu hawa lazima wasaidiwe kwa kununua marefa, wapewe ratina laini, nk. ili kushinda mechi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…