Wachezaji watatu bora kuwahi kucheza Yanga SC

1. Said Maulid SMG, huyu ndio alinifanya nikaipenda Yanga…
2. Nadir Haroub Ally (Cannavaro) huyu ndiye bora muda wote.
3. Shadrack Nsajigwa; Hatokaa atokee mchezaji aliyeipenda Yanga kama huyu, daima ana heshima yangu.
Mbona hamumtaji Mohammed Hussein 'Mmachinga' au Fred Felix 'Minziro'? Ama Athuman Abdallah 'China' na Said Mwamba 'Kizota' ambao baadaye waliangukia kwa Mnyama. Walikuwa watu sana hawa.

Ova
 
Hujagundua kitu ktk hao niliowataja? Ni pekee nilioweza kuwashuhudia.

Huyo SMG mwenyewe nilikuwa katoto sana, Nadir na Shadrack ndio haswa nimewaona ktk utimamu wa akili.

Ila ktk list yako nitamchagua Minziro ‘Baba Isaya’ mpaka sasa namshabikia kwenye timu anazocoach…

Lakini, wewe ulipata kuwashuhudia hao? Au ulitaka tu kuchombeza walivyoangukia huko ujingani kwenu?
 
Huo mstari uliomaliza nao umenibadilisha kabisa cha kuandika. Shida yenu watu wa Utopolo ni kuamini kuwa hiyo simu yenu ni bora sana, wakati yenyewe ni hadhi ya Shirikisho.

Ova
 
Ukiwaongelea finalist wa CCC last season weka heshima ktk jina lao tafadhali!
Kuna kitu mnasahau sana, kwamba semi final mlicheza na timu iliyoshuka daraja, na fainali mkacheza na timu iliyokuwa chini ya nafasi ya tano kwenye ligi yake ya ndani.

Kwanini nasema hivyo? Ni kwamba shirikisho ni michuano ya timu rahisi zaidi, kwa kuwa hukutana timu rahisi zaidi huko, tofauti na Ligi ya Mabingwa.

Ati wasema nini? Umesahau bingwa wa shirikisho kamfunga bingwa wa huko mnapopaabudu sana? Yani Makolo huko CCL mnapaona kama wapi sijui!

Acha tu niendelee kuwashukuru Raja maana mngevuka ile siku kwenda nusu fainali tusingekaa tupewe nafasi ktk mijadala ya soka!
 
Huna haja ya kubishana nao. Tatizo lao ni kwmb, kila timu inayocheza na Yanga, basi ni TIMU MBOVU….!!! Na wanakuja na evidence za kipuuzi…!!!
 
Uzi ulianzishwa kipindi hawajui kwamba kuna mwamba anakuja na fimbo ya chuma, Aliyetabiriwa na manabii wa soka, Kwamba atatuta jangwani atatenda makuu naye kisha kukaa miaka miwili Tanzania ataenda Misri Naye atazihukumu timu pinzani kwa mikwaju mithili ya farasi wa vita

"Nami nikaona watu maelfu kwa maelfu wakiwa wamevaa jezi za kijani nyeusi na njano wakinyoosha mikono mbele huku wakipiga piga mkono wa kushoto na kuume
Mithili ya bata akitetema mkia huku sauti zikisikika pa pa paa! Wengine wakisema FISTON KALALA MAYELE ni mmoja, The King"
 
Timu yoyote inayoshuka daraja huwa ni mbovu tu, hakuna namna ya kueleza timu iliyoshuka daraja kuwa ni kali kwa vile imecheza semi final ya kombe la Shirikisho.

Ova
 
Hapo ametamani kusema Ahly wabovu ila akikumbuka tarehe 20 sio mbali kakaa kimya, namjua.
Mnachanganya msimu huu na uliopita, hao wamempasua Ahly msimu huu baada ya kuimarisha timu. Walikuwa wabovu tu mlipocheza nao.

Kwahiyo Ahly hawajaimarisha timu? Ni wabovu?
Hapa tunaongea imebaki siku 1 ujue?
 
Hatujawahi kushindwa kumfunga Ahly pale kwa Mkapa. Atakufa tu. Ng'ombe atachinjwa kwa namna atakavyolala.

Hakuna mechi tutafungwa pale kwa Mkapa hata awe nani.

Ova
 
Uzi ulianzishwa kipindi hawajui kwamba kuna mwamba anakuja na fimbo ya chuma, Aliyetabiriwa na manabii wa soka, Kwamba atatuta jangwani atatenda makuu naye kisha kukaa miaka miwili Tanzania ataenda Misri Naye atazihukumu timu pinzani kwa mikwaju mithili ya farasi wa vita

"Nami nikaona watu maelfu kwa maelfu wakiwa wamevaa jezi za kijani nyeusi na njano wakinyoosha mikono mbele huku wakipiga piga mkono wa kushoto na kuume
Mithili ya bata akitetema mkia huku sauti zikisikika pa pa paa! Wengine wakisema FISTON KALALA MAYELE ni mmoja, The King"
Huyu mwamba sio kufunga tu anajua, ni fundi hadi wa kushangilia.
 
Back
Top Bottom