Wachimbaji madini nchini wamenunua picha moja kwa Tsh Bilioni 1.8 kwa ajili ya kumpa zawadi, Rais Samia Suluhu Hassan

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Wachimbaji madini nchini wamenunua picha moja kwa ajili ya kumpa zawadi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Samia Suluhu Hassan kwa thamani ya Shilingi Bilioni 1.8.

Wachimbaji hao wamenunua picha inayowaonesha Pomboo (Dolphin) wakiwa ndani ya maji Kizimkazi.
Katika hafla ya usiku wa sanaa za picha uliofanyika Kizimkazi Zanzibar, Rais Samia ameeleza kuwa picha hiyo ina historia kubwa katika maisha yake jambo ambalo limewavutia zaidi Wachimba madini nchini Tanzania kwa umoja wao na kuamua kununua picha hiyo kwa kiasi hicho.

Pia Soma
​
Source TBC Digital
 
Anayeweza kueleza faida ya hii picha yenye thamani kubwa namna hii aje hapa
Sababu ishaelezwa mkuu soma vizuri 😂

"Rais Samia ameeleza kuwa picha hiyo ina historia kubwa katika maisha yake jambo ambalo limewavutia zaidi Wachimba madini nchini Tanzania kwa umoja wao na kuamua kununua picha hiyo kwa kiasi hicho."
 
Mkuu historia ya nini na itasaidia nini baada ya miaka mitatu mbele
 
Madini ya Tope ...Labda..
Hakuna Miner anayeipenda CCM na Viongozi wake na haijawahi kushinda uchaguzi wowote kihalali palipo na Shughuli za Uchimbaji Madini yoyote yenye thamani,hata kama ni wa mpuliza Filimbi ya Taarifa za Mtaa..
Ni Marehemu Lowassa tu..tena baada ya kuhamia CHADEMA.
 
Wachimbaji madini nchini wamenunua picha moja kwa ajili ya kumpa zawadi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Samia Suluhu Hassan kwa thamani ya Shilingi Bilioni 1.8.

Wachimbaji hao wamenunua picha inayowaonesha Pomboo (Dolphin) wakiwa ndani ya maji Kizimkazi.
Katika hafla ya usiku wa sanaa za picha uliofanyika Kizimkazi Zanzibar, Rais Samia ameeleza kuwa picha hiyo ina historia kubwa katika maisha yake jambo ambalo limewavutia zaidi Wachimba madini nchini Tanzania kwa umoja wao na kuamua kununua picha hiyo kwa kiasi hicho.

Pia Soma
​
Source TBC Digital
Money launders katika ubora wao, nchi hij safari ni ndefu
 
Back
Top Bottom