Wachimbaji madini wawili wafariki kwa kuangukiwa na kifusi Geita

Wachimbaji madini wawili wafariki kwa kuangukiwa na kifusi Geita

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Wachimbaji wadogo wawili wa familia moja katika Kijiji cha Sabora wilayani Geita wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba madini ya dhahabu.

Wachimbaji hao Charles Nyamandodi na Benjamin Nyamandodi wanadaiwa kuingia kwenye shimo la uchimbaji lililoko kwenye leseni inayomilikiwa na Hussein Nyamacha kinyemela usiku na kufukiwa na udongo kisha kupoteza maisha.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Geita, Willson Shimo ameagiza mmiliki wa leseni hiyo kuripoti kituo cha polisi kesho Jumatatu Septemba 26, 2022 kueleza kwa nini aliacha mashimo bila kuweka alama ya tahadhari.

Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wachimbaji wadogo kufuata sheria za uchimbaji ikiwa ni pamoja na kuchimba kwenye mashimo rasmi yaliyoruhusiwa.

“Maduara haya yalikuwa yamefungwa hawa waliingia usiku na kuchimba ndipo walipopatwa na maafa nimeagiza mwenye leseni aje kesho polisi aeleze kwanini hakuchukua hatua za tahadhari baada ya kufungiwa mashimo yote aliyaacha wazi hii ni hatari kwa watu na hata wanyama”amesema Shimo.

Diwani wa kata ya Magenge, Edward Misungwi amesema changamoto wanayokutana nayo kwenye eneo hilo ni wachimbaji kutozingatia sheria na kanuni zinazotolewa na wasimamizi wa migodi.

“Vijana tuwe makini wananchi wa magenge wanakutwa na matukio ya watu kupondwa na maduara na watu wanakufa lakini hawabadiliki kila wakizuiwa kuingia wanaingia kinyemela na madhara yake ndio kama haya”amesema Misungwi

Ofisa kutoka Tume ya Madini, Dotto Ernest amewataka wachimbaji kufanya kazi kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na tume na kusema shimo walilofukiwa wachimbaji hao lilifungwa baada ya kujaa maji.

“Kesho hatua za kiuchunguzi na ukaguzi zitafanyika ili kuhakikisha usalama kwenye eneo la migodi kunakuwa salama hasa kipindi hiki cha mvua ambacho kinaathiri maeneo ya mgodi ambayo udongo unakuwa mlaini maeneo yote yatachunguzwa ili isijitokeze tena”amesema Ernest

Chanzo: MWANANCHI
 
Hapo kafara imeshatolewa. Lazima shimo litema madini ya kutosha
 
Back
Top Bottom