Wachina waja na maji haya, wanaliteka soko mdogo mdogo

So mbona waafrica wanafanya yote hayo hayo ,!!! Kwani serikali ya ccm Ina tofauti Gani na hizo sifa ulizozitaja za wachina!?
 
So mbona waafrica wanafanya yote hayo hayo ,!!! Kwani serikali ya ccm Ina tofauti Gani na hizo sifa ulizozitaja za wachina!?
Utofauti uliopo ni kuwa hawa ni wabongo, hawa ni Wachina. Hivi hata ukisema Lake Oil ni mafisadi hela ziliibiwa kwa wananchi ila hata kama ni kweli, bora wamewekeza nchini wanaajiri hapa hapa na wanazungusha faida nchini. Hao Wachina wanakomba kila faida wanarudisha kwao, wanaacha operating capital tu.

China ndio nchi inayoongoza kutupatia trade deficit kubwa kuliko nchi zote tunazofanya nazo biashara. China ni nafasi ya #5 kwa kununua bidhaa kutoka Tanzania, inazidiwa hata na South Africa na UAE, ila wakati huo ni ya kwanza kwa kutuuzia vitu na inayoifuata kwa kutuuzia inazidiwa almost mara nne na China kwa thamani ya bidhaa inazoleta Tanzania.
 
Kumbe hayo yane ni yao, aisee ni mabaya machungu yanakoroga tumbo kabisa. Nikiaagiza mtu akaja nayo huwa namuachia nabakia na kiu yangu
 
Ukiwasoma kwa makini wanaosifia utaona furaha yao ni wabongo kukosa soko hakuna kingine. Mtu hajawahi hata kufanya biashara ya karanga ila anakwmbia bei fulani tunapigwa. Hajui gharama zozote za hio product ila anakwambia anapigwa.
 
Hiyo itakuwa Tanzachia sio Tanzania tena.
 
TBS wanasemaje kuhusu usalama wa bidhaa za mchina?
 
TBS wanasemaje kuhusu usalama wa bidhaa za mchina?
Hawa Wachina wanaokamatwa na mabilioni kwenye viroba hawana la kuambiwa na TBS.

Na tatizo sio kwa TBS pekee, machimbo ya madini kule kanda ya ziwa (ambayo nayo siku hizi yamevamiwa na Wachina) yanamwaga mercury kwenye vyanzo vya maji, unakutana na kesi nyingi za kansa uko Shinyanga na Simiyu. Tatizo ni serikali nzima kuanzia wanaosimamia uwekezaji, manufacturing, biashara, exports na imports, sera za uchumi, mikopo na kila kitu.
 
Kwa nini Wachina ni wawekezaji kutoka nje ila wanauza vitu bei rahisi kuliko wazawa??
Hawana tamaa kama wazawa. Halafu kingine wanatumia technolojia yenye high productivity. Kwahiyo unakuta average cost yao ni ndogo kuliko makampuni ya wazawa.

Halafu kwenye biashar kuna kitu tunakiita predatory pricing--unauza bidhaa kwa bei ya chini ili uuwe ushindani na baadae uweze kuliteka soko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…