Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
www.jamiiforums.com
Yangezuka maandamano na hashtag za kutosha.
Miaka mingi sana mtu mweusi anawaita Waarabu sio Mwafrika. Hatujawahi kuwasapoti hata kuanzia Afcon hadi michuano ya mabara. Hata ikitokea Senegal anacheza na Egypt huwa wanashangilia Senegal ukiwauliza sababu watakwambia hao ni weusi wenzetu.
Mungu alivyo wa ajabu 2022 kule Qatar, Morocco alipambana akatinga nusu fainali na kuna mchezaji wao mmoja Boufal kama sikosei kwenye salamu za shukrani akazipeleka kwa watu wa Morocco na Waarabu wote dunia nzima.
Kwa mara ya kwanza mtu mweusi akaonjeshwa ladha ya dawa waliyokuwa wanawapatia Waarabu. Lilitoka povu hadi sio poa.