Wachina waliokamatwa na 'Mabilioni' wasomewa kesi ya uhujumu uchumi. wapelekwa Gerezani, kesi yao haina dhamana

Wachina waliokamatwa na 'Mabilioni' wasomewa kesi ya uhujumu uchumi. wapelekwa Gerezani, kesi yao haina dhamana

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam muda mfupi uliopita (leo, Jumatano Januari 07.2026) raia wa China waliokamatwa Oysterbay jana (Jumanne) wakiwa na 'mabilioni' ya fedha wamefikishwa Mahakamani hapo kusomewa mashtaka ya uhujumu uchumi.


Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyosomwa Mahakamani hapo leo, Jumatano Januari 07.2026 washtakiwa wote wawili (2) wanakabiliwa na kosa la kwanza la kuongoza genge la uhalifu, ikielezwa kwamba walitenda kosa hilo tarehe tofauti kati ya Desemba 01.2024 na Desemba 30.2025, katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Unguja -Zanzibar, pamoja na maeneo mengine ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Aidha imeelezwa Mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao kwa makusudi waliandaa genge la uhalifu lililojihusisha na kughushi nyaraka, kunakili kadi za ATM, kukwepa kodi na kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu

Katika kosa la pili, washtakiwa wote wanatuhumiwa kutenda utakatishaji fedha, ambapo imeelezwa Mahakamani hapo kwamba katika tarehe hizo hizo za kati ya Desemba 01.2024 hadi Desemba 30.2025, wakiwa Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washtakiwa walijipatia mali ambazo ni Dola za Kimarekani 707,075 pamoja na Shilingi za Kitanzania 281,710,000, huku wakijua wazi kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu wa kuongoza genge la uhalifu

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki alisema kuwa washtakiwa hao hawatakiwa kujibu chochote kwa sasa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo

Pia kwa mujibu wa sheria, mashtaka yanayowakabili washtakiwa hao hayana dhamana hivyo hawawezi kupata dhamana katika ngazi ya Mahakama hiyo

Upande wa Jamhuri uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa, ambapo kesi imeahirishwa hadi Januari 21.2026.

Pia Soma: Wachina wakamatwa maeneo ya Oysterbay wakiwa na takriban Tsh. Bilioni 6 taslim zikiwa zimefichwa ndani ya nyumba
 
Dola 710,000 ni sawa na 1.8 bilioni. Ukijumlisha 2 bilioni hazifiki hata bilioni 4. Hizo 2 nyingine zimeenda wapi? Au walikimbilia kutangaza kabla hawajazihesabu vizuri?

Amandla...
Bilioni 2 yeye kazitoa wapi? Hizo ni 200mil
 
Dola 710,000 ni sawa na 1.8 bilioni. Ukijumlisha 2 bilioni hazifiki hata bilioni 4. Hizo 2 nyingine zimeenda wapi? Au walikimbilia kutangaza kabla hawajazihesabu vizuri?

Amandla...
Lazima kuna mabunda wame kwapua hapo lazima unawajua polisi?
 
Safi kabisa.
Wachina ni kunyooshwa tu hakuna namna, maisha yao ya ujanja ujanja tu.
We nae unaongea na kupaparika kama kuku aliekatwa kichwa...
Hao hao China ndio mnawalilia na kudai ndo marafiki na wawekezaji wenu wa kweli tofauti na Mabeberu Marekani, so usiropoke hovyo tuache mahakama ifanye kazi yake.
 
Back
Top Bottom