Wachina waonja shubiri ya ubaguzi wao dhidi ya watu weusi

Wapi nimekwambia kua nakubali mchina kumbagua black? mimi nalaani ubaguzi wa aina yeyote ile,soma tena nilichokiandika,

Halafu kwa akili yako ilivyo ndogo umeamua kunihukumu kama akili yako ilivyokutuma kwenye huo mstari wa mwisho.

Basi tulia kwenye mada inayohusu ubaguzi wa wachina dhidi ya mtu mweusi, kama unataka kuzungumzia ubaguzi mwingine anzisha mada, la sivyo tulia usituchanganyie madawa.
Wewe unadhani wanaochangia hii mada hawajui kuwa kuna ubaguzi wa aina nyingi?. Usitutoe kwenue reli wakati mada inalenga kuwaamsha watu juu ya ubaguzi wa hawa watu ili wawe makini nao, wasitiwe na upofu na propaganda za win-win
 
Wewe ni nani mpaka unipangie cha kuchangia? hii ni mada ya ubaguzi na sijatoka nje ya mada, Safari moja huanzisha nyingine,

Hii mada yenyewe kwa jinsi ulivyoiwasilisha pamoja na hii comment yako,hasa huo mstari wa mwisho unaonyesha uhalisia wako kua hata wewe ni mbaguzi tu.
 

Basi tulia acha kurukaruka
Changia mada au anzisha ya kwako
Hii mada nimeianzisha mimi, sasa usilete shobo
Nyie self hating blacks ndo kikwazo cha kutokomeza ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wetu, hujitambui wewe!
 
Basi tulia acha kurukaruka
Changia mada au anzisha ya kwako
Hii mada nimeianzisha mimi, sasa usilete shobo
JF is an open forums,ukisha weka mada hapa inakua sio yako tena na member yeyote anakua na haki ya kuchangia,jifikirishe kwanza kabla hujaendelea kujiaibisha hapa kwa kuandika vitu vya hovyo zaidi.
 
Tasfsiri kwa kiswahili:-

Na: Clare C

Najua kwa kuandika nakala hii jinsi unavyoweza kuchukulia hili na jinsi ninavyoweza kutazamwa na umma kwa jumla.Lakini mtu fulani alilazimika kusema jambo na nimngojea kwa muda mrefu kutosha mtu kusema kitu bado hakuna mtu aliyekuja mbele.Sasa niko hapa, akisema amani yangu.

Raia wa China kote ulimwenguni wanalia kwa uchungu juu ya jinsi wanachukuliwa tangu virusi vya ugonjwa huu, jinsi wanaingia kwenye usafiri wa umma na watu wanaogopa kukaa nao, ni vipi wanapokuwa wakitembea barabarani watu huwatazama kwa sura mbaya.

Jinsi migahawa mingine ilivyoenda hadi kufikia hatua ya kuwapiga marufuku. Wanafunzi wa Kichina wanateseka mikononi mwa wenzao wa darasa na waalimu. Kwa kifupi, kila mtu hataki chochote cha kufanya nao, kwa sababu "wanaonekana kuwa na virusi na wenye kupenda kula kila kitu."

Kwa maoni yangu, hatimaye wanapata ladha ya dawa yao wenyewe.

Mimi ni Mwafrika, Mwafrika mweusi.Ninatembea katika mitaa ya Uchina kila siku na huwa wananikwepa, hutoka kwenye njia yangu nitakapita kana kwamba nitawauma.

Ninakaa kwenye usafiri wa umma hufunika vinywa vyao kana kwamba ninanuka, hubadilisha viti vyao, hunichukua video, na ninapotoa sauti kulalamika jinsi inanifanya nihisi(kushtaki), HAKUNA LOLOTE AMBALO SERIKALI YAO HUFANYA.

Badala yake, wanasema, watu wa China wanavutiwa na wewe tu, au, iko kichwani mwako, au bora bado: "wapuuzi tu."

Darasa langu sote ni kwa Wachina.Nimekuwa nikifanya maonyesho yangu kwa zaidi ya miaka 5 na kwa miaka hiyo 5, nimekaa peke yangu.Nimewekwa pekee na wanafunzi wenzangu wa darasa na waalimu wamejumuishwa.Nikiwauliza raia wa China kwanini wanatutenga?...

Wananiambia, vema, ni kwa sababu Waafrika ni masikini na wana Ukimwi.China ina idadi kubwa ya watu walio na VVU lakini watu wangu wanapata lawama .Je hiyo imewahi kuwa na vichwa vya habari huko kwenye media?

Tunapolalamika, jambo la kwanza ambalo Wachina wanasema ni, "Nenda NCHINI KWAKO! HUKU NI CHINA!" Sasa, ninajiuliza, je! Ninapaswa kusema hivyo kwao kwa hali hii?

Labda watu wa China wanahitaji kutazama kwenye kioo kabla ya kulia kuwa mchafu, labda watahitaji kuchukua dawa zao, ushauri wao wenyewe, acheni kufanya vitu vile vile ambavyo umekuwa ukifanya kwa waafrika wenzangu.

Hivi majuzi, kampuni ya simu nchini China ilifanya tangazo la Wachina walivaa kinyago usoni cheusi na hakuna mtu aliyepiga jicho.

Kwenye runinga ya kitaifa (sikukuu ya masika) kulikuwa na mwanamke wa China aliyevaa mavazi nyeusi na aliyevaa vitu vya mwili bandia kuiga mtu mweusi.

Tangazo lingine juu ya sabuni ya kufulia lilionyesha mtu mweusi kwenye washer aliyetengenezwa ili kuonekana kuwa havutii na kutupwa na mwanamke wa China kwenye mashine ya kuosha "kuosha," ambaye alitoka mweupe na ya kumvutia huyo mwanamke.Hayo yote yalikuwa kwenye television(netari) ya Kitaifa!

Unaenda mbali hata kutuita RUVU ZA KIWANDA.

Matangazo mengi ya kazi yataja waziwazi "Wazungu" ("Wazungu") tu, HAKUNA mweusi anaruhusiwa kuomba!

Kwa hivyo China inathubutuje kusema juu ya ubaguzi wa rangi.

Je! Unathubutu kujaribu kucheza mwathiriwa wakati uko mstari wa mbele? Nenda kwa mama yangu na unanyanyasa moyo wetu na kutuita majina na kufanya mzaha kwa tamaduni zetu, njia yetu takatifu ya maisha, haki yetu iko wapi?

Ninasikika kama mtu mweusi aliyekasirika kwa sababu mimi nimekuwa nikiona ubaguzi wa rangi mikononi mwa Wachina, na nimefanya amani na ukweli kwamba hivi ndivyo ilivyo China.

Je! Vipi kuhusu wewe kufanya jambo lile lile, ukubali hatima yako, "usahau tu"? Au labda unaweza kujifunza kutibu jamii zingine kwa heshima fulani?

Ninachosema ni kwamba, virusi hivi vinaathiri kila mtu, na ni shida kwa sisi sote, kitu kimoja na Ebola, watu wangu wametenganishwa, wametengwa kwa watu wengine na wanakabiliwa na ubaguzi mwingi wa rangi. Sio wewe tu anayepitia hii.

Hii ni vita yetu yote sasa. Virusi hii haioni rangi, haijui juu ya mabara au ukabila, inachukua kila mtu. Lakini ondoa ubaguzi katika hili, hauna nafasi katika hali hii, haifai.

ACHENI KABISA.

Hamkusema neno juu ya ubaguzi wa rangi wakati huo ulitokea kila dakika na kila saa kwa Waafrika kote Uchina.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante Amigoh
Mod pandisha hii tafsiri iungane na mada kisha weka huu uzi sticky
 
Baada ya maradhi haya, utaona harakati kubwa sana za serikali ya China kuwachanganya wachina na dunia. Tatizo litabakia labda kwa wahindi na waafrika wanaojiona wao ni bora kwa kuwabagua/kubaguliwa na races nyingine.
Ndugu Wewe unapenda kuchanganya na races zingine?Mimi hapana,najua thamani yangu.
 
HAKUNA WATU WABAGUZI HAPA DUNIANI KAMA WATU WEUSI WACHINA,WAZUNGU,WAHINDI TUNAWASINGIZIA TUU.........

YAANI TUKIWAONA WATU WEUPE TUNAANZA KUWASEMA HAWA NI WABAGUZI WAAFRICA TUWE KITU KIMOJA TUWAPINGE WABAGUZI

TUKIBAKI WENYEWE KWA WENYEWE TUNAANZA KUBAGUANA KWA MAKABILA NA DINI UTASIKIA MARA OHOO KABILA LILE HALIFAI KUSHIKA MADARAKA, MARA OHOO HUYU SIO MTANZANIA HALISI WENGINE WANAFIKA HATUA WANASEMA "TUUNDE UMOJA WA KABILA LETU NCHI NZIMA TUSAIDIANE SISI KWA SISI TUU"" BY GWAJIIII BOY .

KIUKWELI STAKI SEMA SANA ILA SISI WAAFRICA WABAGUZI NAMBARI MOJA APA DUNIAN

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hivi wewe kwa akili yako nani ameumizwa na ubaguzi wa rangi zaidi popote pale duniani, Mzungu au mweusi?

Umewahi kuona mtu mweusi anamuweka mzungu kwenye zoo ili watalii wamshangae?

Umewahi kuona Mweusi ananyanyuka kwenye seat ili asikae na mzungu?

Nani anarushiwa ndizi uwanjani, mzungu au mweusi

Umewahi kuona mweusi anafungua mgahawa na kisha kuandika BLACKS ONLY?

Umewahi kuona mweusi anafungua hoteli au Guest na kuzuia wateja wazungu wasiingie?

Sikiliza, Ubaguzi wa Mweusi ni ubaguzi wa kulipiza kisasi si ubaguzi halisi, ni ubaguzi wa kuonyesha protest ya ubaguzi mkubwa ambao wazungu waliufanya, ni ubaguzi wa hasira juu ya kuuzwa utwamwani, ukoloni, kudharauliwa, kubaguliwa kwa miaka mingi.

Sasa hawa wachina ni wafuata mkumbo tu, wanafuata yale ambayo wabaguzi wa kizungu walifanya kwa miaka 500 iliyopita.

Huwezi kutuita weusi ni wabaguzi zaidi kuliko wazungu wakati ushahidi uko wazi kuwa wageni wakija kwetu Afrika hawapati adha za ubaguzi kama mtu mweusi akienda kwao
 
Kudos Mkuu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ubaguzi siyo ugenini tu ,hapa hapa Tanzania tunabaguana usiseme. Wapinzani utawala wa CCM ni sawa na wazalendo wa Afrika kusini enzi za apartheid.
Siasa iki-occupy eneo kubwa la ubongo Hata wakati wa tendo la ndoa na mkeo/mpenzio utaleta siasa, ikienda haja utafanya kisiasa na mambo mengi

Haiwezekani mtu timamu azungumzie ubaguzi Tanzania kwa namna ulivyo china

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sie wenyewe tuna ubaguzi majumbani mwetu, nguo nyeupe tunazitenga na nguo nyeusi, nguo nyeupe tunaanza kuzifua kwa maji swafi na kuzianika kwa uangalifu, wakati nguo nyeusi tunazi purua purua na kuanika kawaida tu,
Ikidondoka nguo nyeupe tunashtuka na kuumia roho tunasuuza tena na kuanika, ikidondoka nguo nyeusi tunasonya, tunaikung'uta tunaanika,

Wito wangu; dhambi ya ubaguzi ipo ndani mwetu kuonesha kama tunaikataa basi nguo nyeupe na nyeusi zifuliwe kwa pamoja na kuanikwa pamoja.
 
Mbona waitali wairani nao wanatengwa haina hoja hio
 
Ubaguzi ni human nature wala utakiwi ukuumize ni asili ya viumbe vyote visivofanana kubaguana.Hata sisi twabaguana kwa rangi,dini,kabila,vyama,uchumi nk.
 
Wanajua tuna too boo koo dicks zinazopendwa na dada na mama zao,huku wao wakiwa na tudole gumba ambako hatuwaridhishi wanawake zao
 
Nakumbuka Kuna raia wa Malawi alifumwa akifanya mapenz** na mchina huko China alipigwa hadi akafa[emoji849][emoji849][emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…