Wachina watano mbaroni kwa kujeruhi Watanzania kwa sime

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu nane, wakiwemo raia watano wa China, kwa tuhuma za kujeruhi Watanzania wawili kwa kuwacharanga na sime, baada ya kutokea ugomvi kati ya Wachina wanaomiliki kampuni ya michezo ya kubahatisha, maarufu kama Bonanza na watu waliokuwa wanacheza mchezo huo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei, Mei 25, mwaka huu saa 11 jioni maeneo ya Soweto Kata ya Ruanda jijini hapa, watu wawili Abison Hamis (36) na Gilbert Mwakanyema (32) wote wakazi wa Manga Veta, walijeruhiwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na raia wa China, kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ambao ni Watanzania.

Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka kati ya mfanyabiashara na raia wa China, Chen Yen (43) anayeishi Veta jijini hapa na Hamis maarufu kwa jina la Ndele, baada ya Mtanzania huyo kutamka neno la Kichina, lililomuudhi Yen na kusababisha ugomvi uliosababisha baadhi ya watu kujeruhiwa.

Akifafanua, alisema awali raia huyo wa China alifika eneo hilo kuchukua fedha kwenye mashine ya mchezo wa kubahatisha ya Kampuni ya Bonanza akiwa amefuatana na dereva wake, Gift Elia (23) maarufu kwa jina la Mwamelo anayeishi Airport, wakiwa na gari yenye namba za usajili T 252 DNL aina ya Toyota Kluger katika eneo lijulikanalo kwa jina la Sports Centre, linalomilikiwa na Salum Juma pia wa jijini Mbeya.

Alisema wakati huo, Hamis alifika eneo hilo kucheza “pool table” akiwa ameongozana na Gilbert Mwakanyemba, Kennedy Mwamlima na mwenzao aliyefahamika kwa jina moja la Yohana.
Alisema baada ya kuzuka kwa ugomvi huo, Yen alipiga simu kuomba msaada kwa wenzake, ambao walifika na kuanza kuwashambulia akina Abison na Gilbert kwa sime maeneo mbalimbali ya miili yao.

Alisema waliokamatwa ni Wachina Yen, Xiao Jing (30), Lin Hai (30), Lyu Qzing (36), Jiang Ze Dong (39) wote wakazi wa Meta jijini hapa na Watanzania Elia, dereva na mkazi wa Airport, Herman Elius maarufu Mwalwiba (20) dereva na mkazi wa Esso na Mwamlima (28) dereva na mkazi wa Ituha jijini hapa.

HabariLeo
 
Hahah jamaa kawaita wakali wa wu shu wakatumia masime kuwajeruhi wakamaria😂😂😂!!!

Tuacheni upuuzi jamani, hii awamu hamna mtu anataka kufanyiwa comedy za kitoto.
 
Hawa wajinga (wachina) wanadharau sana,ila nadhani ifike wakati tuache kutowaadhibu hawa jamaa
 
Hao wachina wakae celo muda mrefu ili wajifunze

Ingekuwa WATANZANIA wamefanya hivyo huko China wangefanywaje? Hawa wafungwe jela [ without an option of a fine] na baada ya kutumikia kifungo warudishwe kwao ili liwe fundisho kwa wachina waliobaki nchini wanaodharau wananchi.
 
Hao wachina wafungwe maisha,kwa kosa la kujichulia sheria mkononi.
 
Nimefedheheka sana Wachina Watano kuwashinda Wanaume wooote wa Mbeya waliokuwepo maeneo hayo ya karibu. Daaaah pole sana walioumizwa
Mbwembwe zao huishia kwa wake zao huku michepuko ikiwachuna bila gharama wala haishangazi.
 
Hao watu wambeya ni Mazoba wa Mwisho,How come Mchina anakujeruhi kwa Silaha na watu wangine wanaangalia tu?Tena Mchina si bora wangekuwa taifa jengine,Hiyo ingekuwa Vita.
 
wangekuwa wa bongo ndio wamefanya hayo yaliyofanywa na wachina sijui tu hali ingekuwaje huko ktk nchi yao. Ila kwa kuwa ni bongo hatupendi makuu..hili litaisha TU.
 
POLISI mkoani Mbeya inawashikilia watu nane, wakiwemo raia watano wa China, kwa tuhuma za kujeruhi Watanzania wawili kwa kuwacharanga na sime, baada ya kutokea ugomvi kati ya Wachina wanaomiliki kampuni ya michezo ya kubahatisha, maarufu kama Bonanza na watu waliokuwa wanacheza mchezo huo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei, Mei 25, mwaka huu saa 11 jioni maeneo ya Soweto Kata ya Ruanda jijini hapa, watu wawili Abison Hamis (36) na Gilbert Mwakanyema (32) wote wakazi wa Manga Veta, walijeruhiwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao na raia wa China, kwa kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubahatisha ambao ni Watanzania.

Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka kati ya mfanyabiashara na raia wa China, Chen Yen (43) anayeishi Veta jijini hapa na Hamis maarufu kwa jina la Ndele, baada ya Mtanzania huyo kutamka neno la Kichina, lililomuudhi Yen na kusababisha ugomvi uliosababisha baadhi ya watu kujeruhiwa.

Akifafanua, alisema awali raia huyo wa China alifika eneo hilo kuchukua fedha kwenye mashine ya mchezo wa kubahatisha ya Kampuni ya Bonanza akiwa amefuatana na dereva wake, Gift Elia (23) maarufu kwa jina la Mwamelo anayeishi Airport, wakiwa na gari yenye namba za usajili T 252 DNL aina ya Toyota Kluger katika eneo lijulikanalo kwa jina la Sports Centre, linalomilikiwa na Salum Juma pia wa jijini Mbeya.

Alisema wakati huo, Hamis alifika eneo hilo kucheza “pool table” akiwa ameongozana na Gilbert Mwakanyemba, Kennedy Mwamlima na mwenzao aliyefahamika kwa jina moja la Yohana.
Alisema baada ya kuzuka kwa ugomvi huo, Yen alipiga simu kuomba msaada kwa wenzake, ambao walifika na kuanza kuwashambulia akina Abison na Gilbert kwa sime maeneo mbalimbali ya miili yao.

Alisema waliokamatwa ni Wachina Yen, Xiao Jing (30), Lin Hai (30), Lyu Qzing (36), Jiang Ze Dong (39) wote wakazi wa Meta jijini hapa na Watanzania Elia, dereva na mkazi wa Airport, Herman Elius maarufu Mwalwiba (20) dereva na mkazi wa Esso na Mwamlima (28) dereva na mkazi wa Ituha jijini hapa.

HabariLeo
Tatizo wabongo wanazngua sana wamebuni njia ya kuhack machines za bonanza ambayo wanatoboa tsh 200 kisha wanaifunga uzi wakitumbukiza kwenye bonanza mara nyingi kwa kurudia machine inatema pesa ndefu, itakuwa wachina waliwastukia wabongo maana wakikusanyaga pesa kwenye machine zao uwa wanazikuta baadhi ya 200tsh zilizotobolewa
 
Wasamehewe,,wachina ndio wamewafikisha hapo mlipo,,mwanzo mlikua mnazurura tu mzazi akiuza bisheti mnapatiamo kiasi cha karanga,,,leo hii mnatumia bidhaa zake kula mnakula vizuri milo mi4 kwa siku. Wasameheni tu wajameni
 
Back
Top Bottom