Wachumi Na wafanyabiashara tushauriane, naanzisha biashara ya kukopesha

Kweli kaka , ni kama kias gan Na wapi PA kuanzia[/QUOTE]
Anza wilayani upate leseni ya biashara hiyo, sidhani kama ni zaidi ya 50,000/=.
Pili nenda TRA iliyopo karibu na wewe, uwe na mahesabu mazuri, yaani forecasts, naomba urekebishe kuhusu hesabu ya kukopeshana, naona umeweka kama utapata faida sana au una chaji riba kubwa sana.
Amuwa kwa kuwaambia TRA unachaji riba 25% kwa mwezi ya hela akopayo mtu, watakuuliza mtaji wako, tafadhali kuwa makini hapa, nadhani uanze na 1m/- kwanza...
Maana lazima watakupigia mahesabu kabla hata hujaanza biashara?! Kichekesho, ila ndivyo walivyo!
Waweza kuni PM nikupe maelezo zaidi mkuu..
 
Fanya marketing mfano kwa wamama ntilie,chagua kama 50 hivi wale unaona biashara zinatoka,wengi wao malighafi wananunua daily madukani mfano mchele,maharage,ngano etc juu hawana mitaji mikubwa,
waelimishe faida ya kununua in bulk jinsi itakavyowapa faida,
kisha unawambia unatoa microfinancing,kwa interest ya 30%,utawapata tu maana mtu atataka anunue mchele,ngano kwa bei ya jumla ili awe anauza,anarejesha pesa na kubaki na faida,

tatizo moja tu hawa wamama wanatumia teckno za elfu 20,
sasa sijui thamana atawekesha nini
 
Fanya marketing mfano kwa wamama ntilie,chagua kama 50 hivi wale unaona biashara zinatoka,wengi wao malighafi wananunua daily madukani mfano mchele,maharage,ngano etc juu hawana mitaji mikubwa,
waelimishe faida ya kununua in bulk jinsi itakavyowapa faida,
kisha unawambia unatoa microfinancing,kwa interest ya 30%,utawapata tu maana mtu atataka anunue mchele,ngano kwa bei ya jumla ili awe anauza,anarejesha pesa na kubaki na faida,

tatizo moja tu hawa wamama wanatumia teckno za elfu 20,
sasa sijui thamana atawekesha nini
 
Kila wiki urejeshe elfu 40, 60 au 80?? Kama ningekuwa na guarantee ya kuipata hiyo kila wiki nisingekuja kukopa wala..issa NO for me, super high interests for a regular person. Hiyo si biashara hiyo ni greedy
 
Hapa kweli mkuu umenipa mwanga
 
Hiyo ni changamoto ya techno, lakin kama wakiwekewa utaratibu wa.kurejesha mwa amwamu, yaan unampa 50, kila siku akupe 2500 tu kwa mwezi yaan siku 30 kwanza ni affordable pili ni peaceful way of repayment haiumizi, nitatenga mamantilie 100 tu jiji la dar, unawapa 100,000 kila mtu then daily warejeshe 5000 tu ndani ya mwezi
 
Hivi hii inaruhusiwa kweli kisheria ? Kuna uzi mmoja wadau walikuwa wanasema biashara ya kukopesha haruhusiwi mtu binafsi labda iwe bank au viccoba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa hivyo vigezo na mashart utashinda Sana mahakamani
 
Hili swala linafanyika sana nchi za magharibi pawnbussiness changamoto ni huku kwetu sheria zimekaa vipi maana lazima itakurazimu uwe na mwanasheria wako, swala la kudai ni gumu mno, jwa uzoefu wangu afisamikopo kudai ni ngumu sana
 
Hiko kiasi cha riba ni kama biashara itakushinda maana microfinance nyingi ni 18% hadi 20%
 
Sijawahi ona riba kubwa kama yako duuuh. Yaani 50,000 kwa week mtu alipe 75,000? Kiukweli atakayekuja kukopa kwako ni yule asiye 'na sehemu ya kukopa kabixa kwa bei nafuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nitaanza kukopesha kama wewe ila nitafanya kama ifuatavyo 50,000/= riba itakuwa ni 5,800/= na 100,000/= riba yake itakuwa ni 15,800/=
 
Kwa hivi viwango vya riba ukipata wakopaji wengi watakuwa sio walipaji watakuja kwa sababu wanashida ila kwa lugha nyepesi watakuwa wapigaji dhamana za uongo nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…