Ningependa kupewa ufafanuzi wa kiuchumi ni hali ipi huwa ina unafuu
A. Mzunguko wa pesa kuwa mdogo ila bei za bidhaa / huduma ni kawaida.
Awamu hii ilisifika kwa msemo maarufu vyuma vimekaza, mzunguko wa pesa ulipungua kwa sababu biashara nyingi zilifufungwa ama kusua sua, hakukuwa na ongezeko lolote la mishahara, pesa mtaani ilipungua sana yani , hata ile nguvu ya kununua ilipungua ila be zilikuwa kawaida
B. Mzunguko wa pesa kufufuka ila bei zinakuwa zimepanda
Kwa sasa biashara nyingi sana zinafunguliwa na hata zile zilizofunga virago awamu iliyopita zimerudi,
mishahara nayo imeongezeka, ndivyo vitu vikuu vilivyoongeza mzunguko wa pesa ila bei nazo zimepanda,