Wachumi tuambieni parameters atakazotumia makonda kushusha bei za vinywaji

Wakuu kwenye soko Kuna kitu/factor kinaitwa price elasticity, hapa ndipo atakapokwama. Muda alioutaja (6hrs) hauwezi kuaccomodate hiyo price elasticity. Kwa kifupi hakuna parameter itakayoapply kwa kuwa induced by external forces. Hiyo inawezekana tu kama sellers and retailers wakikubali na wakawa na utayari wa Kufanya hivyo. Siasa kwenye masuala ya kibiashara huwa haifiti sana.

NB:Kauli kama hizi huwa zina nguvu sana kwenye spot Market, kama vile stock and currency exchange market and not otherwise.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je?
1.TRA ITASIMAMISHA WAJIBU WAKE KWA 6 HRS?

2.MASHINE ZA MALIPO ZITAKUWA MUTED?

3.SERIKALI ITATOA SUBSIDY?

AU ITAKUWAJE? maana naibu rahiisi kasema hashindwi kwa tangazo hili lisilo na mipaka ndani ya jamhuri!

Mbeya jiandaeni kula gambe!!

chid benz naomba haka msaidie makonda kuwa mshauri wake.maana kazi ya mkoa haja ijua mpaka sasa
 
Je?
1.TRA ITASIMAMISHA WAJIBU WAKE KWA 6 HRS?

2.MASHINE ZA MALIPO ZITAKUWA MUTED?

3.SERIKALI ITATOA SUBSIDY?

AU ITAKUWAJE? maana naibu rahiisi kasema hashindwi kwa tangazo hili lisilo na mipaka ndani ya jamhuri!

Mbeya jiandaeni kula gambe!!
Hamna vyovyote ambavyo theory za uchumi zinaweza kutuelekeza kwa mkuu mkoa kuingilia bei za bithaa sokoni. Isitoshe kwa sheria zetu hazimpi nafasi mkuu wa mkoa kuingilia utaratibu wa ukusanyaji mapato hapa Tanzania.

Jambo pekee linalowezekana ni kwa mkuu wa mkoa kuamua kutumia ushawishi wake KUWASHAWISHI wazalishaji na wauzaji wa vinywaji kukubali kuuza kwa bei pungufu. Na hapa naamaanisha itakua ni kuwaomba wakubali, maana wanaweza kukataa pia na wakawa hawajavunja sheria.

Ili kufanikisha hilo, anaweza kukubaliana na wazalishaji/ wauzaji kuweka maeneo maalum (kama vile alivosema watafunga baadhi ya mitaa) ambapo hapo vinywaji vitauzwa kwa bei pungufuu kwa kipindi cha masaa 6.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anachoweza kufanya Bashite ni kuleta magari ya vinywaji uwanjani au maeneo maalum yenye punguzo hilo la bei, Otherwise uratibu wake mkoa mzima ni ngumu,
 
Kuhusu huyo mtu upeo wake ni kama GENTAMYCINE au lemutuz, wanafanya ujinga ila ule ujinga wao wanauona ni ishu ya maana.

Jambo la hatari linakuja kwamba ukiwaambia nyie ni wajinga, arrogance yao inasema kwamba hiyo ndio IQ.?

Ninachofurahi tu ni kwamba nafananishwa na Watu mbalimbali na hatimaye leo tena nafananishwa na Le Mutuz wakati huko nyuma nilishafananishwa na Nape Nnauye mara Haji Manara mara tena Shaffih Dauda baadae tena nikafananishwa na Humphrey Polepole huku wengine pia wakinisema Mimi ni Hussein Bashe yaani ni Kufananishwa tu na Watu kila mara. Nadhani sasa labda nimebaki tu Kufananishwa na Baba yako Mzazi au Yesu Kristo au Mtume Muhammed.

Kweli GENTAMYCINE nawateseni na nawahenyesheni mno. Na hapa bado mtanikoma hadi mtanyooka na kwenda nitakavyo. Na labda kwa Faida yako / yenu tu Naitwa Kalemera Rwigyema Mazimpaka nina Uraia Pacha wa nchi tatu za Afrika Mashariki Tanzania, Rwanda na Uganda ( na usiniulize ni kwanini nina huu Uraia kwani si Kazi yako na wala haitokusaidia na cha Msingi jali tu Maisha yako ) na Shughuli zangu ni Kubwa tatu tu ambazo hata Mdau wangu britanicca anazijua ambazo ni 1. UKULIMA, 2. UFUGAJI na 3. UVUVI.

Elimu yangu ni ndogo sana siyo kama zenu yako / zenu Kubwa mlizonazo ambapo ninapambana sasa Kumalizia Masters Degree ( Shahada ya Uzamili ) ili nikimaliza hiyo nifanye tena Masters Degree yangu nyingine na mwishoni nije Kuanza Doctorate Degree yangu. Nia na madhumuni nataka nami nijitahidi nije kuwa Msomi kama Wewe na wale wote mnaonichukia kwani nyie Wenzangu mmesoma sana na kuelimika mno.

Mwisho kabisa utake usitake kama nitaendelea kuwa Hai hivi basi kati ya mwaka 2045 au 2055 kwa ' Mikakati ' yangu ambayo hata hivyo inaenda vizuri tu ndiyo nitakuja kuwa Rais wako wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo itakuwa ni Historia kwa mara ya Kwanza Mtandao huu wa JamiiForums kutoa Rais. Na labda nianze Kukuahidi tu kuwa nitakuwa Mmoja wa Marais wazuri sana ambao Tanzania hamkuwahi kuwapata ambapo nami nitafuata vyema nyayo za Marais niwapendao waliotawala Tanzania wakianzia na Kipenzi changu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Benjamin Mkapa na huyu Rais wa sasa Dkt. John Magufuli.

Ni haya tu kwa sasa na naomba bandiko hili ' Wafowadie ' pia na wale ' Wapumbavu ' wenzio wote na lisambae upesi sana.
 
Mbona simple sana mkuu! Atafanya kila njia tufungwe tu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii combination ya kusaidia taifa stars imeniacha hoi, eti dab, sepenga eti nini sijui! Nilitegemea kuona kataraia majeshi Minziro, Tenga, Mkwasa nk. Sasa kundi la bongo movie ndo linasaidia football! Siendi wala sitaki kusikia hiyo mechi.
 
Mkuu ianelekea we hapa ndo unaongoza kwa kufananishwa na watu
 
Itakuwa anampango wa kuchachusha machozi kuwa bia, kama yesu alivyobadilisha maji kuwa divai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…