Wanalamika pale interests zao zinapoguswa. Kama kweli wao ni Watu wa Mungu, mbona hawakutoa tamko lolote wakati wanachama wa CHADEMA walipopigwa na Green Guards wa CCM kule Busanda, kama ilivyotokea, na hatimaye hao waliopigwa kufunguliwa mashtaka ya kufanya fujo na Polisi? Haki ilikuwepo kweli?
Hawa si Watu wa Mungu hawa?
Mara kadhaa kwenye hotuba za Salat Jumaa, Masheikh wanatuhubiria Waislam kuyakemea maovu tunapoyaona. Sisi Waumini tunakemea, wao walimu wetu wanapaswa kuwa mstari wa mbele. Mbona hawakemei?
Leo, misamaha ya kodi imeondolewa, ndio wanakaa kimya? Mbona Waziri Nagu (kabla ya muswada huu kwenda Bungeni) alitangaza kusudio la Serikali kufuta misamaha ya kodi kwenye taasisi za kidini na NGO? Ina maana hawakuliona? Au walidhania serikali inafanya dhihaka?
Well, hii si dhihaka, hii ni sabotage kwa Watanzania. Sasa nadhani mnaelewa wapi CCM inaelekea. Mkiichagua tena 2010, litakalotokea shauri yenu. Mimi simo!
./Mwana wa Haki
Mbowe: Nataka kugombea Moshi Vijijini, tumwondoe Kimaro.