Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

Wachungaji na Mashehe wanafiki! - Mmevuna mlichopanda!

Religions ni non gv organizations. Kazi yake ni kutangaza mazuri na kukuza jamii kwa kupitia imani, inter-alia, Polisi na Serikali are practicing the same laws by executing and/or inforcing exisiting laws of the state kwa jamii. Sasa, unapoona kuwa viongozi wa dini wanatumia organization zao za kidini kujinufaisha, na ukaa kimya, basi na wee kwa njia moja au nyingine unachangiza kuvunja haki, and you are liable for obstracting justice by not reporting the issue to the GV, inter-alia, same is applicable to the gov leaders.

Kwa Serikali ku optout tax exemption kwa religion organizations si jambo la burasa na/au jema, kwasabau bado kuna viongozi wa kidini ambao wana integrity ya juu na si mafisadi, na ukifuatilia organizations zao utaona au gundua kuwa bado zinasaidia watu wengi vijijini na organizations hizo ni safi, to wit. Furthermore, it may open other doors which were not open na kukuza ufisadi kwa njia ambayo bado haijulikani, kupitia hizo interim conduits.

Ingekuwa kwa best interest kwa jamii, kama Serikari ingetoa undani halisi na sababu halisi za ku optout exemtion kwa dini, than coming to a general conclusion kuwa exption is prohibited, null and void, ad infinitum, for what ever reasons they have to religious orginzations.

It is my prayer that, the GV of Tanzania will re-consider/review again their decision towards religious organization's tax exemption pursuant to the laws of TZ, and see if it is profitable not to have them.

God bless Tanzania.

Max Shimba, A Bondservant of Jesus Christ
 
Je NGOs ziko tayari zikaguliwe mahesabu yake ..na independent Auditors kama CAG anavyofanya serikalini?

Hizi NGOs ziko Accountable kwa nani??
 
They are NGOS and are accountable to themselves. They can be audited if it is discovered that they are knowingly and consciously abusing the privileges they have as NGOS and breaching the laws of the sovereing State, and if proven gilty, they will be prosecuted.
 
NB

I don't think it is ethical to tax religious organizations, iter-alia, I don't see any merits, to wit, due to the fact that religious organizations are charitable and educational.

I feel the decision of opting out exemption from religious organization, if is passed and become a law, is malicious, unethical, and lacks merits.
 
ZeMarcopolo,
Mkuu huwezi kuweka fixed amount kwa sababu kila kijiji au sehemu inahitaji vitu tofauti.. Swala kubwa ni ufuatiliaji wa hii misaada. kama mtu kaingiza mabati 4,000 project nzima inayohitaji mabati 4,000 inatakiwa kupitishwa na vyombo vya serikali toka huko kunakohitajika. Hatua kwa hatua.
Kama kanisa linajenga shule ya sekondary au Zahanati ni lazima kiongozi wa serikali iwe wilaya au mkoa ana habari kwamba kanisa au Zahanati inahitaji mabati 4,000. Mara zote hizi NGOs huomba misaada kutokana na shida iliyopo na kama wamepewa mabati 4,000 ina maana initial plan waliyowakilisha kwa wadhamini ni ujenzi unaohitaji mabati hayo... Hiyo plan iko wapi na nani kaipitia hadi kupitisha mabati 4,000 ambayo hayahitajiki..
Hivyo kinachotakiwa ni mkono wa kiongozi wa serikali..mara zote misaada inayoingia nchini huwa tayari matatizo yapo na hesabu kamili ya kile kinachohitajika ipo..Huwezi kujenga kanisa linalotaka mabati 200 yakaingizwa 4,000 bila chombo cha serikali kufahamu yalihitajika mabati 200 tu..
Hii inaonyesha uzembe uliopo sii wa NGOs bali serikali yenyewe.. Hivyo kilichotakiwa kufanywa ni kuhakikisha kuna misingi bora ya kupokea misaada kama hii na jinsi ya kuepuka wizi kama huu..Kutolipa kodi ni criminal case na sheria zipo iweje tutafute sababu nje ya kosa la wazi kama hili!.

Utaratibu ulioshauri ni bora zaidi, ila kwa vile wasimamizi wa ukusanyaji kodi wamedhihirisha kuwa lele mama, na wanaosimamia uendeshaji wa NGOs vilevile ni lelemama. Na kwa vile NGOs nazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa notorious kwenye hili, basi solution inayobaki ni kwamba NGOs zilipe kodi. Kodi hiyo itaingizwa kwenye mifuko ya maendeleom na hapo hakuna atakayeumia na gharama za uendeshaji zitapungua. Hata misamaha kwa wafanyakazi wa serikali na wabunge pia ilibidi ifutwe.kwanini misamaha iwaguse wafanyakazi wa serikali tu na tena wale wenye mshahara mkubwa kuanzia ngazi ya D?!
Misamaha ndio inaleta mianya ya ukiukwaji kodi. Futa hii misamaha tukusanye kodi ya kujenga nchi.
 
NB

I don't think it is ethical to tax religious organizations, iter-alia, I don't see any merits, to wit, due to the fact that religious organizations are charitable and educational.

I feel the decision of opting out exemption from religious organization, if is passed and become a law, is malicious, unethical, and lacks merits.


Max,
Tatizo lililopo ni kwamba hizo relig orgs zimeshindwa kujitunzia heshima kama relig orgs. Angalia mfano wa viongozi wa dini waliokuwa wanaendesha DECI. Hivi viongozi kama wale uwaachie kodi, kweli hawafanyi biashara juu ya msamaha huo?! Tulipofika sasa inabidi vyama vya dini vilipe kodi.
 
DECI kama walikuwa wezi wachukuliwe hatua za sheria. I wonder how long does it take for the GV of TZ kugundua mafisadi kama DECI? Inashangaza kupita kiasi.

Lakini, wabaya wachache si sababu ya kufungia wengi ambao ni wazuri. In every group of people, there are few Judas, it is an escapable situation. All they have to do is to create laws that will deal with such people, and prohibit fictitous and unverifiables DECI/UPATUS. The GV has to deal with situations na sio to run away from them.
 
Je NGOs ziko tayari zikaguliwe mahesabu yake ..na independent Auditors kama CAG anavyofanya serikalini?

Hizi NGOs ziko Accountable kwa nani??

Bla bla bla tena. Kwani kila wanaopewa exemption wote huwa wanakaguliwa na CAG? Hivi makampuni ya madini ambayo kwa miaka na miaka yamepewa exemption yanakguliwa na CAG?
Kuna guide lines zinazoongoza hesabu za serikali na kumfanya CAG kujihusisha na kukagua hesabu za mahali fulani! Si kila taasisi CAG atakagua yeye.
 
NB

I don't think it is ethical to tax religious organizations, iter-alia, I don't see any merits, to wit, due to the fact that religious organizations are charitable and educational.

I feel the decision of opting out exemption from religious organization, if is passed and become a law, is malicious, unethical, and lacks merits.

Kuna taasisi za kidini zina mipango ya kufungua benki. How is this charitable and educational?
 
Jamani someni mawazo ya viongozi wetu kwa ndani msiangalie fuvu. Ngoja niwakumbushe kidogo matukio mawili kisha muone mtatumia kipimo gani kutafakari uwezo wa kufikiri wa viongozi hawa.
1. Uvunjaji wa maadili ya vyombo vya habari dawa yake ni kuweka sheri ya kila mmiliki awe na chombo kimoja tu cha habari i.e. Gazeti au Redio basi
2. Ukwepaji wa taratibu za misamaha ya kodi kwa baadhi ya mashirikia husika dawa yake ni kufuta misamaha hiyo
3. Ukionyesha dalili ya kukataa ilani ya chama mwanafulani dawa yake ni kukuwekea nguzo wakati wa uchaguzi na kuamini umeme unakuja kesho kumbe danganya toto.
Swali
Hivi mtoto akinyea mkono dawa ni moja tu kukata mkono au mtoto mtoro shuleni dawa yake ni kuifunga kabisa shule?
Nisaidieni tutumie kipimo gani kujua uwezo wa kufikiri wa viongozi wetu.
 
Kama Marekani inamtoza Obama kodi na yenyewe ni nchi tajiri, sisi ni nani tusamehe JK, mawaziri, wabunge, wawekezaji na taasisi za kidini kodi?

Halafu tunadai hatujui kwanini sisi ni maskini.
 
Mungu hatozwi kodi kwasababu dunia niyake tumemshkia...lol

Hakuna anayetaka kumtoza Mungu kodi. Walengwa ni wale wanaonunua mabati 4,000 yaliyosamehewa kodi kwa jina la Mungu, kisha Mungu wakampa 200 tu na 3,800 wakauza kwa bei ya soko na kuweka hela mfukoni.

Tusichanganye madawa.
 
Kuna taasisi za kidini zina mipango ya kufungua benki. How is this charitable and educational?


Once such a "NGO" opens a profitable corp/institute, then a new corp/profitable one will be charged and taxed just like any other institution.

Remember, the laws does not prohibit NGOS to open and operate a profitable corp.
 
Hiyo kodi watakayotozwa na serikali si itatumika huko huko kwenye community development (kujenga mashule, kununua madawa nk.)?

After all dini zingine (mfano ile dini ya Kakobe, etc.) ni private owned na hazina mchango wowote kwenye community development (hakuna cha hospitali, shule, nk - pesa yote wanaweka mfukoni).

Ni kodi ngapi zilizokusanywa toka enzi hizo na bado hazijaweza kufanya kile kilichofanywa na mashirika haya ya dini?

Tusijisahau kwa kuwa tuna maisha mazuri fikirieni wale wa vijijini ambao wamekuwa wakilishwa na kunyeshwa na mashirika haya ya dini. Zahanati zao vimekuwa zikifadhiliwa na haya mashirika ya dini ndio maisha ya watu walio wengi nchini yanakwenda.

Ni wazi kuna mianya katika sheria na sera za nchi lakini suluhisho si kufuta kodi kwa mashirika haya bali kuziangsalia upya sheria hizo ili kuzuia watu kutumia vibaya misamaha hiyo.

Serikali ikubali kuwa imekuwa ikilegalega katika usimamizi mzima wa misamaha hii na katu isitoe adhabu kwa watu wasiostahili kwani kwa kufanya hivyo watakaoumia si viongozi wa dini tu bali hata wananchi wanaotegemea huduma nafuu zitolewazo na mashirika hayo
 
Mwenyezi Mungu anataka Wachungaji na Mashehe walipe kodi.

Wamepanda magugu yameota!
 
Kisa cha Kanisa Katoliki kuingia kwenye 'Elimu ya Siasa' !

HABARI za uongo zilipelekwa kwa wafadhili na baadhi ya watu toka kanisa hilo eti kwa kuwa nchi ina rais Muislamu rais huyo hataki wananchi wapewe elimu ya siasa na ya uchaguzi.

Kutokana na hili kanisa hilo liliombwa kuomba fedha za kuendesha elimu hiyo ya siasa na uchaguzi nchini kwa mwaka 2008-2009. Maombi yalifanywa kwa njia rasmi na zisizo rasmi na hivi sasa kanisa hilo lina mabilioni kwa ajili ya kuendesha elimu hiyo ya siasa na uchaguzi.

Ili 'kujustify' hilo hivi karibuni maaskofu wa kanisa hilo wamelazimika kujitokeza mara kwa mara kwenye vyombo vya habari ili waonekane wanafanya kazi waliyokubaliana na wafadhili wao.

Bila shaka umewahi kuwaona mara kadhaa maaskofu hao kwenye vioo vya luninga, magazetini na hata katika shughuli za kupanda miti ambazo huko nyuma yalichukuliwa ni mambo ya kawaida hivi leo yanaonekana muhimu kiasi cha kuwaita wapiga picha wa magazeti na televisheni kuwanasa viongozi hao watukufu.

Of kozi, wapiga picha wa magazeti na televisheni ambao asilimia 60 yao sio wa dhehebu hilo hufika hapo sio kwa sababu za imani bali kutokana na mshiko mnono unaomwagwa na makuwadi wa viongozi wa kanisa hilo.

Hatuwezi kuwalaumu kwa sababu na kiongozi wa nchi naye ameonesha njia ya kuwanusuru Watanzania ni kuwa ombaomba. Na wao wameamua kuwa ombaomba. Na mfadhili kama ilivyo kawaida yake akishakupa msaada inabidi ufuanye atakayo. Na hayo ndio matunda ya msaada iwe kwa serikali au kanisa-hayajali kama tutalinda umoja na amani yetu bali tu waliofaidika wahalalishe KULA kwao kwa kunawa kwao kwa sabuni na maji ya sumu na kufuta kwao mikono kwa taulo ya sumu. Na sumu imeshaingia, suala sasa ni je itachukua muda gani kufanya kazi.

Kinachoendelea nchini sio kitu kinachoacshiria Wakiristo kuwachukia Waislamu au waislamu kuwachukia Wakiristo au Wakatoliki kuichukia CCM na serikali yake bali ni vita vya viongozi wa kanisa hilo kuona NANI, NINI, KWANINI, WAPI, LINI na kadhalika ANAPATA nini na wao wanajiona kama wacha Mungu na watu wanaoongoza kanisa lenye fedha nyingi nchini wanastahili daima kupata zaidi kuliko wanasiasa au watu wa dini nyingine.

Tuwe macho na viongozi wetu wa dini Tanzania, maana njaa yao kali, inaweza kuwasukuma kusababisha tuanze kusukumana na kuburuzana huku ndani wakati wao wanakula na kusaza na wanalala katika vitanda bora na vya thamani ijapokuwa hawana wa kuwaliwaza au wanao ?
 
Uwiano Maalumu,

Mimi huwa najiuliza: hivi Raisi, VP, WM, JM, Spika, Raisi wa Zanzibar..je hulipa kodi kiasi gani??

Je sii haki yetu sisi raia kujua ni kodi kiasi gani hawa wanalipa kila mwaka??

Soma hapo chini......from ITA 2004!


The following amounts are exempt from income tax -
(a) amounts derived by the President of the United Republic
or the President of the Revolutionary Government of
Zanzibar from salary, duty allowance and entertainment
allowance paid or payable to the President from public
funds in respect of or by virtue of the office as President;
Act No.5
of 1986
Cap.245
(b) amounts derived by the Government (including Executive
Agency established under the Executive Agencies Act,
1997) or any local authority of the United Republic or by
the Revolutionary Government of Zanzibar or any local
authority of Zanzibar except amounts derived from
business activities that are unrelated to the functions of
government;
(c) amounts derived by any person entitled to privileges under
the Diplomatic and Consular Immunities and Privileges
Act to the extent provided in that Act or in regulations

made under that Act;


Ngoja nipitie matundiko yawadau wengine then tacomeback kwa comments zangu on this!
 
Kabla hamjashabikia kuhusu kufutwa hii misamaha ya kodi tujuilize yafuatayo:
1. Ni kina nani hasa wanaosamehewa hizo kodi?
2. Hiyo misamaha ya kodi inawafaidisha vipi watu masikini ambao hawana hata uwezo wa kulipa kodi?

Sasa niwape ya kwangu.

Kutumia kigezo cha taasisi za kidini kama sifa ya kusamehe kodi ni kosa kubwa maana humo ndani yao pia kuna ufisadi mkubwa. Misamaha inayotolewa ya kodi kwa taasisi za kidini kwa kiasi kikubwa bado iaishia kufaidisha watu matajiri na kuwaacha masikini wakiendelea kuteseka. Nina mifano.

Shule kama St Marian kule Bagamoyo, St Francis, St Mary Goreti ya Moshi na nyingine za namna hiyo zinazosifika zinaeleweka kuwa ni za taasisi za dini, kwa hiyo zinapata msamaha wa kodi. Lakini hebu nenda leo kwenye shule hizo kama utakuta mtoto wa masikini! Loh atafikaje humo, wamejaa watoto wa mafisadi tu! Shule ada tu ni zaidi ya milioni, eti nao wanataka wasamehewe kodi, si ufisadi huo ni nini? Wanakusanya hela nyingi, karo aghali sana bado hawataki kulipa kodi? Walipe kodi kama wafanyabiashara wengine!

Mimi nitasapoti msamaha wa kodi kwa shughuli zinazolenga masikini kweli, ama za misaada ya kibinadamu. Yale mahospitali ya misheni vijijini ambako watu wanapata huduma bure au kwa gharama ndogo sana, yaendelee kupata msamaha wa kodi maana msamaha huo unawafikia wahitaji. Na yeyote anayeanzisha huduma kama hiyo apate msamaha huo, sio lazima iwe taasisi za dini tu. Lakini hii ya blanketi la msamaha wa kodi kwa kila taasisi inayojiita ya kidini ni wizi mtupu.

Hakuna anayezuiwa kufanya biashara. Kama taasisi za dini zinafanya biashara kama hiyo niliyoona kwenye hayo mashule niliyotaja, zilipe kodi kama wengine, wasitake kutuibia kila siku.
 
Back
Top Bottom