Kwa nini isiwe viongozi wa dini -- unatumia mashehe na wachungaji ( hujataja mapadri )
Mazee it seems like hapa tulikuwa tajadiliana vitu visivyokuwepo. Waziri Mkulo kwenye taarifa ya habari ya saa mbili amenukuliwa akisema kodi iliyoondolewa ni kwa bidhaa/vifaa viingizwavyo nchini na mashirika ya kidini kwa minajili ya kibiashara.
(xii) Kuondoa msamaha maalum wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT Special Relief) kwa asasi zisizo za kiserikali (NGOs) na
mashirika ya dini. Hatua hii itahusisha madhehebu yote ya dini
ambayo ni pamoja na Waislamu, Wakristo, Wahindu, Mabohora
nk. Hata hivyo, vifaa vya kiroho na ibada vitaendelea kupata
msamaha wa kodi;
Kwa nini isiwe viongozi wa dini -- unatumia mashehe na wachungaji ( hujataja mapadri )
Nadhani unahitaji ku-revise chanzo cha umaskini nchini. FYI, Chanzo cha umasikini wa mtu mweusi ulianza hata kabla ya kuja kwa wakoloni na dini za kigeni.
Mwanaharakati kwanza naomba ufute usemi wako kwamba mashehe na mapadri ni wanafiki.Wanalamika pale interests zao zinapoguswa. Kama kweli wao ni Watu wa Mungu, mbona hawakutoa tamko lolote wakati wanachama wa CHADEMA walipopigwa na Green Guards wa CCM kule Busanda, kama ilivyotokea, na hatimaye hao waliopigwa kufunguliwa mashtaka ya kufanya fujo na Polisi? Haki ilikuwepo kweli?
Hawa si Watu wa Mungu hawa?
Mara kadhaa kwenye hotuba za Salat Jumaa, Masheikh wanatuhubiria Waislam kuyakemea maovu tunapoyaona. Sisi Waumini tunakemea, wao walimu wetu wanapaswa kuwa mstari wa mbele. Mbona hawakemei?
Leo, misamaha ya kodi imeondolewa, ndio wanakaa kimya? Mbona Waziri Nagu (kabla ya muswada huu kwenda Bungeni) alitangaza kusudio la Serikali kufuta misamaha ya kodi kwenye taasisi za kidini na NGO? Ina maana hawakuliona? Au walidhania serikali inafanya dhihaka?
Well, hii si dhihaka, hii ni sabotage kwa Watanzania. Sasa nadhani mnaelewa wapi CCM inaelekea. Mkiichagua tena 2010, litakalotokea shauri yenu. Mimi simo!
./Mwana wa Haki
Mbowe: Nataka kugombea Moshi Vijijini, tumwondoe Kimaro.
Hizo hospitali na shule ndiyo wanatakiwa walipe haswa. shule nyingi zinazomilikiwa na taasisi za kidini karo zao ni za juu sana,Mahospitali vile vile ada zao za juu,vyuo vile vile kwa ujumla wanajiendesha kibiashara na bado hata ukitaka nafasi kwenye hizo shule pamoja na ada na vigezo vingine kutimiza bado lazima umjue fulani.Kwa mfano kwenye mahospitali madaktari na watumishi wengine wanapelekwa huko kufanya kazi na serikali na kulipwa na serikali lkn bado mashirika yanawatoza wagonjwa bei mbaya kwa kutoa huduma.Jamani hizo huduma zamani ndiyo ilikuwa nafuu na si sasa.Haya mashirika huduma zao zote kwa jamii kwasasa ni ghali.Ninachoitaka hii serikali isiishie kwa mashirika ya dini vipi kwa wanaochukua mrahaba bila ya kulipa kodi au kulipa kiduchu?Na huko nako kwanini wasiende!Mkulo na nenda kwa hao wakezaji mufilisi pia.I have been always in support of KULIPA KODI...... however......
Tujiulize in the first place kwanini hizi taasisi za kidini zilipewa misamaha ya kodi...what was the rationale............
na sasa serikali kuondoa kodi what is the rationale..............
Hizi taasisi za kidini inatakiwa ziwe audited/assessed na iangaliwe ni shughuli zipi wazifanyazo zilipiwe kodi na zipi zisamehewe.....mfano zile shughuli ambazo ni huduma kwa jamii hospitali and the like.....serikali should think again....zile za kibiashara mfano radio stations and the like....zilipe kodi
Serikali itoe muongozo kwenye hilo ili kusitokee kutokuelewa............
Serikali pia lazima ikumbuke kuwa si kila biashara ifanyazo hizo taasisi ni kwa ajili ya manufaa kibiashara............inawezekana kabisa kuwa charge wanazotoza ni ili kugharamia shughuli za uendeshaji wa hizo shughuli.........na ndio maana hapo mwanzi nimesema hizo taasisi ziwe audited kujua what is what
Mwanaharakati kwanza naomba ufute usemi wako kwamba mashehe na mapadri ni wanafiki.
Hiyo siyo lugha nzuri kwa viongozi wetu wa kidini lakini naomba pia nikupe pole kwa kukipenda chama chenye mwelekeo wa kikabila. Pole sana maana chadema hawana sera zaidi ya kutangaza ukabila lakini kama wewe ni mchaga nakutakia kila la kheri
"Kuna watu wamekuwa mamilionea kwa kutolipa kodi kupitia mgongo wa dini…kwa kweli hawa wanaopata hii misamaha wanaitumia vibaya, kwani wanasingizia dini wakati wanaenda kufanya biashara," alisema Mkulo.
Waziri huyo alitoa mfano wa moja ya madhehebu lililoagiza mabati 4,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa likatumia mabati 200 tu na mengine mmoja wa viongozi wa kanisa hilo akaenda kuyauza kwa bei ya soko. Pia alitoa mfano wa madhehebu ya dini ambayo yaliagiza tani 5,000 za sukari kutoka Malawi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima, lakini tani tano tu zilienda Singida kwenye kituo hicho na tani zingine zilizobaki zilikwenda Makambako na kufungwa kwenye mifuko na kuwauzia wananchi.
Katika kuelezea namna baadhi ya watu wanavyonufaika na misaada hiyo, alitoa mfano wa kiongozi mmoja wa kidini aliyeagiza magari kwa ajili ya kanisa lakini akayatumia magari hayo kwa kuanzisha kampuni ya kitalii (tour operator) kwa ajili ya kukodisha kibiashara. Alitoa mfano wa taasisi zisizokuwa za kiserikali (NGOs) kuwa kuna zinazotumiwa na wafanyabiashara kuagiza vifaa mbalimbali sio kwa ajili ya matumizi ya kijamii bali kibiashara.
"Hawa wanatumiwa na wafanyabiashara licha ya kuwa zipo chache zinafanya kazi vizuri." Hata hivyo, Mkulo alisema jopo hilo la kitaalamu ambalo limefanya uamuzi huo limeona kuwa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani uendelee kutolewa kwa kwa vifaa vya elimu, huduma za afya na vifaa vya hospitali ambavyo vitaagizwa na taasisi za kidini.
Ila alisisitiza kuwa vifaa vitakavyoingizwa na taasisi za kidini kwa lengo la biashara ni lazima zilipewe ushuru na akatoa mfano taasisi ya St Gasper inayoendesha hoteli na zingine zinazofanya biashara hiyo iwapo zitaagiza vifaa vya hoteli ni lazima zilipie kodi. Alisema serikali haiwezi kukubali kuendelea kupoteza kiasi kikubwa cha fedha kwa kutoa msamaha kwa vifaa ambavyo sio vya kiroho au ibada ila wanataka kuhakikisha vifaa vya biashara vinatozwa kodi vyote."
Siku hizi dini imekua biashara na kuna baadhi ya watu wamekua waki tumia huu msamaha wa kodi kuji nufaisha. Kuna "viongozi" wengi tu wa dini wana tumia makanisa yao kama biashara sasa kama wana jiendesha kibiashara kwa nini wasi tozwe kodi? After all makanisa/misikiti mingi ina tegemea sadaka za wananchi kwa hiyo hawawezi kulalamika wakati jasho za pesa zao tunazi tolea sisi tunao wachangia.