Kugoma kutoa sadaka hakusaidii, just stop kwenda uone watakvyo rudi chiniDawa ni kugoma kutoa sadaka... tumechangishwa kitopeni wee kumbe wana option B ambayo jamaa kapewa ma millioni, sasa waje tena hatutoi na kama mbiguni wanaenda kwa style hii basi tusiende.
Askofu umetukosea sana tena sana.
Wachumgaji maskini hawana sauti wao ni kama sisi tu ukisema kinyume na Askofu mkuu unaitwa kitimoto na ukizubaa ùnatengwa kabisa na kanisa.
HakikaAibu kwa muumba wao zaidi. Najua leo Mungu atakuwa amekasirika sana. Wanastahili kutubu
Wachache wanaojielewa, wengi machawa, Hawa kina shoo.Kweli kabisa. Alafu KKKT wengi wanajielewa sana hawana mambo ya kipuuzi
Kwakweli mimi ni KKKT ila kitendo cha jana kimenikatisha tamaa sana ukizingatia sharika mbalimbali zilifanya harambee kwa lengo la kufikisha kiasi fulani cha fedha za hicho kituo na sharika nyingi zilifikia na kuvuka malengo. Sasa nikawaza imekuwaje kwenye kilele cha harambee wahangaike kiasi cha kumuita mtu katili na makatili wenzake kuja kuchangia.Katika Biblia takatifu tunafundishwa kuchukia na kukemea dhambi zote. Kuanzia Wizi, Uzinzi, Kuua, Kuonea watu, zinaa pamoja na matendo maovu yakiwemo ya ubakaji na ulawiti.
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na matukio ya wakosoaji wa Serikali kutekwa, Kuuwawa, Kubakwa na kulawitiwa( Udhalilishaji wa kingono). Matukio haya yamethibitishwa na watu mbalimbali waliofanyiwa vitendo hivyo wakiwemo wanaharakati wa Kenya na Uganda Boniface Mwangi na Agather Atuhaire.
Nyie mmesoma theolojia miaka zaidi ya 3. Nyie mnasoma Biblia na kufundisha matendo mema kila siku.
Ingekuwa ni mkutano wa CCM tungeelewa ila kwa sababu ni nyie lazima tuwaulize. Imekuwaje mnampigia makofi mtu anayehusishwa na Watanzania kutekwa, kuuwawa na kufanyiwa ukatili wa Kingono ikiwemo sodomy?