Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
Sijui kama ni mimi tu, hivi kuna tatizo gani kila mhubiri anayehubiri upendo TV, awe Mchaga, Mhaya, Mndengereko, Msukuma au mnyakusa nakadhalika, anaiga sauti ya Mwakasege? au ndio wanaamini kuhubiri ni kutumia sauti ya Mwakasege?
Yule mwenzenu ile sauti ni ya kinyakyusa, pamoja na kuishi Arusha kwa miaka mingi lafudhi ya kinyakyusa haijamwondoka, wanaiga kuongea, kutembea, kuimba, gestures, kutunisha kifua, kupandisha mabega kila kitu.
Hivi kama mnamhubiri Mungu kweli kwenye mahubiri yenu, Mungu hawezi kuwapatia sauti ya kwenu? na wakitoka pale madhabahuni wanaongea lafudhi zilezile tu, au mnahubiri kimwili kwa kuiga vile mtu mwingine anavyofanya?