Wachungaji Wanaodai Miujiza ya Uponyaji wakatoe huduma kwa wagonjwa mahospitalini.

Wachungaji Wanaodai Miujiza ya Uponyaji wakatoe huduma kwa wagonjwa mahospitalini.

Aiseeh Umezungumza Kitu kikubwa sana kwenye Imani ambayo wengi hawaijui! Hapa nina Ushuhuda!

Pia ukikumbuka wana wa israel walipofika bahari ya Shamu wakakosa njia yoyoye ile na kukata tamaa kwamba wanakuja kuuawa.Ndipo Mungu akamuuliza Musa una nini Mkononi mwako,? akajibu nina Fimbo ndipo akambiwa apige maji, ndipo bahari ya shamu ikagawanyika. Mungu anafanya Muujiza at the Point of No return.

Ushuhuda wangu! 2023 Nilikua mambo yangu yalikua yamevurugika kabisa nikawa nadaiwa kodi ya Miezi 6! jaribu huko kwa ndugu, jamaa na marafiki wate walinikimbia fanya kila namna hakuna chochote!

Hapo nikiwa nina sali sana na ndio option niliokua nayo hiyo Kupiga Goti na kumlilia Mungu tu,! Kwamba katika maisha yangu Mungu hajawahi kuniacha nikaaibika hata siku moja! Hapo mwenye nyumba nimemuahidi Jumapili ndio nitampa hiyo hela kwa IMANI na sijui nitapata wapi (1,020,000) Ila MOYONI nina amani na Imani kuwa Nitapata ! Aiseeh Jumapili nikaenda kanisa moja la kinabii hapa DSM na ndo ilikua mara yangu ya kwanza na kabla ya kwenda Mungu alinipa Ndoto mbili juu ya kanisa lile kuwa ni kanisa la Kweli, Kabla sijaenda Mungu alitengeneza CONNECTION kwenye Ulimwengu wa Roho! Aiseeh sitakuja kusahau hiyo siku Nabii aliniona na akanitumia hiyo 1,020,000 na nikapata utabiri mkubwa sana kwenye maisha yangu ambao upo mbioni kutimia
. Nika praise kwa Mungu na nikampa sifa na Utukufu Mungu aliye mbinguni!
Watu wakabaki wanashangaa pale hii imewezekanaje! Kumbe walishindwa kujua majira yake yalikua yametimia.!

Watumishi wa Kweli wa Mungu Wapo kabisa!

NB; Mambo ya Kiimani huyo mtoa Uzi asije kudhani ni rahisi rahisi hivo hasa kwa mambo ya Upande wa NURUNI maana Mungu ili ajifunue kwako lazima akupitishe kwenye HEKIMA zake ili akujenge vizuri kwa kupokea Baraka Zake.

Ninaweka picha na Muamala hapa

View attachment 3204958
Kwahi 2023 ni yesterday hahahaha 🤣🤣🤣🤣 danganya wajinga
 
Wakina Mama zetu wanapigwa pesa hatari! Juzi kati nimekutana na mzozo mmoja, yaani Mzee amesafiri kaenda Kikazi halafu bi mkubwa kapeleka pesa ya matumizi yote kwa Mwamposa. Watoto walikuwa wanapiga pass ndefu.
Shuhuda za wengi waliokaa kimya unaambiwa ni kuanzia 3m na kuendelea
 
Kwahi 2023 ni yesterday hahahaha 🤣🤣🤣🤣 danganya wajinga
Nilijua watu kama nyinyi mtakuwepo!! Mzee hiyo ni Screenshot ilivotumwa siku hiyo kesho kesho yake nika screenshot na nikahifadhi kama kumbukumbu kwa huo muujiza maana siku nitakwenda kutoa kama shukrani zaidi ya hiyo ili siku ziwasaidie wengine!! watu wanapitia changamoto mkuu! Mungu Yupo.

hiyo ni screenshot ya siku hiyo nikaipiga kesho yake.. Sio ya leo wala jana!
Unavoona Yesterday sio ya jana hiyo Mzee!

NB: Na utu uzima wangu huu nidanganye ili ije inisaidie nini? Au nitafaidika na nini nikidanganya.? Try to Think Beyond that....
 
Hospitali ni taasisi ya umma,ambayo mtu mwenye imani yeyote na hata asiye amini anaenda pale kutibiwa, hawa watenda miujiza wana taasisi zao za dini wabaki hukohuko makanisani wasiingilie taasisi za umma. Au mkitaka hivyo anzisheni hospitali za makanisa wawe wanaenda huko. Over
 
Ni possible miujiza kutoka ila Huwa haitokeaji mara kwa mara kama mwamposa anavyodai,miujiza hutokea ila ni mara nyingi huwapata watu wapya kwenye Imani,ila ukiokoka unaweza kukaa muda mrefu bila kuona miujiza lakini hyo haimaanishi kuwa Mungu hawezi kutenda miujiza
 
Nakumbuka nilienda kwenye tamasha moja la Kapola, ambapo alijaribu kujibu hili swali.

Alisema ni wajibu wa kila aaminiye kutumia nguvu aliyopewa na Mungu kuponya watu. Kwahiyo mnavyowasema wachungaji, mjiulize mbona nyie hamfanyi hivyo?

Sasa nikajiuliza amejibu swali au amerusha mpira tu.

Hawa majamaa ni matapeli ila ndo hivyo sio kila mtu anaelewa.
 
Nakumbuka nilienda kwenye tamasha moja la Kapola, ambapo alijaribu kujibu hili swali.

Alisema ni wajibu wa kila aaminiye kutumia nguvu aliyopewa na Mungu kuponya watu. Kwahiyo mnavyowasema wachungaji, mjiulize mbona nyie hamfanyi hivyo?

Sasa nikajiuliza amejibu swali au amerusha mpira tu.

Hawa majamaa ni matapeli ila ndo hivyo sio kila mtu anaelewa.
Hapo alirudha swali hewani
 
Back
Top Bottom