Wachungaji Wanaodai Miujiza ya Uponyaji wakatoe huduma kwa wagonjwa mahospitalini.

Wachungaji Wanaodai Miujiza ya Uponyaji wakatoe huduma kwa wagonjwa mahospitalini.

Katika misingi ya Kibiblia; ili muujiza wa kweli uweze kutokea unahitaji vitu viwili:

1. Imani ya mtendewa muujiza

Yesu mwenyewe hakuponya kila mtu; na alikuwa haponyi watu kihololela tu. Ndiyo maana mara nyingi alipomponya mtu alisikika akisema "Imani yako imekuponya". Ni wazi kwamba kuwa na imani thabiti ndiyo msingi-mama wa muujiza wo wote wa kweli kutokea.

Na dhana hii haishii katika mambo ya kiroho pekee bali ni kanuni ya jumla katika maisha kimalimwengu. Ukiamini kabisa kabisa kuwa utafanikiwa maishani ni kweli utafanikiwa. Ukijiaminisha kuwa utakuja kupata mke mwema ni kweli utampata. Ukijinenea mema na kujibariki mwenyewe kwa imani kabisa kabisa ni kweli itakuwa hivyo.

2. Hali ya kukata tamaa kabisa (Desperation).

Iko hivi:
Mungu huwa hapendi ku-share utukufu wake na kiumbe cho chote kile. Ndiyo maana huwa Anasubiri mpaka umefika mwisho wa reli kabisa na matumaini yamepotea. Wakati ule umefanya kila kitu ambacho kinawezekana kufanywa na mwanadamu, hapo ndipo utukufu wa Mungu hupenda kujichanuza. Wakati madaktari bingwa wameshakupa miezi mitatu ya kuishi kwa sababu kansa yako imeshaenea mwili mzima na hawawezi kufanya operesheni wala chemo, basi hayo ndiyo mazingira sahihi ya kupata muujiza wa kweli wa Mungu. Wakati ambapo umekata tamaa kabisa kabisa kama yule mwanamke aliyekuwa na tatizo la kuvuja damu kwa miaka 12 mpaka akaamua kujiripua tu na kwenda angalau kugusa pindo la vazi la Yesu huku ikiwa ni kinyume na sheria za torati maana mwanamke aliyekuwa anatoka damu alikuwa najisi na hakutakiwa kuchangamana na watu; then you are primed for God's miracle.

Siku hizi ni kweli kuna ubabaishaji mwingi kuhusu miujiza na mara nyingi kinachofanyika ni mazingaombwe tu na alkadabra za kishirikina na kisaikolojia; lakini miujiza ya kweli bado ipo, na inafanywa na watumishi wa kweli wachache waliobaki.

Kwa hiyo unaposema eti watumishi waende mahospitalini wakaponye watu huko, ni wazi kwamba huelewi misingi ya Kibiblia kuhusu miujiza.

Na ukimuona Gwajima kazuka kanisani kwake na maiti anapambana eti aifufue ili kuonyesha nguvu zake za kiroho; na upako aliona, jua kuwa hayo ni mazingaombwe tu unafanyiwa ili upigwe.

Tena Yesu Aliponya watu wanaofahamika na watu. Ndiyo maana aliaminika mapema. Mtu kazaliwa kipofu hapo kijijini mnamuona miaka na miaka na leo amekutana na Yesu kapona. It must be a miracle! Hivyo ukiona mhubiri kaja mjini kwenu halafu viwete wanaotupa magongo yao na kuanza kutembea wote ni wageni basi anza kutilia shaka uponyaji huo.....
Huyo sio mungu mwenye upendo,

That is a sadistic god.
 
Jibu lako ni rahis tu hakuna kinachofanikiwa kwenye mambo bila imani mpaka anaeombewa awe na imani sasa huwezi kwenda tu lazima wenye iman na wewe wakufuate ndio maana leo ofisin kwako akija muuza mchicha utamfukuza akiwa getin kabla hajakufikia lakin mke wako akiitaji mchicha ule ule ataufuata gengeni au akigongewa mlango atatoa ushirikiano na kusisitiza na kesho aletetwe tena so mgonjwa anaitaj kupona ila iman yake hapa kuhusu yesu anaona upuuz so hawez kupona
yaani ili mungu anayekupenda akuponye anahitaji umuamini?

hivi msaada unatolewa kwa masharti kweli?

hebu tukae chini tutafakari kidogo

ukimuamini unamuongezea nini yeye muweza wa yote aliye kamilika?

acheni utani basi
 
Back
Top Bottom