Wachungaji Wanaodai Miujiza ya Uponyaji wakatoe huduma kwa wagonjwa mahospitalini.

Kwahi 2023 ni yesterday hahahaha 🤣🤣🤣🤣 danganya wajinga
 
Wakina Mama zetu wanapigwa pesa hatari! Juzi kati nimekutana na mzozo mmoja, yaani Mzee amesafiri kaenda Kikazi halafu bi mkubwa kapeleka pesa ya matumizi yote kwa Mwamposa. Watoto walikuwa wanapiga pass ndefu.
Shuhuda za wengi waliokaa kimya unaambiwa ni kuanzia 3m na kuendelea
 
Kwahi 2023 ni yesterday hahahaha 🤣🤣🤣🤣 danganya wajinga
Nilijua watu kama nyinyi mtakuwepo!! Mzee hiyo ni Screenshot ilivotumwa siku hiyo kesho kesho yake nika screenshot na nikahifadhi kama kumbukumbu kwa huo muujiza maana siku nitakwenda kutoa kama shukrani zaidi ya hiyo ili siku ziwasaidie wengine!! watu wanapitia changamoto mkuu! Mungu Yupo.

hiyo ni screenshot ya siku hiyo nikaipiga kesho yake.. Sio ya leo wala jana!
Unavoona Yesterday sio ya jana hiyo Mzee!

NB: Na utu uzima wangu huu nidanganye ili ije inisaidie nini? Au nitafaidika na nini nikidanganya.? Try to Think Beyond that....
 
Hospitali ni taasisi ya umma,ambayo mtu mwenye imani yeyote na hata asiye amini anaenda pale kutibiwa, hawa watenda miujiza wana taasisi zao za dini wabaki hukohuko makanisani wasiingilie taasisi za umma. Au mkitaka hivyo anzisheni hospitali za makanisa wawe wanaenda huko. Over
 
Ni possible miujiza kutoka ila Huwa haitokeaji mara kwa mara kama mwamposa anavyodai,miujiza hutokea ila ni mara nyingi huwapata watu wapya kwenye Imani,ila ukiokoka unaweza kukaa muda mrefu bila kuona miujiza lakini hyo haimaanishi kuwa Mungu hawezi kutenda miujiza
 
Nakumbuka nilienda kwenye tamasha moja la Kapola, ambapo alijaribu kujibu hili swali.

Alisema ni wajibu wa kila aaminiye kutumia nguvu aliyopewa na Mungu kuponya watu. Kwahiyo mnavyowasema wachungaji, mjiulize mbona nyie hamfanyi hivyo?

Sasa nikajiuliza amejibu swali au amerusha mpira tu.

Hawa majamaa ni matapeli ila ndo hivyo sio kila mtu anaelewa.
 
Hapo alirudha swali hewani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…