Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,548
- 28,817
Uholanzi walikuwa na kampuni ya inayoitwa Nexperia ya kutengeneza semiconductors ambayo ilikuwa inaelekea kufirisika.
Wakaja wawekezaji wa Kichina kampuni ya Wingtech Technology Co wakainunua Nexperia. Hivyo Nexperia ikawa ni kampuni tanzu ambayo inamilikiwa kihalali na Wingtech ya China.
Na kuanzia hapo ikawa inafanya vizuri sana kwenye utengenezaji wa semiconductors.
Takwimu za karibuni zinaonyesha Nexperia produces over 100 billion components kwa mwaka.
Karibu sehemu kubwa ya viwanda vya magari na viwanda vya vifaa vya umeme barani Ulaya na duniani vinaitegemea Nexperia kama supplier wao wa semiconductors.
Wakati wa hili vuguvugu la vita vya kiuchumi Marekani ikaishawishi Uholanzi ifanye namna kuikwamisha kampuni ya Wingtech ya China inayomiliki Nexperia.
Kama kawaida kibaraka akamtii bwana mkubwa wake. Serikali ya Uholanzi ikaipokonya Wingtech umiliki wa Nexperia. Wakaubadilisha uongozi wakamtoa CEO Mchina wakamweka Mholanzi wakidai kuwa hilo badiliko ni temporary.
Mchina alichowaweza Wadachi mapema tu baada ya kuinunua Nexperia, wakahakikisha zaidi ya 80% ya uzalishaji unafanyika China huku majengo ya HQ yakibakia Uholanzi na sehemu ndogo ya uzalishaji ukifanyika Ujerumani, Uingereza, n.k.
Walichofanya Nexperia China (Wingtech) ambako ndiko kuna uzalishaji mkubwa wa semiconductors na vifaa vya kutengenezea semiconductors wakazuia exportation kwenda Ulaya.
Hii inamaanisha hata viwanda vya Nexperia vilivyopo Uingereza na Ujerumani haviwezi kuoperate bila kuimport key components kutoka China.
Mdachi kajifunga own goal, kapoteza credibility kimataifa kama nchi safe kwa wawekezaji, wengine kazi zimesimama, serikali inapoteza mapato na huku viwanda vya magari barani Ulaya na duniani vikianza kupitia wakati mgumu kutokana na kuanza kuadimika kwa semiconductors.
Imebidi Waziri wa Biashara wa Uholanzi amwendee hewani wa China kutafuta suluhu ya mzozo huo.
Mchina jibu lake moja tu aliiambia Uholanzi izingatie mkataba na utawala wa sheria.
Kuwa vibaraka wa Marekani kuna wagharimu sana bara la Ulaya, wakijitoa kwenye kuinyenyekea Marekani huenda wakarudia their past glory.
Hili sakata likanikumbusha kampuni ya Kidachi ya enzi za karne ya 17 na 18 iliyoitwa Dutch East India Company.
Ilihusika katika kupora utajiri na mali sehemu mbalimbali duniani (plundering and looting) ili kulitajirisha taifa lao. Ni miaka mingi imepita kumbe hii kitu ya uporaji bado iko kwenye damu.
CREDIT: https://www.cnn.com/2025/10/19/business/nexperia-us-china-car-prices