Vigezo ni swala la kibinafsi zaidi.....kama Juma anavyomchagua Asha kua mke wake badala ya Ashura anakua ametumia vigezo anavyovijua yeye na ndio maana Amani atakuja kumuoa Ashura japo Juma hakuona anamfaa yeye.
Na kuridhishana kama ilivyo kwa wanaotafuta wachumba ni kwamba mtu anakua anajua wewe ni mtu wa aina gani,,,unapenda na unataka nini...hata kama kutakua na viwili au vitatu mnavyotofautiana bado wanaweza kuamua kua pamoja....hiyo ina maana kwamba kila mmoja ameamua kuridhika na mwenzake.
Juzi kuna mtu alianzisha thread kwamba anataka kutafuta nyumba ndogo kwasababu mke wake amekataa kuperfom oral sex.....mume haridhishwi na hiyo hali kwasababu alishazoea kabla ya kukutana na mwenzake na hakujua kwamba hilo litakua tatizo.Kama angejua kabla na bado akaamua kua nae hivyo hivyo asingekua na mawazo ya ''kutafuta nyumba ndogo'' kwasababu alijua hatapata na akaamua kukubaliana na hali halisi mapema...hapo asipobadili mawazo ndoa yao inaweza kuvunjika iwapo mkewe atagundua kwamba mumewe anatoka nje ya ndoa.
Mke nae haridhishwi na hali ya mumewe kutaka afanye kitu ambacho yeye hataki/hawezi......hivyo kadri atakavyomlazimisha ndivyo watakavyoongeza migogoro na kununa ndani ya nyumba kwasababu kila mmoja anaona kwamba hatendewi haki na mwenzake.
Swala kusema mtu atazunguka na wangapi ili apate wa kumridhisha ni relative....rejea kwenye maelezo ya juu.Lengo kuu ni kumjua ili umkubali na kuridhika na mwenzako alivyo kabla ya kuingia kwenye commitment ambazo ni ngumu kujitoa...
Sasa kuliko kuingia kwenye ndoa alafu uwe unatafuta chochote kile nje ya ndoa kwasababu hupati ndani ni ulimbukeni....soma...tambua...kubali...RIDHIKA.