Wadada wa kazi na kupasua vyombo

Kumbukeni Kuna bahati mbaya na makusudi cyo mnaona karibu tu muone na mbili pia!
 
Achana na house girl bana, wa nini kwanza? Vyombo tafuta dish washer, kufua tafuta kitu cha sympson 7kg autowash & drier, kupika iwe ni quick food like noodles au pasta; vacuum cleaner tafta auto robot unaiprogram kuosha floor mwezi mzima
ahhaaaaa umetisha baba
 
Kupasua vyombo huo upepo karibia wanawake wote wanao,sio mahousegirl tu.Ni kuomba Mungu hilo lijini mufilisi lisikupitie maana utapasua hadi tv ukishamaliza kupasua screen za simu.
ahaaaa mbona mimi sipasuagi?
 
Ni kumuelekeza na kumvumilia tu, unaweza kumfukuza ukapata ambaye ni bomu zaidai,na wanaweza kukuchana mdomo kwa kuongea tehe tehe tehe
 
Wamezoea kutumia/kuosha vyombo vya plastic na sahani za mifupa sasa unawaachia glass na sahani za udongo ukiweka tu sabuni uoshe zinateleza kinoma
 
Wape maelekezo ya kutosha... Toka day1. Wangu alinivunjia glass karibu zote, ila baada ya semina elekezi... Hajavunja tena
 
Ni kumuelekeza na kumvumilia tu, unaweza kumfukuza ukapata ambaye ni bomu zaidai,na wanaweza kukuchana mdomo kwa kuongea tehe tehe tehe
ahaaaaa me kuongea mvivu sanaaana .wana visa sana acha tu basi tu maisha
 
Semeni nyie me kwangu kuamka asubuhi na glass moja ya kunywa maji / juice ndio kawaida nimeshasema nimechoka iliyobaki nanunua tu glass kama chumvi.
Nimeleta za plastic zinaachwa nimeleta cha chuma zimeachwa yuko na za vioo tu anavunja kama sehemu ya maisha yake [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Naona huu ni ugonjwa wa kila nyumba kiukweli toka nakua sina mkono wa kuvunja vyombo....ila msichana niliempata safari hii ananinyoosha yaan mpaka namuuliza unavunja makusudi?

Wifi angu msichana akivunja chochote anamkata wanaenda kununua wote ila mimi siwezi nawaza angekua mwanangu angevunja ningemlipisha?

Nilichokifanya ninanunua glass ninaziacha kwenye maboksi sijazitoa
 
Tatizo ushamruhusu baba anapakua tu, basi beki tatu muda wote ana stress kwamba utamkaripia ndiyo maana anakuwa anatembea kama ana funza anaangusha vyombo na kupasua.

Kama umemruhusu baba kupasua, mwambie beki tatu asiwe na hofu afanye kazi bila stress.

On the real though, kuna direct relationship kati ya mtu kufanya makosa makosa mara nyingi kazini na stress levels.

Kuna mambo mengine hapo kwako unayaona ya kawaida tu, lakini mfanyakazi aliyetoka mbali anaona mtihani inakuwa stress kwake mpaka anavunja vyombo.

Kuna wadada wengine kuangaliwa tu wakati kabeba kitu tayari ni sababu ya kuweza kumfanya aangushe alichobeba.
 
Mkuu hawa wadada wa kazi kwenye vyombo kweli kabisa unachokinena, but hakuna jinsi ni sehemu tu ya maisha, akivunja vyombo we nunua vyengine la kama unaona kuna vyombo ni vya bei mbaya na unahofu atakuvunjia wakati wa kuosha basi kuwa unaviosha mwenyewe, mi mdada wangu wa kazi sometime nikiwa na hofu hiwa namwambia ye akacheki Tv vyombo vyangu mi naosha mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…