Wadada wa mitandaoni punguzeni hizi janjajanja zenu

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,424
Wadau,

Haya ni mawazo yangu na sitaki kulazimisha mtu kukubaliana au kupingana nayo. Asilimia kubwa ya wadada wa mitandaoni ni waongowaongo na wajanjawajanja sana.

Anaweza kukwambia yupo ubungo kumbe yupo kinyerezi, anaweka picha yake ikijionesha ni mdada wa kiuno cha nyigu kumbe mwenyewe halisi ni bonge wa tele kwa tele juu chini, anaweza kukwambia umtumie hela ya mafuta ili aje na gari yake kumbe hata toothpick hana.

Anaweza kukwambia anamiliki mashamba ya machungwa na matikiti kwao kumbe hata Msamvu stend hajui panafananaje.

Anaweza kukwambia hana mtoto kumbe anao tena si mmoja ni watano.

Anaweza kukwambia yupo wilaya ya jirani umtumie nauli aje, unatuma nauli ndani ya dk sifuri mwenzio huyo anachomoza toka hapo mtaa wa pili.

Anaweza kukwambia umtumie vocha akupigie, ukituma imekula kwako anapigia watu wengine ikiisha anabip.

Nyie wadada wa mitandao msifanye hivyo mumwogope Mungu kwani anawaona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mkuu ukisikia mtandaoni au online unaelewa nini?
 
mkuu mtu kuwa nyuma ya keyboard huwezi kumjua vizuri kufake ni kawaida kabisa
 
Pole Sana Wewe Humu Mgeni Na Id Unazozitongoza Nazo Ngeni Hivyo Wote Mmekutana Wageni Mpaka Mnajiita Makapuku Forums Acha Sie Old Member Wa Jf Tutongozane Wenyewe Maana Tunajuana Vyema Haswaa
 
Ndio Maana hata wewe umewaita Wadada wa Mtandao... Mtandao ni Mfumo unaoweza kukurahisishia kitu bila hata kutumia nguvu nyingi bali vile wewe utakavyouelekeza..

Sasa na wao kwa kuwa Wanaitwa wadada wa Mtandaoni wameshapoteza ule uhalisia wao wa kibinadamu hivyo wameshajiweka kimtandao mtandao tuuu.. Kwa hiyo Kijana we endela kuwahudumia usichoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…