Wadada wa siku hizi sielewi wanawezaje kuendesha biashara zao ndogo kwenye fremu za gharama kubwa

Wadada wa siku hizi sielewi wanawezaje kuendesha biashara zao ndogo kwenye fremu za gharama kubwa

Kila mtu ana mtindo wake wa namna ya kufanya maisha yake yaende kilingana na matakwa na vionjo vyake, mazingira yanaweza kuwa sawa ila kila mmoja wetu amejaliwa namna yake ya kuendesha maisha yake kulingana na mazingira yake.
Mwisho wa yote anapata riziki yeye na wanaomtegemea .

Wabarikiwe sana wadada wapambanaji haidhuru aina ya wanachofanya jamii itawaonaje maadamu tu hawachukui cha mtu bila ridhaa.
 
Umenikumbusha mzee mmoja alikuwa na taxi....muda wote kapaki kwenye kijiwe cha gahwa...anaifutafuta gari yake...mtu akitaka kukodi hasa vijana anakataa.....kumbe alfajiri ameshapiga dili zake za kusambaza chang'aa...hivyo basi kwa hao wa maduka...si ajabu ngada.
 
Unakuta,

Mdada kakodi fremu kodi 1m, kaweka vigauni na madela, ukipiga hesabu yake vigauni kama 7, na Madela 15 jumla haifiki mtaji wa 1M anashinda hapo kila siku.

Mashoga zake wanamtembelea hapo ni mwendo wa kuagiza misosi na vinywaji ki pub cha jiran, nje kapaki IST yake safi kabisa, jioni huyo anaenda kwake, unakuta biashara ngumu lakini anakomaa hivyo hivyo, kuna nini nyuma ya pazia? Au ndo masponsa?

Unakuta mdada kakodi fremu kaweka vyupi pc kadhaa, bra pc kadhaa na pochi kama 10 tu kamaliza. Anashinda hapo biashara hamna na ukimuona mdada mwenyewe high class. Ama kweli dunia ina mambo!

Unakuta mdada kafungua saloon, anashinda ti huko na mashoga zake lakini hakuna kinachofanyika humo ndani na still life going on.

Hasa maeneo haya ya mijini unakuta mdada kafungua let's say bakery, hamna movement zozote lakn kila siku yumo, na kodi ikiisha italipwa ya mwaka. Kuna nini behind?

Kuna mahali nina kiofisi mjini mjini hivi, Jirani yangu ni mdada wa makamo 40's ni zile types za wadada ambao hawazeeki, full kupendeza, sunglasses n.k. Tuwaite mishangazi.

Ni jirani nikimaanisha fremu zetu zimefatana. Kachukua frem mbili kavunja kati ikawa moja kubwa, kaweka mini supermarket nzuri ya kisasa mzigo wa kutosha, kafunga Ac, milango aluminium, pana muonekano mzuri. Hana mfanyakazi anauza yeye mwenyewe, pia ana harrier hizi wanaziita matako ya nyani, hamna biashara kabisa. Kwa siku ameuza sana haizidi laki moja, nadhani watu wanapaogopa kulingana na muonekano wanahisi vitu ni bei Sana.

Mashoga zake wanakuja ni kujiagizia pombe tu na vyakula, akijisikia hata saa 8 mchana anafunga anaondoka, weekend anafunga muda wowote ule.

Mifano ni mingi iliyo hai, wanawake na hizi biashara ni kama geresha, au ni pakuzugia tu wana migodi yao wanayochimba pesa (mabwana ).
Masponsa
 
Back
Top Bottom