Wadau ambao hamuielewi michezo ya kubeti, tukutane hapa

Wadau ambao hamuielewi michezo ya kubeti, tukutane hapa

Nshomile wa Muleba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
2,166
Reaction score
5,620
Jambo Jambo?

Nakumbuka kipindi kile kama sikosie kampuni ambayo ilikuwa miongoni mwa makampuni ya awali ya michezo ya kubahatisha “Kubeti” ilikuwa ni M-BET, MERIDIAN na kadhalika.

Kama ilivyo mazoea kwa vijana kujaribujaribu vitu mbalimbali, vivyo hivyo kwenye kubeti kijana nikazama huko na mwanzoni nilikuwa nakula kula kiasi kwasababu pia nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira kuliko kawaida.

Ila badae akili ikanicheza na nkajikuta napoteza mvuto na michezo ya kubeti licha ya kufuatilia kabumbu barabara.

Wapo vijana ambao wameufanya mchezo huu kuwa kama “Addiction” na haipiti siku wala saa bila kubeti au kuandaa hiyo mikeka.

NAKUMBUKA NILIJIAMBIA;

HAKUNA PESA RAHISI, ZAIDI YA KUFANYA KAZI/BIASHARA KWA BIDII.
Hii ya leo mhindi sijui kanila, sijui mkeka umechanika, sijui chelsea kaniuaa
sikuiweza kwa kwakweli

Mbaya zaidi ni kampuni zimeongezeka sanaaa kuonyesha namna gani sisi vijana tunataka Easy money na pia kiwango cha Jobless kwetu.

(Sipingi suala la kubeti ila nimesema kwa mtazamo wangu kuwa nilishindwa kuielewa kabisaa na nkapoteza mvuto nao).

Nshomile
Kagera,Tanzania
 
Allah anasema katika qur an..
.يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

[ AL - MAIDA - 90 ]
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa...

Akili kichwani kwako.....
 
Ata sielewagi sijui odd ,ngapi sijui ma Nini ata sielewi na nafatiliaga sana soka
 
Huwa naona Kama mapichapicha hizi habari za kubet japo jamaa zangu wa karibu wanadai kupiga mpunga.
 
Nashangaa sana kuona mwanaume apigi nyeto wala kubet, hv mwanaume unaanzaje kuacha kufanya hayo mambo.
Anyway, leo tumpe ushindi wa magoli zaidi ya mbili kwa Man City.
 
Jambo Jambo?

Nakumbuka kipindi kile kama sikosie kampuni ambayo ilikuwa miongoni mwa makampuni ya awali ya michezo ya kubahatisha “Kubeti” ilikuwa ni M-BET, MERIDIAN na kadhalika.

Kama ilivyo mazoea kwa vijana kujaribujaribu vitu mbalimbali, vivyo hivyo kwenye kubeti kijana nikazama huko na mwanzoni nilikuwa nakula kula kiasi kwasababu pia nilikuwa mfuatiliaji mzuri wa mpira kuliko kawaida.

Ila badae akili ikanicheza na nkajikuta napoteza mvuto na michezo ya kubeti licha ya kufuatilia kabumbu barabara.

Wapo vijana ambao wameufanya mchezo huu kuwa kama “Addiction” na haipiti siku wala saa bila kubeti au kuandaa hiyo mikeka.

NAKUMBUKA NILIJIAMBIA;

HAKUNA PESA RAHISI, ZAIDI YA KUFANYA KAZI/BIASHARA KWA BIDII.

hii ya leo mhindi sijui kanila, sijui mkeka umechanika, sijui chelsea kaniuaa
sikuiweza kwa kwakweli

Mbaya zaidi ni kampuni zimeongezeka sanaaa kuonyesha namna gani sisi vijana tunataka Easy money na pia kiwango cha Jobless kwetu.

(Sipingi suala la kubeti ila nimesema kwa mtazamo wangu kuwa nilishindwa kuielewa kabisaa na nkapoteza mvuto nao)

Nshomile
Kagera,Tanzania
Mm sitaki kujua lolote juu ya haya mazingaombwe
 
Utasikia leo mpunga nje nje
Ukipata
Odd 2 ukiweka Laki unapata laki mbili hyo ni kwa wenye Pesa ndio wanaona utamu waBetting
Lakini wenzangu wa kuweka Jero upate Laki kila siku utakuwa unamtajilisha Kanji
 
wanabeti mpaka 100 au 200[emoji23][emoji23]

wapo ma nimekutana nao
 
Back
Top Bottom