Wadau hebu njooni tushauriane

Wadau hebu njooni tushauriane

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
8,323
Reaction score
18,051
Nimenunua simu hivi karibuni kutoka duka moja hapo kariakoo. Sim nimeitumia tokea mwezi wa kumi na moja tarehe 15 mwaka jana (2024). Mwaka huu mwezi wa kwanza kwenye tarehe kama 20 hivi simu ghafla ikazima nikiwa naitumia.

Na ilizima katika hali ya kawaida tu kama imejirestart ila hii haikujirestart ukiwasha inapiga vibration tu kama inastuka ikitaka kuwaka ila haiwaki.

Sijaifungua wala kuipeleka kwa fundi nimeirejesha dukani na walinipa kikadi cha warrant cha miezi 6.

Lakini naona wanajizungusha kunipa majibu kwamba tunafanyaje baada ya hapa. Simu wapo nayo na kijana ambaye yupo dukani anaonyesha ukaidi na kushindwa kunipa ushirikiano ninaotaka baada ya changamoto hii.

Alichosema nisubirie amfikishie boss wake yaani mwenye biashara hiyo issue then atanipa jibu. Tokea ijumaa ya wiki iliyoisha hadi leo jumatano tunazungushana nikiwapigia simu wanasema subiri washughulikie.

Nipeni ushauri nisije nikafanya maamuzi kwa kukurupuka nikaonekana sina hekima au nikakosea nikaonekana mzembe.

Nipeni ushauri.
 
jamani si tulishaonywa kuhusu simu za kariakoo?? Kwamba huwa ni refurbished phones?
Duka ni la kueleweka yaani kama vile unaovyoona zahoro matelephone. Ngoja nitapost hapa jina la duka ili na ninyi muwe na tahadhari msije kufanys biashara na hilo duka maana wanauza vitu vingi pale wanauza simu,laptops na baadhi vifaa kama speakers za Bluetooth.
 
Simu , aina ipi, vitu vyote unavyo , maana ya risiti na warrant yake,na simu haina damage ya nje nk.
Risiti ninayo ya kielectronic nililipia kwa simu. Warrant walinipa kadi. Simu ni Sony Xperia 1 Mark 4 haikuwa na damage yoyote na tokea kuichukua haijawahi kuonyesha dalili za changamoto but ghafla ikazima. Nimeichukua mwezi wa 11 tarehe 13 mwaka jana imekuja zingua mwezi wa kwanza katikati mwaka huu.
 
Back
Top Bottom