Wadau hebu njooni tushauriane

Wadau hebu njooni tushauriane

Ni heri ununue simu refurbished, kuliko used. Kwanza refurbished nyingi bei zake zipo juu na zinauzwa kama mpya, mtoa mada anazungumzia used.
Mzee refurbished ndio jina lingine la used. Refurbished ni imefunguliwa kufanyiwa inspections kubadilishiwa kama kuna parts zinazozingua then ikawekwa dukani.

Refurbished still ni used item. Hii hata kwa kuitazama ilikuwa ni mpya kabisa.
 
Nimenunua simu hivi karibuni kutoka duka moja hapo kariakoo. Sim nimeitumia tokea mwezi wa kumi na moja tarehe 15 mwaka jana (2024). Mwaka huu mwezi wa kwanza kwenye tarehe kama 20 hivi simu ghafla ikazima nikiwa naitumia.

Na ilizima katika hali ya kawaida tu kama imejirestart ila hii haikujirestart ukiwasha inapiga vibration tu kama inastuka ikitaka kuwaka ila haiwaki.

Sijaifungua wala kuipeleka kwa fundi nimeirejesha dukani na walinipa kikadi cha warrant cha miezi 6.

Lakini naona wanajizungusha kunipa majibu kwamba tunafanyaje baada ya hapa. Simu wapo nayo na kijana ambaye yupo dukani anaonyesha ukaidi na kushindwa kunipa ushirikiano ninaotaka baada ya changamoto hii.

Alichosema nisubirie amfikishie boss wake yaani mwenye biashara hiyo issue then atanipa jibu. Tokea ijumaa ya wiki iliyoisha hadi leo jumatano tunazungushana nikiwapigia simu wanasema subiri washughulikie.

Nipeni ushauri nisije nikafanya maamuzi kwa kukurupuka nikaonekana sina hekima au nikakosea nikaonekana mzembe.

Nipeni ushauri.
Mkuu, inaonekana ulipewa simu ya 'demo version' bila kujua. Sasa system imeamua kuwa trial period yako imeisha, wanakusubiri ujiunge na full version kwa gharama za ziada!

Lakini kwa hali ilivyo, usikubali kuzungushwa sana. Nenda dukani moja kwa moja, ongea na mwenye duka badala ya huyo kijana wa duka, na kama hawatoi suluhisho, wataje hadharani ili wengine wasije wakaingia mkenge kama wewe!
 
Hiyo siyo risiti.
Mzee lugha ndio shida au unaklemisha? 😂 Receipt inaweza kuwa ya kidigitali mfano ukinunua luku au unaponunua kifurishi zile sms za miamala huwa ni digital au electronic receipts mzee.

Usiklemu kuwa receipt lazima iwe kikaratasi.
 
Mzee refurbished ndio jina lingine la used. Refurbished ni imefunguliwa kufanyiwa inspections kubadilishiwa kama kuna parts zinazozingua then ikawekwa dukani.

Refurbished still ni used item. Hii hata kwa kuitazama ilikuwa ni mpya kabisa.
Used Phones: Previously owned, sold as-is without repairs or major modifications. May show signs of wear and have no warranty.

Refurbished Phones: Pre-owned but restored to like-new condition through repairs, testing, and quality checks. Often come with a warranty.
 
Nimeongea na mwenye duka ameahidi kwenda kuona tatizo ni nini kisha atanirejea kesho ndio nasikilizia hadi na yeye nione atanipa mrejesho gani nijue naanzia wapi kuwasha huu moto.
 
Used Phones: Previously owned, sold as-is without repairs or major modifications. May show signs of wear and have no warranty.

Refurbished Phones: Pre-owned but restored to like-new condition through repairs, testing, and quality checks. Often come with a warranty.
Sasa tumepishana wapi mzee mbona umepita mule mule ninapoongelea mimi. Nimesema ni used kwa maana simu ilishawahi milikiwa. Then nikasema ina warrant kutoka dukani kumaanisha ilishakuwa refurbished. Au nimekuchanganya wapi?
 
Mzee refurbished ndio jina lingine la used. Refurbished ni imefunguliwa kufanyiwa inspections kubadilishiwa kama kuna parts zinazozingua then ikawekwa dukani.

Refurbished still ni used item. Hii hata kwa kuitazama ilikuwa ni mpya kabisa.

Sasa tumepishana wapi mzee mbona umepita mule mule ninapoongelea mimi. Nimesema ni used kwa maana simu ilishawahi milikiwa. Then nikasema ina warrant kutoka dukani kumaanisha ilishakuwa refurbished. Au nimekuchanganya wapi?
Tumepishana hapa
"Mzee refurbished ndio jina lingine la used."
 
Mzee lugha ndio shida au unaklemisha? 😂 Receipt inaweza kuwa ya kidigitali mfano ukinunua luku au unaponunua kifurishi zile sms za miamala huwa ni digital au electronic receipts mzee.

Usiklemu kuwa receipt lazima iwe kikaratasi.
Endelea kuwa mjinga, na kukwepa kodi
 
Endelea kuwa mjinga, na kukwepa kodi
Mzee huwa unasoma zile risiti za malipo kwa njia ya mobile money au bank?😂😂😂 So Kodi gani huwa inakwepwa hapo?
 
Kipindi tigo wanauza Tecno h6 kwa promotion nilinunua ikazima hivyo hivyo...... Nikaenda tegeta kibo wakakaa na simu siku 5 naenda kuchukua wakasema Bado, nije baada ya siku Tano tena. Siku Tano zimepita wakaniambia njoo baada ya siku Tano tena. NILICHOWAFANYIA PALE KIBO COMPLEX TIGO HAWATAKAA WANISAHAU ... Walikuwa wahindi 2 kuniomba sana na simu nikapewa mpya ndani ya nusu saa. WATANZANIA HASA WANAWAKE CUSTOMER CARE NI HOVYO SANA. Bila ukorofi HUTOBOI.
 
Una ushahidi kama umerudisha simu?
Lini?
Ulimpa nani,tunafeli padogo kiasi
 
Waambie wakubadilishie nyingine, na ishu kama hizo mwenye duka atakuwa anaijua sema tu wanakusikilizia.

Ukienda tu huko police ni sawa ununue simu nyingine tatu.
 
Kipindi tigo wanauza Tecno h6 kwa promotion nilinunua ikazima hivyo hivyo...... Nikaenda tegeta kibo wakakaa na simu siku 5 naenda kuchukua wakasema Bado, nije baada ya siku Tano tena. Siku Tano zimepita wakaniambia njoo baada ya siku Tano tena. NILICHOWAFANYIA PALE KIBO COMPLEX TIGO HAWATAKAA WANISAHAU ... Walikuwa wahindi 2 kuniomba sana na simu nikapewa mpya ndani ya nusu saa. WATANZANIA HASA WANAWAKE CUSTOMER CARE NI HOVYO SANA. Bila ukorofi HUTOBOI.
Hawa naona wananichukulia poa sababu nawaonyesha uungwana. Ila nitakwenda kuwawashia moto hawataamini.
 
Una ushahidi kama umerudisha simu?
Lini?
Ulimpa nani,tunafeli padogo kiasi
Hapo sasa kama wanalengo la kunitapeli ndio watakuwa wamejikaanga vema maana dhamira yao itaonekana wazi kuwa walikuwa na lengo la kutapeli. Pesa ya mtu haipotei bure.
 
Mzee huwa unasoma zile risiti za malipo kwa njia ya mobile money au bank?😂😂😂 So Kodi gani huwa inakwepwa hapo?
Ujumbe wa malipo pekee hauchukuliwi kama risiti rasmi kisheria. Ujumbe huo ni uthibitisho wa malipo tu (payment confirmation) unaoonyesha kiasi kilicholipwa, tarehe, muda, na namba ya muamala. Risiti halali inapaswa kutolewa na muuzaji na iwe na maelezo muhimu kama:

1. Jina la kampuni au muuzaji
2. Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)ikiwa biashara imesajiliwa na TRA
3. Maelezo ya bidhaa au huduma iliyouzwa
4. Kiasi kilicholipwa pamoja na kodi zinazohusika (kama VAT)
5. Tarehe ya muamala
6. Sahihi au muhuri wa kampuni kwa biashara zinazohitaji.

Back
Top Bottom