Acha Kunichafua we msukuma nini😀Mambo Ya Zahoro Matelephone
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha Kunichafua we msukuma nini😀Mambo Ya Zahoro Matelephone
niwe serious kwa mambo ya kijinga kama uliyo posti??Kuwa serious basi mzee.
Zemanda ananichekesha sana, toka wajuba wampore manzi wake anatumind wanawake wote humu..!! 😹Ndio maana umegoma kutuma picha ya katress zako sio 😂 mdomo
Badala ya kunifariji unanicheka hivi ni kweli?Zemanda ananichekesha sana, toka wajuba wampore manzi wake anatumind wanawake wote humu..!! 😹
Nikajua kale ka ushamba kameisha kumbe bado wamemuingiza kwenye 18 watoto wa kkoo 🤣
Halafu ukaamua kuwaacha wakutapeli kienyeji hivyo? Au kuna hatua utazifuata kupata haki yako?MREJESHO:
Nimepata mawasiliano na m'miliki wa duka na baada ya kuongea nae akaniambia atalishughulikia hili swala bila shida akinielezea kuwa kiutaratibu wanatakiwa kucheki simu kama inashida gani kwanza na kupata ripoti ya fundi then ndipo waamue cha kufanya kwa mujibu wa ripoti ya fundi.
Baada ya kuzungumza nae Tarehe 2 mwezi February na kunipa ahadi hiyo,nikawa naendelea kumtafuta ili kunipa mrejesho kama amefikia wapi. Na katika hatua hiyo alipokea simu mara tatu akisema yupo busy na kazi na ameshindwa kufika dukani atakwenda siku inayofuatia.
Hili jambo likanipa mashaka sana kwasababu haiwezekani zipite siku tatu mtu hajakwenda dukani kwake. Mara ya mwisho kuzungumza nae tarehe 7 February,aliniambia ndio anaelekea dukani tuwasiliane jioni au kesho anipe mrejesho. Nilipiga simu jioni kuanzia saa moja jioni hadi saa nne usiku simu haipokelewi.
Niliendelea kupiga simu siku iliyofuatia pia hakupokea siku nzima. Leo sasa ikabidi niende tu pale dukani. Nikawakuta vijana wake na kuongea nao ambapo walionesha ushirikiano mdogo na walionekana kama kunikwepa hivi. Ilibidi niwaamuru kumpigia boss wao sababu simu yangu hapokei wakampigia na kumuuliza kuhusu swala langu akawajibu tu kuwa yeye alishazungumza na mimi na ameshanipa mrejesho jambo ambalo si ukweli sababu amekuwa hapokei simu zangu.
Akawaambia kuwa tatizo la simu yangu ni kuwa imekufa display na hiyo ndio ripoti ya fundi. Nikamwambia amuulize sasa nini kinatakiwa kufanyika sasa, akamwambia kuwa inatakiwa kununuliwa display yaani kioo kipya kwa gharama za mteja sababu warrant yao haibebi gharama ya manunuzi ya kioo kipya.
Sasa nikauliza kwa huyu muhudumu, mimi nahusika vipi na kununua kioo kipya cha simu wakati sijafahamu hata chanzo cha hiyo damage simu imezima tu bila sababu as if ilikuwa imekwisha chaji?
Sijawahi kuidondosha wala kuigonga wala kuipa damage yoyote,iwaje simu izime ghafla tu na kioo ndio kiwe tatizo?
Nikawaambia basi nitafutieni simu nyingine ambayo itareplace hii kwasababu mimi sijui hapa naanzia wapi ina maana nikiishia hapa na haya malekezo yenu tafsiri yake ni kuwa nilitoka nyumbani nikaja kununua simu kopo nikatupa pesa yangu then kirahisi tu niachane na hili swala liishie juu juu tu hivi?🤔
Wale vijana hawakuwa na majibu ya kunipa zaidi ya kusema "boss sisi hatuna maamuzi nje ya hapo maana mwenyewe ndio katupa hayo majibu".
Nimeondoka pale dukani nikiwa nimekasirika sana na kuchefukwa. Nimechukua ile simu ikiwa katika hali yake ya ubovu na kurudi home hadi hapa muda huu nawapa mrejesho hasira hazijaanisha.
Kioo kipya cha simu nimetazama hapa mitandaoni bei yake ni laki tano.
Kuna kitu kinaniambia huyu mwenye duka anajua anachokifanya. Hivi simu haijaanguka,haijagongwa popote,inakufaje kioo aisee?🤔
Sasa nataka nifanye maamuzi ya kupeleka hii kesi mahakamani ili tufanye kufuata taratibu za kisheria pengine yeye ataweza kuiambia mahakama kuwa ni kwa utaratibu upi simu inaweza kuzima tu halafu kioo kiwe ni tatizo then mteja ndie awajibishwe kwa tatizo ambalo sio physically inflicted kwenye hiyo simu?
Ni bora ningekuwa nimeidondosha au hata imeweka crack mtu anaweza sema ni sababu,yaani kioo hakiwaki kabisa na simu ukibonyeza power button inafanya kuvibrate bila reaction yoyote kwenye kioo sio mwanga waka kuonyesha chochote.
Hii kitu imenifundisha sana na kunipa umakini kimsingi kuanzia sasa sitathubutu kununua simu yoyote used au refurbished sababu naona kuna elements za utapeli na kukwepa kuwajibika kwa baadhi ya wauzaji ambao si waaminifu.