Wadau, kuna mahusiano gani baina ya mbu na sikio?

Wadau, kuna mahusiano gani baina ya mbu na sikio?

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wadau aiseee ebu wataalam waelezee kidogo uhusiano uliopo kati ya mbu na sikio manake mbu anataka damu so inabidi akungate sasa hii kulia sikioni yaani anauzi atazunguka koote atarudi sikioni ziiiiiiiii na sikioni hakuna damu sijui anataka nini
 
Niliona kuna post moja wanasema ile sauti ya mbu huitoa kama kukuzubaisha.

Yan kama unapigiwa kinanda ulale
Mwingine huyu ana lake👇👇
IMG_20210102_170637_498.jpg
 
Nifikiliavyo ni Kuwa na wenyewe ni waoga wa mabanzi so huwa wanaogopa mabanzi Sasa ili kutests kwanza Kama hapa mabanzi ni free au njemba imelala anakuja sikioni kukukera ukionyesha ishara upo active anatuliza mshono lkn akipiga kelele halafu bado upo cool hapo anajichagulia eneo la kukula kimasihara..

Kuna wale mbu wakorofi haswa ukiwa huna hela akikujua anaingia hadi sikioni anakupigia kelele wapuuzi sana wale..😂
 
Kazi ya sikio ni kusikia frequency range ambayo unaweza kuisikia...

Sasa zile kelele unasikia zinatokana na kasi ya mabawa yake kuchapa chini na juu kiasi kwamba yanatoa sauti hiyo nyembaba (udogo/ukubwa wa mabawa huchangia sauti kuwa ndogo au kubwa)...

Haina maana kwamba mbu anavizia sikio lako ili akufyonze damu
 
Kuishiwa ni kubaya sana.
Hata paka akipiga mihayo baada ya kuamka unaweza dhani amekuamkia
 
Wadau aiseee ebu wataalam waelezee kidogo uhusiano uliopo kati ya mbu na sikio manake mbu anataka damu so inabidi akungate sasa hii kulia sikioni yaani anauzi atazunguka koote atarudi sikioni ziiiiiiiii na sikioni hakuna damu sijui anataka nini
Sikio ni moja kati ya milango mitano ya fahamu katika mwili wa binadamu.
Kazi yake ni kunasa mawimbi ya sauti.

Mbu akiwa mbali na sikio, mawimbi ya sauti yake hayawezi kulifikia sikio, na hivyo huwezi kusikia sauti yake ingawa sauti yake ingalipo. Akirukaruka eneo la miguuni, huwezi kusikia sauti yake ingawa anatoa. Lakini mbu huyohuyo akiruka karibu na sikio, utaisikia sauti yake.

Hivyo sio sahihi kwamba mbu anatafuta sikio tu, bali huzunguka mwili mzima na akifika sehemu ya sikio mawimbi ya sauti hunaswa na kusikika.
 
Ni hivi! Mbu Ni mdudu mdogo ile sauti unayoisikia Ni jinsi anavyo flap mbawa zake sio analia au kuimba Kama ufanyavyo wewe!!

Sasa nikujibu sio kwamba anapenda sikio tu huwa anakuzunguka kuanzia chini mpaka juu Sasa akikuta kichwani hakuna blanket umelala kichwa wazi ataanza zunguka hapo kwenye kichwa na vile sikio lipo kichwani utasikia


Lakini akizunguka miguuni hata Kama umelala uchi hauwezi sikia milele
 
Back
Top Bottom