Wadau kupeleka barua Ubalozi wa China kuishinikiza Serikali yao isiunge mkono mradi wa EACOP, wasema kuna ukiukwaji wa Haki za Binadamu

Wadau kupeleka barua Ubalozi wa China kuishinikiza Serikali yao isiunge mkono mradi wa EACOP, wasema kuna ukiukwaji wa Haki za Binadamu

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Baadhi ya mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania pamoja na nchini Uganda wamekosoa vikali mradi wa Bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa zaidi ya kilomita 1400 kutokea nchini Uganda hadi Tanzania kwenye mkoa wa Tanga kwamba ulipitishwa katika Mazingira yasiyo shirikishi huku wakidai kunusa harufu ya ukiukwaji wa haki za Binadamu pamoja na upigaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Organization for Community Engagement, Richard Senkodo amedai kuwa licha ya mradi huo kudaiwa kuwa na tija kubwa kwa jamii ya kitanzania likini unaweka hatarini maisha ya watu wengi, huku akidai baadhi ya watu ambao wameachia maeneo yao kupisha mradi huo wamelipwa fidia kuduchi.
IMG_3279.jpeg

Akizungumzia suala hilo Mei 25, 2024 amesema "Moja ya athari kubwa ambazo zinatukwaza sana ni ukiukwaji wa haki za binadamu hasa watetezi wa haki za binadamu na wahifadhi wa mazingira wanapojaribu kuelezea changamoto mbalimbali ambazo huu mradi umeanza kuzionesha ambapo vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kuwanyamazisha na kuwakamata lakini hata ukitumia wale waathirika wenyewe wa bomba hawajapata zile faida kutokana na kile walichohaidiwa kila wanapojaribu kuomba stahiki zao ziweze kuboreshwa au kuwapa kwa wakati, hawataki kuwapa Serikali imekuwa ikitumia nguvu"

Kufuatia hoja hizo na nyingine ambazo amesema kuwa wamezifanyia tafiti kabla ya kuja na kampeini ya #STOPEACOP, ikiwemo suala la uchafu wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji amesema kuwa wanakusudia kupelekea barua maalumu kwenye Serikali ya China kuishinikiza Serikali ya China kutojihusisha na mradi huo.

"Tunakusudia kupeleka barua ambayo imesomwa nasisi pamoja na wenzetu wa Uganda kwa Serikali ya China ambako kwa nchini Tanzania tutaipeleka ubalozi wa China siku ya tarehe 27/5/2024, kwanini tuseme Serikali ya China, ni kwa sababu maendeleo ya huu mradi kwa sasa ambapo umefikia kutokana kubwa ambazo zimeanza kujitokeza hata kabla ya usafirishaji wa mafuta kuanza bomba limeshaonesha athari kubwa miongoni mwa athari hizo zinatofautiana kulingana na jamii husika "amesema Mkurugenzi huyo

Amesema kuwa suala la kupeleka barua kwenye Serikali ya China halitakuwa suala jipya kwa kuwa wamewai kufanya hivyo japokuwa barua hiyo iliishia kupokelewa na mlinzi. Lakini kwa nchini Uganda amesema kuwa wadau wamekuwa wakifanya hivyo pia hili kutuma ujumbe kwenye Serikali ya China.

Pia ameongeza "Katika kampeini hiyo (STOPEACOP ) tumeweza kuzishawishi benki kubwa 27 mpaka sasa zisiweze kutoa ufadhili kwenye hili bomba lakini pia makampuni 28 ya insurance tumeweza kuyashawishi yasiweze yasiweze kulihakikishia hili bomba usalama wa kusafirisha mafuta kutoka 𝗁𝗈𝗂𝗆𝖺 Uganda mpaka chongol𝖾𝖺𝗇𝗂 Tanga, Tanzania"

Baadhi ya wananchi waliodaiwa ni waathirika wa mradi huo kutoka Tanga na Dodoma, wamedai kuwa miradi huo umegusa shughuli zao za kiuchumi hususani kilimo na uvuvi.

Bausi Ramadhan ambaye Mkazi Chongol𝖾𝖺𝗇𝗂 Tanga ambaye anajishughulisha na shughuli za uvuvi amedai kuwa shughuli hizo zimekuwa ngumu kutokana na eneo la karibu ambapo awali shughuli hizo zilikuwa zikifanyika kuwekwa miundombinu ya mradi huo jambo ambalo kwa sasa linawapelekea kufuata samaki umbali mrefu licha ya kuwa na vifaa vyenye uwezo mdogo wa kwenda umbali huo.
IMG_3284.jpeg

Vilevile amedai kuwa fidia ambazo zilikuwa zikitolewa ni ndogo jambo ambalo linawafanya wananchi wengi kuwa katika mazingira ambayo hawelewi hatma ya kesho yao hasa kiuchumi.

Vilevile mkazi wa Dodoma ambaye amedai nae ni sehemu ya waathirika amesema kuwa maeneo ambayo wameyatoa kwa ajili ya mradi yalikuwa makubwa ikilinganishwa na fidia ambazo walipewa, ikidaiwa wengi walikuwa wanapewa kiasi cha T. Sh 300,000/= , kwa eneo la eka𝗋𝗂 moja na zaidi, jambo ambalo amesema kuwa kwa gharama hizo kwa wengi imekuwa vigumu kupata maeneo mapya ya kwa gharama za aina hiyo ili kuendesha shughuli za kilimo.

Aidha Mtaalamu wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi, Baraka Machumu ambaye amedai kuwa amekuwa akifuatilia huo mradi tokea mwaka 2017, amedai kuwa katika maeneo mengi ambayo amezunguka amekutana na changamoto ya ulipwaji fidia.

"Nimekuwa nikizinguka maeneo mengine kuanzia Kagera nimekutana na wananchi wengine pesa waliyolipwa inafanana kwa Tanzania utakuta mtu kuchukuliwa ekari moja kalipwa laki tatu yule ambaye ampona zaidi labda mwenye miti ndani yake, lakini tathimini umefanyika 2017 mtu anakuja kulipwa 2023 unaweza ukaona hapo hakuna usawa"amesema Baraka Machumu
IMG_3283.jpeg

Lakini imeelezwa kuwa Baraka Machumu, Richard Senkodo na wengine ambao wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu mradi huo kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipokea wito wa Polisi jambo ambalo wanalihusisha moja kwa moja na ukosoaji wa mradi huo, licha ya hivyo wamedai kuwa baadhi ya wananchi ambao wameonesha kutolidhishwa na stahiki mbalimbali walizopewa wamekuwa wakipewa wito na Polisi wa kuripoti mara kwa mara bila hata kupelekwa kwenye vyombo vingine vya kisheria.

Hata hivyo wamedai kuwa wanahisi uwepo wa harufu ya upigaji kwenye mradi huo kutokana na ripoti ya CAG kuonesha hilo kwenye mradi huo, pia wanadai kuwa wanapatwa na hisia hizo kwa sababu siku za hivi karibuni kwenye suala la mradi huo zimekuwa zikionekana sura zinazoleta wasiwasi zaidi.

Wadau hao wanadai wakati mradi huo unapitishwa hasa kwa nchini Tanzania ilikuwa vigumu kukosolewa kwa kuwa mazingira ya kuikosoa Serikali yalikuwa magumu na yenye hofu hususani kwa vyombo vya habari na Asasi za Kiraia.

𝖬𝖾𝗂 𝟤𝟧, 𝟤𝟢𝟤𝟦 𝖼𝗁𝗈𝗆𝖻𝗈 𝖼𝗁𝖺 𝗁𝖺𝖻𝖺𝗋𝗂 𝖼𝗁𝖺 '𝖳𝗁𝖾 𝖢𝗁𝖺𝗇𝗓𝗈' 𝗄𝗎𝗍𝗈𝗄𝖺 𝗇𝖼𝗁𝗂𝗇𝗂 𝖳𝖺𝗇𝗓𝖺𝗇𝗂𝖺 𝗄𝗂𝗅𝗂𝖼𝗁𝖺𝗉𝗂𝗌𝗁𝖺 𝗍𝖺𝖺𝗋𝗂𝖿𝖺 𝗒𝖾𝗇𝗒𝖾 𝗄𝗂𝖼𝗁𝗐𝖺 𝖼𝗁𝖺 𝗁𝖺𝖻𝖺𝗋𝗂 "Wananchi Hanang Watishiwa Kupewa Kesi ya Uhujumu Uchumi Wakidaiwa Kupinga Mradi wa EACOP. Wasisitiza Hawapingi Mradi"
 
Wendawazimu kabisa maendeleo yanakuja with cost, yani tuache mradi mkubwa wa maendeleo kama huu tiwasikilize wao? Au wametumwa na wakenya? Maana kenya alikuwa anautaka mradi huu kwa nguvu zote wajinga kabisa
 
Wazungu ni wapumbavu sana. Halafu hawajawahi kuficha shauku yao ya kuifanya Afrika kuendelee kuwa masikini.
 
Nadhani wanatumiwa na Kenya,ningekuwa kiongozi ningewachapa viboko kuanzia asubuhi hadi jioni kwa siku mia moja ishirini na tano.

Wapumbavu wa kiwango cha SGR.
 
Nadhani wanatumiwa na Kenya,ningekuwa kiongozi ningewachapa viboko kuanzia asubuhi hadi jioni kwa siku mia moja ishirini na tano.

Wapumbavu wa kiwango cha SGR.
Hawa enzi za magufuli wangejuta kuzaliwa huu ni uhujumu uchumi kabisa yani nchi tunahangaika kuleta miradi wao wanapewa vihela na washindani wetu watuhujumu, hawa sio wa kuwachekea
 
Back
Top Bottom