informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Baadhi ya mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini Tanzania pamoja na nchini Uganda wamekosoa vikali mradi wa Bomba la mafuta ghafi lenye urefu wa zaidi ya kilomita 1400 kutokea nchini Uganda hadi Tanzania kwenye mkoa wa Tanga kwamba ulipitishwa katika Mazingira yasiyo shirikishi huku wakidai kunusa harufu ya ukiukwaji wa haki za Binadamu pamoja na upigaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Organization for Community Engagement, Richard Senkodo amedai kuwa licha ya mradi huo kudaiwa kuwa na tija kubwa kwa jamii ya kitanzania likini unaweka hatarini maisha ya watu wengi, huku akidai baadhi ya watu ambao wameachia maeneo yao kupisha mradi huo wamelipwa fidia kuduchi.
Akizungumzia suala hilo Mei 25, 2024 amesema "Moja ya athari kubwa ambazo zinatukwaza sana ni ukiukwaji wa haki za binadamu hasa watetezi wa haki za binadamu na wahifadhi wa mazingira wanapojaribu kuelezea changamoto mbalimbali ambazo huu mradi umeanza kuzionesha ambapo vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kuwanyamazisha na kuwakamata lakini hata ukitumia wale waathirika wenyewe wa bomba hawajapata zile faida kutokana na kile walichohaidiwa kila wanapojaribu kuomba stahiki zao ziweze kuboreshwa au kuwapa kwa wakati, hawataki kuwapa Serikali imekuwa ikitumia nguvu"
Kufuatia hoja hizo na nyingine ambazo amesema kuwa wamezifanyia tafiti kabla ya kuja na kampeini ya #STOPEACOP, ikiwemo suala la uchafu wa mazingira hususani kwenye vyanzo vya maji amesema kuwa wanakusudia kupelekea barua maalumu kwenye Serikali ya China kuishinikiza Serikali ya China kutojihusisha na mradi huo.
"Tunakusudia kupeleka barua ambayo imesomwa nasisi pamoja na wenzetu wa Uganda kwa Serikali ya China ambako kwa nchini Tanzania tutaipeleka ubalozi wa China siku ya tarehe 27/5/2024, kwanini tuseme Serikali ya China, ni kwa sababu maendeleo ya huu mradi kwa sasa ambapo umefikia kutokana kubwa ambazo zimeanza kujitokeza hata kabla ya usafirishaji wa mafuta kuanza bomba limeshaonesha athari kubwa miongoni mwa athari hizo zinatofautiana kulingana na jamii husika "amesema Mkurugenzi huyo
Amesema kuwa suala la kupeleka barua kwenye Serikali ya China halitakuwa suala jipya kwa kuwa wamewai kufanya hivyo japokuwa barua hiyo iliishia kupokelewa na mlinzi. Lakini kwa nchini Uganda amesema kuwa wadau wamekuwa wakifanya hivyo pia hili kutuma ujumbe kwenye Serikali ya China.
Pia ameongeza "Katika kampeini hiyo (STOPEACOP ) tumeweza kuzishawishi benki kubwa 27 mpaka sasa zisiweze kutoa ufadhili kwenye hili bomba lakini pia makampuni 28 ya insurance tumeweza kuyashawishi yasiweze yasiweze kulihakikishia hili bomba usalama wa kusafirisha mafuta kutoka πππππΊ Uganda mpaka chongolπΎπΊππ Tanga, Tanzania"
Baadhi ya wananchi waliodaiwa ni waathirika wa mradi huo kutoka Tanga na Dodoma, wamedai kuwa miradi huo umegusa shughuli zao za kiuchumi hususani kilimo na uvuvi.
Bausi Ramadhan ambaye Mkazi ChongolπΎπΊππ Tanga ambaye anajishughulisha na shughuli za uvuvi amedai kuwa shughuli hizo zimekuwa ngumu kutokana na eneo la karibu ambapo awali shughuli hizo zilikuwa zikifanyika kuwekwa miundombinu ya mradi huo jambo ambalo kwa sasa linawapelekea kufuata samaki umbali mrefu licha ya kuwa na vifaa vyenye uwezo mdogo wa kwenda umbali huo.
Vilevile amedai kuwa fidia ambazo zilikuwa zikitolewa ni ndogo jambo ambalo linawafanya wananchi wengi kuwa katika mazingira ambayo hawelewi hatma ya kesho yao hasa kiuchumi.
Vilevile mkazi wa Dodoma ambaye amedai nae ni sehemu ya waathirika amesema kuwa maeneo ambayo wameyatoa kwa ajili ya mradi yalikuwa makubwa ikilinganishwa na fidia ambazo walipewa, ikidaiwa wengi walikuwa wanapewa kiasi cha T. Sh 300,000/= , kwa eneo la ekaππ moja na zaidi, jambo ambalo amesema kuwa kwa gharama hizo kwa wengi imekuwa vigumu kupata maeneo mapya ya kwa gharama za aina hiyo ili kuendesha shughuli za kilimo.
Aidha Mtaalamu wa mabadiliko ya Tabia ya Nchi, Baraka Machumu ambaye amedai kuwa amekuwa akifuatilia huo mradi tokea mwaka 2017, amedai kuwa katika maeneo mengi ambayo amezunguka amekutana na changamoto ya ulipwaji fidia.
"Nimekuwa nikizinguka maeneo mengine kuanzia Kagera nimekutana na wananchi wengine pesa waliyolipwa inafanana kwa Tanzania utakuta mtu kuchukuliwa ekari moja kalipwa laki tatu yule ambaye ampona zaidi labda mwenye miti ndani yake, lakini tathimini umefanyika 2017 mtu anakuja kulipwa 2023 unaweza ukaona hapo hakuna usawa"amesema Baraka Machumu
Lakini imeelezwa kuwa Baraka Machumu, Richard Senkodo na wengine ambao wamekuwa wakifuatilia kwa ukaribu mradi huo kwa nyakati tofauti wamekuwa wakipokea wito wa Polisi jambo ambalo wanalihusisha moja kwa moja na ukosoaji wa mradi huo, licha ya hivyo wamedai kuwa baadhi ya wananchi ambao wameonesha kutolidhishwa na stahiki mbalimbali walizopewa wamekuwa wakipewa wito na Polisi wa kuripoti mara kwa mara bila hata kupelekwa kwenye vyombo vingine vya kisheria.
Hata hivyo wamedai kuwa wanahisi uwepo wa harufu ya upigaji kwenye mradi huo kutokana na ripoti ya CAG kuonesha hilo kwenye mradi huo, pia wanadai kuwa wanapatwa na hisia hizo kwa sababu siku za hivi karibuni kwenye suala la mradi huo zimekuwa zikionekana sura zinazoleta wasiwasi zaidi.
Wadau hao wanadai wakati mradi huo unapitishwa hasa kwa nchini Tanzania ilikuwa vigumu kukosolewa kwa kuwa mazingira ya kuikosoa Serikali yalikuwa magumu na yenye hofu hususani kwa vyombo vya habari na Asasi za Kiraia.
π¬πΎπ π€π§, π€π’π€π¦ πΌππππ»π πΌππΊ ππΊπ»πΊππ πΌππΊ 'π³ππΎ π’ππΊπππ' ππππππΊ ππΌππππ π³πΊπππΊπππΊ πππ ππΌππΊπππππΊ ππΊπΊπππΏπΊ ππΎπππΎ πππΌπππΊ πΌππΊ ππΊπ»πΊππ "Wananchi Hanang Watishiwa Kupewa Kesi ya Uhujumu Uchumi Wakidaiwa Kupinga Mradi wa EACOP. Wasisitiza Hawapingi Mradi"