Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Date::11/24/2009Shamhuna,Khatib watia doa shangwe ya Karume, Maalim Seif
Na Salma Said, Zanzibar
Â
WAKATI Zanzibar ikiendelea kushangilia maafikiano ya kihistoria baina ya Rais Amani Abeid Karume na katibu mkuu wa CUF, Seif Sharif Hamad, juu ya uwezekano wa kuwepo kwa Serikali ya Mseto, mawaziri wawili wamejitokeza hadharani kutia doa shangwe hizo.
Wameeleza bayana kuwa Serikali ya Mseto si muhimu visiwani hapa.
Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Muungano), Mohammed Seif Khatib, wametofautiana na msimamo wa Karume ambaye alisema kuwa uamuzi wa kuwa na Serikali ya Mseto ni wa Wazanzibari wenyewe.
Tamko hilo la Karume alilitoa siku chache baada ya kukutana kwa faragha na Maalim Seif, ambaye baadaye aliitisha mkutano wa hadhara na kueleza kuwa CUF imeamua kumtambua rais huyo kwa kuwa kufanya hivyo kutarahisisha mazungumzo ya kutafuta muafaka.
Lakini Shamhuna, ambaye pia ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ), alisema Zanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa, bali kinachotakiwa ni kujenga utamaduni wa kukubali matokeo ya uchaguzi ya kushinda na kushindwa.
Alisema hayo katika kipindi cha âHarakati za Kisiasaâ kinachorushwa hewani kila siku ya Jumanne na kituo cha redio cha Zenji FM, ambacho kinamilikiwa na Waziri Seif.
Tamko hilo la Shamhuna lilirudiwa kwa siku tatu mfululizo; Jumapili, Jumatatu na jana asubuhi, kuonyesha kuwa hakuna haja ya ajenda hiyo ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwenye mazungumzo ya muafaka baina ya vyama hivyo viwili vikuu visiwani Zanzibar.
Â
âZanzibar haihitaji Serikali ya Mseto wala Serikali ya Umoja wa Kitaifa wala serikali ya nini hapana, la msingi ni tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa na kushinda... tukijenga utamaduni huo tutafanya kazi kwa pamoja na rais atakayeingia madarakani atachagua watu wenye uwezo wa kufanya kazi,â alisema Shamhuna.
Â
Shamhuna alisema watu wengi wanafikiri kwamba suluhisho la mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ni kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa na serikali hiyo ndio itakayoweza kuondoa matatizo yaliyopo, lakini hilo sio sahihi kwa kuwa hata ikiundwa serikali ya umoja matatizo bado yataendelea kuwepo.
âMasuala yaliyopo yanatokana na baadhi yetu kuweka mbele umimi na si utaifa kwa hivyo kuundwa au kutokuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa hakutusaidia,â alisema.
âKadiri umimi utakavyokuwepo miongoni mwetu wana siasa, tatizo bado litaendelea. Solution (suluhisho) ni kuondoa umimi. Hakuhitajiki hotuba wala hakuhitajiki mikutano, kunataka management,â alisema Shamhuna kwa kujiamini.
Shamhuna alikwenda mbali zaidi na kusema watu wanasahau kwamba Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi na wanadhani kwamba ni nchi ya watu kupiga kura na kutangazwa tu huku wengine wakifikiri kuwa Zanzibar ni nchi yenye watu walegevu legevu.
Â
Lakini hakufafanua anamaanisha nini, ingawa suala la mapinduzi limekuwa likizua mgogoro baina ya wafuasi wa vyama hivyo viwili, baadhi wakipinga mapinduzi hayo na wengine wakiunga mkono.
Akizungumzia urais, Shamhuna alisema Zanzibar haihitaji rais kijana wala mzee, lakini inahitaji rais meneja ambaye ataweza kuwakusanya watu wote pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo sasa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Â
âKarume anamaliza muda wake; nikiulizwa tunataka rais wa aina gani nitajibu tunataka rais meneja (kiongozi) sijui nimefahamika,â alisema waziri huyo machachari.
âKwa hapa tulipofikia, tunataka tuwe na kiongozi meneja na sio lazima awe kijana kama wengi mnavyodhani. Zanzibar hatutaki rais kijana wala mzee, tunataka meneja ili aweze kuondoa challenges (changamoto) zote...sasa nani ana quality (ubora) ya umeneja,â alihoji.
Â
Alisema rais wa aina hiyo atachagua watu wenye kuweza kufanya kazi hata bila ya kujali ametoka wapi.
Â
âSio huyu anatoka wapi na huyu anatoka wapi watu ni inclusive government (serikali inayojumuisha) na sio idadi ya watu kutoka chama cha siasa... tufanye hivyo kwa matakwa yetu na sio kulazimishwa, hapo tutajenga umoja na tutafanya kazi.â
Â
Shamhuna alisema mbio za urais kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2010 tayari zimeshaunda makundi zaidi ya matatu na kwamba tayari wapo watu wameshaanza kupigia debe viongozi wao. Alisema watu hao wameanza kutoa lugha za vitisho kuwa mgombea wa kundi lao asipopitishwa na CCM, hawatakipigia kura chama hicho.
Â
âTunawasikia wanasema hivyo wengine wanasema sasa ni zamu yetu; wengine wanasema sisi vijana tuchagueni ili tufanye mabadiliko ya nchi; wengine wameamua kunyamaza kimya; tegemeo lao hatulijui. Sasa tuna makundi matatu mpaka manne hivi yanayotafuta urais wa Zanzibar,â alisema Shamhuna. Â
Â
Akizungumzia suala linalopendekezwa na baadhi ya watu kuwa safari hii rais atoke Pemba ili kupunguza joto la kisiasa, Shamhuna aliwaita watu wenye mapendekezo hayo kuwa wamefilisika kisiasa.
Â
âZanzibar hatuchagui rais kwa zamu na suala la kusema sasa zamu yetu Wapemba; zamu yetu  Waunguja limekwisha. Hiyo ni hoja batili na anayezungumza lugha hiyo sijui nimuite kwa lugha gani,â alisema Shamhuna.
Â
âRais Amani anaondoka na Rais Kikwete anaendelea kipindi cha pili na hapa mitazamo tofauti kwa kuwa anayeondoka anataka arithiwe na ni nani huyo wa kurithi?
âMuungano unataka apatikane mtu kutoka Zanzibar ambaye ataweza kufanya naye kazi hivyo ndio mitizamo miwili ya msingi hii, mitizamo ya kuwa anatoka Pemba au Unguja ni mitizamo ya umimi na huko ni kufilisika kisiasa kwa jinsi navyoangalia suala hilo haraka haraka.â
 Â
Naye Waziri Seif, ambaye anatajwa kama mmoja wa watu wanaoweza kujitokeza kuwania urais wa Zanzibar, aliwaambia wananchi wa kisiwani Pemba wiki hii kwamba umoja wa Wazanzibari hauhitaji kushirikishwa chama kingine chochote kwa kuwa CCM pekee inaweza kuweka umoja na mshikamano kwa kuwa hiyo ndio sera ya chama hicho.
Aliwaambia wananchi wa kisiwa hicho kwamba MwanaCCM wa Pemba anakuwa ni CCM wa kweli kweli kwa kuwa wanakabiliana na mambo mbalimbali yanayofanywa na wapinzani, lakini wameweza kumudu na kuvumilia bila ya kutoka katika chama hicho.
âNikwambieni ndugu zangu kuwa katika suala la umoja hakuna haja ya kushirikiana na chama kingine kwani CCM wenyewe tunaweza sana kuwaunganisha Wazanzibari wote. Na huku Pemba, CCM anakuwa wa kweli kweli maana vitimbi na vituko anavyofanyiwa na wafuasi wa CUF ni vingi, lakini bado anaweza kubakia kuwa CCM, hilo si jambo dogo,â alisema Khatib katika kipindi kilichorushwa na Zenj FM wakati wa ziara yake kisiwani Pemba.
Hii ni mara ya pili kwa Waziri Shamhuna kupingana na viongozi wakuu wa nchi katika kipindi cha miaka mitatu. Oktoba 5, 2006 Shamhuna alipingana na Rais Kikwete kuhusu suala la mwafaka wa Zanzibar.
Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema utatuzi wa mpasuko wa kisiasa Zanzibar umefikia mahali pazuri, Shamhuna, aliibuka na kusema kamwe serikali ya umoja wa kitaifa au ya mseto haitaundwa visiwani.
Shamhuna alitoa msimamo alipokuwa akiwahutubia viongozi wa ngazi mbalimbali na wazee wa CCM wa Kikombweni Wilaya ya Kaskazini A, Unguja na hotuba hiyo kutangazwa na vyombo vya habari vya SMZ.
 "Hakuna Serikali ya Mseto itakayoundwa nchini kama inavyodaiwa na viongozi wa chama cha upinzani," alisema Shamhuna.
Facebook

Tuma maoni kwa Mhariri